Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akitia sahini Mkataba wa CCARDESA ofisini kwake leo.

Na Issa Sabuni

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa, Profesa Jumanne Maghemba leo ametia sahini kwa naiaba ya Tanzania ili kuridhia mkataba wa mahusiano ya Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kwa nchi Wanachama Kusini mwa Afrika (SADC) ili kushirikiana katika Tafiti na Maendeleo katika sekta ya kilimo (The Centre for Coordination of Agricultural Research and Development for Southern Africa- CCARDESA)

Mkataba huo una lengo la kutambua uwezo wa Watafiti wa ndani katika sekta ya kilimo lakini pia unatoa fursa kwa Watafiti kutatua matatizo ya wakulima wa nchi Wanachama wa Jumuia hiyo ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

Nchui nyingine zilizotia sahini ya kutekeleza Mkataba huo ni pamoja na Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lesotho, Madagascar, Malawi na Mauritius.

Nyingine ni Msumbiji, Namibia, Afika Kusini, Swaziland Zambia na Zimbabwe, Mauritius ni nchi pekee ambayo bado haijasahini Mkataba huo.

Waziri Maghembe kabla ya kusaini Mkataba huo alisema hii ni fursa ambayo itakuza mahusianao ya nchi wanachama kwenye sekta ya kilimo katika juhudi za kukifanya kilimo kiwe cha tija kwa kuzalisha chakula cha kutosha ambacho kilisha familia na ziada itauzwa ili wananchi waondokane na umaskini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wanaoridhia mikataba ni Bunge tu. Maghembe atakuwa amesaini tu. Na baada ya hapo Bunge ndo liridhie kama kuna ulazima. I hope I am clear.

    ReplyDelete
  2. Msaada unasomwa kwa nusu saa??..aaaaa...mikataba hii????? Mawakili wako wapi hapo?Mambo yakivurugika ndio wanatafutwa baadaye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...