Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kulia) akizungumza jambo kwa msisitizo leo wakati akitangaza safari ya mikoa mitano kwa wasanii walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards katika ukumbi wa mikutano kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).Katikati ni Mratibu wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kutoka Basata,Angelo Luhala na kushoto ni Mkurugezi wa Prime Time Promotions,Godfrey Kusaga.
Mratibu wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kutoka BASATA,Angelo Luhala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na vile watakavyokuwa pamoja na wasanii wa muziki walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards katika safari yao ya mikoa mitano hapa nchini.Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na kushoto ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotions,Godfrey Kusaga.
Mmoja wa wasanii watakaokuwepo katika safari hiyo,John Simon a.k.a Joh Makini akizungumzia safari itakavyokuwa kwa niaba ya wasanii wenzake wote.

Baada ya Mchakato wa Tunzo za Muziki za Tanzania zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards zilizokuwa na mafanikio makubwa Mwaka huu, Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Kilimanjaro premium Lager imeona ni vyema kuwapa fursa Wasanii walioibuka washindi pamoja na baadhi ya wateule kufanya matamasha ya muziki katika baadhi ya mikoa ya Tanzania kama ishara ya shukrani kwa wapiga kura wao.


Wasanii wa Muziki walioibuka Washindi wa Tunzo za 2011
1. 20%
2. Mapacha Watatu
3. Mpoki
4. Joh Makini
5. Hard Man
6. C Pwaa
7. Khalid Chokoraa
8. Lady Jay Dee
9. Linah
10. Barnaba
11. JCB
12. Jahazi Modern Taarab
13. Ben Po
Baadhi ya Wateule
1. Godzilla
2. Sam wa Ukweli
3. Mwasiti
4. Mataluma.
Wawezeshaji:

Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kufanya kazi na makampuni mbalimbali katika katika kufanikisha safari hizi . Makampuni haya ni pamoja na:

1. Prime Time Promotion – Wasimamizi wakuu wa safari za Mbeya, Dodoma, Mwanza na Moshi.
2. Entertainment Masters – Wasimamizi wa Shughuli ya Dar .

Mwaka huu Kilimanjaro kama mdhamini imeamua kuwarudishia wadau na wapenzi wa muziki wa Tanzania Safari za Shukrani.
Kwa Tamasha la Jumamosi Viwanja vya Posta Kijitomasha hapa Dar es salaam litasindikizwa na Wateule wa wimbo bora wa Afrika Mashariki Radio and Weisal pamoja na Bebe Cool kutoka Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...