Wiki kadhaa zilizopita, nikiwa Madison, katika mkutano wa Peace Corps, niliingia katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison. Nilifurahi kuingia katika maktaba hii, ambayo niliizoea wakati nasoma katika chuo hicho, 1980-86.

Niliangalia vitabu vya ki-Swahili, ambavyo ni vingi katika maktaba hii, nikavutiwa na vitabu vya Someni Kwa Furaha, tulivyosoma tulipokuwa shule ya msingi.

Nilijikumbusha kuhusu Bulicheka na mke wake Lizabeta, Wagagagigikoko na mfalme wao, Makari Hodari, Kalumekenge, na Pauli mwenye mikono michafu.

Tulibahatika, enzi za utoto wetu, kuwa na vitabu vya kusisimua, vilivyotupa motisha ya kusoma. Vitabu hivi viliandikwa kuzingatia umri wetu. Walimu walikuwa makini, katika kufundisha, kwa mbinu mbali mbali, kama vile nyimbo. Tuliimba alfabeti hadi orodha. Nawasifu na kuwashukuru waalimu wale.



Mtembelee Profesa Mbele BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2011

    Yaani Prof.umenigusa kweli..ni majuzi tu nilikuwa najaribu ku-recall maisha ya utoto wangu nikawa nakumbuka zile nyimbo za "Pauli/o usije kucheza na mimi..uuna mikoono michaaafu..!Sijui heee YAKOOBOO..heee YAAKOBOO amka twende shule..amka twende shule...haaya njoo,haaya njoo.!!!Elimu ya siku hizi"siyo".

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2011

    Thanks Prof kwa kuturudishia miaka yetu nyuma kwa miaka arubaini na ushei.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2011

    Tumbo niache nimwachie Manenge uji....

    wadau kilikua kitabu gani hicho....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...