Na Ally Kondo, London

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) ameainisha baadhi ya changamoto anbazo Serikali inakabiliana nazo tangu ilivyoanza mchakato wa kuwahamasisha Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) kushiriki katika kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Waziri Membe alianisha changamoto hizo wakati akihutubia mkutano wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Uingireza tarehe 07 Mei, 2011. Waziri alieleza kuwa, moja ya changamoto hizo ni kujua idadi kamili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Katika kujaribu kutatua tatizo hilo, Membe alizielekeza Balozi na vyama vya watanzania wanaoishi ughaibuni kubuni mikakati itakayowezesha kupata idadi kamili ya watanzania wanaoishi nje. Waziri Membe aliagiza jukumu hilo litekelezwe katika kipindi cha mwaka mmoja.

Alieleza kuwa, sababu ya yeye kuja London kuhudhuria mkutano huo ni kukusanya hoja kutoka kwa wadau hao ili ziweze kusaidia suala la Diaspora kupelekwa Bungeni na hatimaye kuingia katika Katiba.

Waziri Membe alieleza kuwa, changamoto nyingine ni kwamba watu wengi hawafahamu vizuri maana ya Diaspora na kueleza kuwa, jitihada za makusudi zinahitajika kueleimisha umma kuhusu maana kamili ya neno Diaspora.

Akifafanua maana hiyo, Membe alieleza kuwa Diaspora ni walowezi wa Kitanzania wanaoishi nje ya nchi na kwamba bado wanajitambulisha kama Watanzania. Alisisitiza kuwa, wanafunzi wanaosoma nje ya nchi katika kipindi cha masomo yao iwe miaka miwili au mitatu hao sio Diaspora.

Waziri Membe pia aligusia suala la uraia pacha. Alieleza kuwa, nchi zinazoruhusu uraia pacha zimewafanya watu wao kupata kazi nzuri zenye mishahara mikubwa na hivyo kuwawezesha kutuma wanapotoka fedha nyingi.

Changamoto nyingine ambayo Waziri Membe aliitaja ni kubuni utaratibu bora wa kuwashirikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni kuchangia maendeleo ya nchi yao. Alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuzisawishi asasi mbalimbali kuhudhuria mikutano ya Diaspora. Kwenye mikutano hiyo asasi hizo zitafafanua fursa za kiuchumi zinazopatikana nyumbani ili jumuiya ya Diaspora ipime yenyewe kuendelea kukaa nje au kurudi nyumbani kutumia fursa hizo.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuwa na jarida la Diaspora litakalokuwa na taarifa zinazojiri nyumbani na nje ya nchi. Jarida hilo litasaidia kuwaunganisha watanzania walio nyumbani na wale wa nje ya nchi kuhusu taarifa mbalimbali zenye maslahi kwao.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walipata fursa ya kutoa mawazo yao mbele ya Waziri. Mjumbe mmoja alipendekeza kuwe na kituo maalum cha kuratibu masuala ya Diaspora kama vile Kituo cha Uwekezaji kinavyoratibu masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.

Aidha, mjumbe mwingine alishauri wakati wa Sensa inayotarajiwa kufanyika mwakani kubuniwe maswali ambayo yatawezesha kujua idadi ya watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Wazo la kuanzisha kumbukumbu mkeka (database) ya ujuzi na fani walizonazo watanzania wanaoishi nje ya nchi lilitolewa. Kumbukumbu mkeka hiyo itumike wakati Serikali au asasi za kiraia kupata watu wanaowahitaji zinapotokea nafasi za kazi. Hii pia izingatie kuanisha kazi maalum kwa ajili ya jumuiya ya watanzania wanaoishi ughaibuni.

Mkutano wa Diaspora unafanyika kwa mara ya tatu nchini Uingereza ambapo mwaka huu wajumbe takriban 55 kutoka sekta ya umma na sekta binafsi wanahudhuria mkutano huo wakiwamo wabunge wawili pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2011

    Je wapigabox waliruhusiwa kuhudhuria na walifika?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2011

    Mmoja ya Kitu cha msingi kwetu wa-TZ tunaishi nje ya nchi ni DUAL CITIZENSHIP. Wenzetu Kenya na Uganda wameisha pitisha.GOD BLESS TZ.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2011

    HASHIM SWDEN?
    NASHUKURU KUPATA TAARIFA HII KWENYE MTANDAO WA BWANA MICHUZI, LAKINI HOJA NI KWAMBA JEE WATANZANIA WANAOHITAJIKA KATA KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA NI WALE WANAOISHI UK PEKEE AU NI WOTE WANAOISHI UGHAIBUNI? SSA SSIS WENGINE MBONA HATUKUALIKWA NA HALI TUMEJIANDIKISHA KWENYE BALOZI ZETU? BAADA YA KUSOMA HABARI HII NILIWASILIANA NA WADAU WENGINE NIKAWADOEZA HABARI HII, TUMESIKITISHWA SAAAAANA NA HALI YA KUTOOPEWA FURSA YA KUHUDHURIA MKUTANO HUUUUU. AKINA DIASPORA TUKO WENGI SANA HAPA EUROPE. NINGEOMBA WADAU WAANDAE UTARATIBU WA KUPEANA HABARI MAPEMA ILI TUWEZE KUHUDHURIA KWA WINGI NA UMOJA PIA MSHIKAMANO. MAANA MADA HII INATUHUSU WOTE,
    AHSANTE.

