Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya SMS Kati ya Wananchi wa Bumbuli na Mbunge wao, Ndugu January Makamba, yamezinduliwa tarehe 29 Januari 2011 kwenye Semina Elekezi aliyoitisha Mbunge huyo kwa viongozi na watendaji wa vijiji na Kata wapatao 250 wa Jimbo la Bumbuli.

Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika.

Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu.

Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi.

Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana.

Mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu imewezesha kufanya gharama ya huduma hii iwe "at cost" na hivyo Mbunge bado kuwa na uwezo wa kuigharamia kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - lakini kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).

Kwa habari nyinginezo tembelea tovuti ya Mbunge:

http://www.januarymakamba.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sasaaa, Mbunge kwa sasa si wa wote au wa CCM? Nilifikiri mambo ya chama yanakaa kando sasa Mbunge anatujumuisha wananchi wote wa Bumbuli au hio jezi aliovaa haina rangi ya chama chake? Ila nasifu huu mfumo wa kupata maoni na habari kutumia short code.

    ReplyDelete
  2. Wazo ni zuri lakini lingeweza kuboresha kuwa na maana zaidi kama hizo SMS za bure zingekuwa za kumwezesha mwananchi moja kwa moja kupata huduma ya dharura mfano kwenda: Fire brigade, Police, Ambulance, Takukuru n.k

    Kuwakilisha kero kwa Mbunge si lazima iwe jambo la dharura na pengine kiutekelezaji uwasilishaji huo huwa unahitaji maelezo marefu ya Kero kuliko ujumbe wa SMS. Nasema huduma ya dharura ielekezwe kunakohusika moja kwa moja na sio kupitia kwa mtu maana udharura utapoteza maana.

    ReplyDelete
  3. Ukisoma Bio yake utampenda! I suggest you to read please and you will end by wishing him to be our 2015 president of United republic of Tanzania! Gombea gombea unafuture kwa waTz!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana kwa huduma hii. Mimi ninashauri na wabunge wengine waige jambo hili na ikiwezekana litengewe budget ni njia nzuri ya kuelewa kero na kuzitatua

    ReplyDelete
  5. Wazo zuri na huenda likawanufaisha wananchi wa Bumbuli.Nisichokijua ni idadi ya wananchi wa Bumbuli wenye simu.Je kwa wale ambao hawana simu,alternative yao ni nini?

    Pili sidhani kama yeye kama Mbunge hazijui kero za wananchi wake.Alipogombea bila shaka alishazifanyia uchunguzi kero zinazowakabili watu wa Bumbuli na tayari alikuwa na mipango ya kuzitatua.Sasa je anahitaji kuendelea kukusanya maoni na kero za wananchi?Sijui.

    Tatu lipo suala la kujiuliza;Mbunge huyu anapata wapi fedha ya kulipia huduma hii?Kama ni ubia ambao ameingia na makampuni ya simu ni kwa manufaa gani ya kibiashara?

    ReplyDelete
  6. good idea mie ni mwananchi wako na nimependezwa na jambo hili, keep it up kijana sie ndio tunajua umuhimu wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...