Katika mkutano wake mkuu wa mwaka uliofanyika Disemba 11, 2010 katika hoteli ya MovenPick jijini Dar es Salaam Chama cha Teknolojia ya Habari Tanzania (TITA) pamoja na mambo mengine ulimchagua Profesa Faustin Kamuzora wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa mwenyekiti wa TITA, awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dr. Jabiri Omari wa Chuo Kikuiu Huria cha Tanzania ambaye sasa anakuwa makamu mwenyekiti wa TITA.
Katika mkutano huo wajumbe waliochagua kuwa wajumbe wa kamati kuu ya TITA ni na taasisi wanazotoka zipo kwenye mabano; Bw. Peter Mayala (Mamlaka ya Mapato Tanzania), Bw. Mayala pia ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa TITA, Bi. Kalunde Kisesa ambaye anakuwa mweka hazina (Mamlaka ya Mapato Tanzania) na Bw. Adam Mambi (Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania) ambaye ameteuliwa kuwa Makamu Katibu Mkuu.

Wajumbe wengine wa kamati ya utendaji ni Bw. Said Masimango (National Social Security Fund), Bw. Mulembwa Munaku (Chuo Kikuu cha Dar Dar es Salaam), Bi. Elizabeth Mkoba (Mamlaka ya Elimu Tanzania), Bw. Frank Goyayi (FTS Service Ltd), Bw. Joseph Nyansiro (Wizara ya Maliasili na Utalii) na Bw. Arbogast Fabian (Chuo Kikuu cha Aga Khan)
TITA ilianzishwa mwaka 2002 ili kuweza kukabili changamoto inazojitokeza katika Telnolojia ya habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) chini Tanzania. Lengo la TITA ni kuhakikisha inakuza taaluma ya TEKNOHAMA na kulinda haki za watumiaji TEKNOHAMA.
TITA inahamasisha wanataaluma ya TEKNOHAMA, waajiriwa, waajiri na watu wanaopenda TEKNOHAMA nchini Tanzania kuungana ili kuhakikisha sekta hii inakuwa na kuwa chachu ya maendeleo ya watanzania.
• Kwa mawasiliano zaidi tembelea www.tita.or.tz
• Kwa wale wenye nia ya kujiunga na TITA wanaweza kupiga simu namba 255 784 601164 or 0715 60 1164 au watume barua pepe kwenda info@tita.or.tz
Bw. Peter Mayala
Katibu Mtendaji TITA

Hongereni sana viongozi wapya wa TITA na shukran nyingi kwa wale waliomaliza muda wao. Ndoto zetu kuhusu TITA zinatimia taratibu.
ReplyDeleteMdau Deogratias Nondi
Edmonton, Canada
A very good team - congratulations to everyone!
ReplyDeleteDS.
Kwa kweli hizi ni pongezi stahili kwa hatua hii iliyofikiwa. We started as small meetings at UDASA. Now, wow!!! Kudos to all.
ReplyDeleteJustice Faustin
Dar es Salaam
Hongereni nyote kwa kuchaguliwa kuongozi asasi hii muhimu!
ReplyDeleteAndrew Kwayu
Kilimo