Lori likiondoa gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyogongana na basi la abiria la Moro Best maeneo ya Ruvu Darajani ambapo mtu mmoja ambaye ni dereva wa Land Cruiser anasadikiwa amefariki dunia hapohapo. Mashuhudu wameiambia Globu ya Jamii eneo la tukio kwamba ajali hiyo imetokea mara tu baada ya msafara wa Mama Salma Kikwete uliokuwa unatokea Dar kupita mbele kidogo ya daraja la Ruvu ndipo ajali ikatokea, ambapo hilo basi likitokea Morogoro kwanza liliipamia Hiace kwa nyuma kabla ya kurudi barabarani na kupambana na la hilo Land Cruiser ambalo insemekana lilikuwa kama gari la nne hivi nyuma ya msafara wa Mama Kikwete ambaye hakudhurika. Juhudi za kumpata msemaji wa polisi kwa maelezo rasmi ya kina zinaendelea na tutawapasha
Wakaazi wa Ruvu wakiangalia gari lililopata ajali
Askari wa usalama barabarani na wananchi eneo la tukio
Basi la Moro Best likiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
Picha na mdau wa Globu ya Jamii





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ajali za barabarani zitatumaliza. ajali ni zinazotokea ni nyingi sana japokuwa zinaweza kuepukika. Hivi ni lini hawamadereva hasa wa mabasi watathamini uhai zaidi ya kufika haraka????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...