TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



SHEREHE ZA SIKU YA SHERIA NCHINI (LAW DAY) MWAKA 2011

MAHAKAMA YA TANZANIA INATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA (LAW DAY) NCHINI MNAMO TAREHE 02.02.2011.

SHEREHE HIZI AMBAZO ZINAADHIMISHWA NA MAHAKAMA NCHI NZIMA ZINAASHIRIA MWANZO WA SHUGHULI ZA MAHAKAMA MWAKA 2011

MSAJILI WA MAHAKAMA YA RUFANI, ANAPENDA KUWATAARIFU WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KUWA KAULI MBIU YA SHEREHE ZA MWAKA HUU NI:

“UMUHIMU WA ELIMU KUHUSU MAHAKAMA KAMA HATUA YA MSINGI YA UTATUZI WA MGOGORO KATIKA JAMII.”

MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE.

KWA HAPA DAR ES SALAAM SHEREHE HIZO ZITAADHIMISHWA MBELE YA JENGO LA MAHAKAMA KUU (KIVUKONI FRONT) SAA 02:00 ASUBUHI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii taarifa ingetolewa mapema na kwenye vyombo vingi zaidi na ingefafanua ufungwaji wa barabara kwa ajili ya shughuli hii ili watumiaji wa barabara wajipange kutumia njia mbadala.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...