Mchezaji maarufu wa mpira wa Kikapu duniani Dwight Howard akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam  leo. Dwight Howard ni mchezaji nyota wa timu ya kikapu ya Orlando Magic ya nchini Marekani.
 Nyota mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard akimwangalia Simba aliyekaushwa kitaalamu na kupamba lango la Ikulu jijini Dar es Salaam huku akifurahia jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati nyota huyo alipokwenda Ikulu kumsalimia Rais na kutoa ahadi ya kutoa msaada ili kukuza vipaji vya mchezo huo nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia),Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard(Katikati)wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam leo. Nyota huyo anachezea klabu ya Orlando Magic.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. jamaa mara kajisahau kampiga konzi JK

    ReplyDelete
  2. Ahahaaa! wewe Ananymous wa Tuesd 8/23 usiniache hoi, ahahahha naona kama Mr Presidaaa kama anaogopa vile kwenye picha imebidi ajichekeshe.

    ReplyDelete
  3. Where is Hasheem Thabit?

    ReplyDelete
  4. Ahahahahahha! @Anonymous Aug 23 1240. Thubutu!...Enhe haya Thabeet yuko wapi?!...

    ReplyDelete
  5. On the last picture, the focal point is Dwight Howard instead of President Jakaya Kikwete.

    ReplyDelete
  6. Jamaa anapanga namna ya kumwona msaada lol!

    ReplyDelete
  7. raisi wetu anapenda sana kucheka mie huwa najiuliza anakasirika saa zingine au ni mcheshi tu? yaani hata ukiangalia historia nzima ya maraisi wetu utaona yeye ni mcheshi sana inaonyesha hata ni rahisi kwenda kumweleza tatizo lako raisi mstaafu ambae ninamwogopa ni benjamim mkapa afadhali hata marekemu nyerere, tulikuwa tukisali nae st.peters alikuwa anasalimia saa zingine.

    na mie siku moja nitakuwa mbunge

    ReplyDelete
  8. Hiyo picha ya Mwisho sipati picha angekuwa amesimama kulia Mkapa kushoto Mwinyi.

    ReplyDelete
  9. Mnugu ni mnugu tuuu....nchi ya watu anampa rais 'deuces'.

    ReplyDelete
  10. Duh! hii noma...ghafla bin vuu JK kafanania KIPARE zaidi.....kwikwikw

    ReplyDelete
  11. This guy is huge... Duhhh

    ReplyDelete
  12. jamani hasheem thabeeeet yupo wapiiii?...usikute hadi kikwete kamsahau...am not a hater am just saying

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...