    ReplyDelete
  4. Mdau uliyesema kwamba hukualikwa, sidhani kama unamaanisha ulitaka utumiwe barua binafsi ya mwaliko. Habari za kuhusu mkutano huu wa Diaspora zilikuwepo katika blog hii ya jamii kwa siku nyingi tuu kabla ya mkutano wenyewe.
    Kuhusu UK, ni kwamba wote tunaelewa historia ya nchi yetu na UK. Ingawa siyo historia nzuri, lakini bado ni historia. Historia hii ndiyo inayofanya UK iwe na watanzania wengi kuliko nchi zingine za Ulaya, na hivyo basi, "by default", UK imekuwa ndiyo kitovu cha watanzania walowezi wa Ulaya. Ingawa hii haina maana kwamba watanzania wa UK ni muhimu kuliko watanzania wa nchi zingine za ulaya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2011

    MPEVU asante sana kaka UMESOMEKA fullstop.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2011

    Kwa mara ya kwanza nimehudhuria London Diaspora 3, nimefurahishwa na conference nzima kwani ni moja ya chombo muhimu sana ambucho watu wanachangia hoja kwa uwelewa wa juu sana kwani haiangalii uchama bali ni kwa maendeleo ya nchi.
    Binafsi ninashauri Serikali iangalie umuhimu wa kuunda Diaspora kama chombo kisichounga upande wowote wa kichama, na iwatumie wana Diaspora kuwa ni source for economic policies. Inasikitisha report iliyotolewa na mtu wa BOT is very biased haizingatii International Macroeconomic na hii ni kwa sababu BOT is not an independent institution! therefore every report must support country political situation. My suggestion is that we must have a further vision for Diaspora Unit and might have a big impact to our economy only if it wont be associated with any side politically.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2011

    Mmesikia BBC Swahili kuna nchi za kina burundi zinataka kugoma kupitisha mizigo pale dar kwa ajili ya utapeli?habari inakuja mkuu akizidi kuwahamasisha diaspora.kwa kweli ieleweke bandari na TRA ni sehemu nyeti kwa nchi hasa inapotuhitaji sisi diaspora.Tuige Rwanda jamani wenye dhamana wawe responsible.Kagame hamtazami mkwamisha maendeleo usoni mara mbili Bongo vipi tunatawaliwa na ujanja ujanja tu?binafsi mwaka jana nilipitia Rwanda maendeleo unayaona nje si kwenye mitandao.Tuweni wakali na wakwamisha maendeleo ya nchi yetu tumsupport Raisi wetu yuko seriouse ila aige kuwajibisha bila kutazama usoni otherwise tutakaa diaspora miaka dahari tunapigia ngoma majini

    ReplyDelete
  8. everybodyMay 08, 2011

    Mimi sikuweza kuhudhuria Diaspora kwa sababu nilikuwa na udhuru kidogo. Ila napenda kutoa maoni yangu kidogo kwenye hili swala la Dispora na maendeleo ya Tanzania. Kwanza ningependa kuishauri Serikali chini ya muheshimiwa Rasi Kikwete kwamba huu sio wakati wa siasa na maneno yasioyokuwa na utekelezaji. Nakumbuka (kama kumbukumbu zangu zipo vizuri) rais alishawahi kusema wakati akiwa US miaka ya nyuma kwamba "watanzania walioko nje wanaonea wivu watanzania wa bong ndo maana wanataka uraia wa nchi mbili". Samahani kama nitakuwa nimenukuu vibaya ila tafsiri yake ndo hiyo. Sasa kama Tanzania kweli ipo serious kwa maendeleo yake ni bora ikaruhusu hili swala la uraia wa nchi mbili. Wenzetu Kenya wameshalipitisha hili na katika hii East African Community wao watakuwa wanabenefit zaidi kwa sababu wanayo access kwenye market ya Tanzania and at the same time Wakenya waliopo nje ya nje wanauhuru wa kufanya investment nchini kwao. Jamani viongozi wetu wa Tanzania, tusidharau wananchi walipo nje. Huku nje ya nchi (mfano UK nilipo mimi) hata mfanyakazi wa ndani anapata hela inayomwezesha walau kujenga kajumba ka kawaida bongo na kupangishia na serikali kupata mapato kupitia property tax. Naishauri serikali iharikishe mchakato wa kuwaruhusu watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi ili kupata mapato ya wanzania walio nje ya nchi. Kwa sasa inaonekana kama watanzania walio nje ya nchi wana tamaa lakini tuangalie mbeleni hili swala ni kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla wake. Tuambiane ukweli ni kwamba mwisho wa siku kama mimi naishi nje ya nchi na serikali hairuhusu uraia wa nchi mbili ili kuniwezesha kufanya investment popote Tanzania ninapotaka mwisho wa siku nitakuwa naifikiria familia yangu tu na ndugu zangu waliopo Tanzania. Lakini tukiangalia kwa mapana watanzania tuliopo nje tunaweza kufnaya investments kwa udogo wake ambazo zitaweza kutoa ajira kwa watanzania wenzetu. WAKUU WA SERIKALI EMBU LIANGALIENZI HIL KWA UPESI JAMANI...Hata kama Serikali itaendelea kuuzuia uraia wa nchi mbili, ukweli ni kwamba Tanzania haina Ajira za kutosha kuwashawishi watanzania waliopo nje kurudi. Alternative itakuwa kwa hao watanzania waliopo nje kujilipua(kuukana uraia wa Tanzania) na kuchukua uraia wa nchi walizopo. Hivyo basi serikali itafakari hili swala na kulifanyia maamuzi kwa haraka. Poleni kwa kuwachosha kusoma ila ni mtazamo wangu tu kwa maendeleo ya Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...