Ankal Michuzi

Ni matumaini yetu kuwa unaendelea vema na Hongera  kwa kazi nzuri ya kuihabarisha jamii ya watanzania kupitia Blog yako.

Ankal,  sisi wakazi wa Mivumoni Block 5 and 6 zaidi ya kero nyingi tunazokabiliwa nazo kama ya maji na barabara. KERO kubwa hapa MIVUMONI sasa hivi ambayo imekuwa inaleta usumbufu na kelele ni ya wachimba mchanga katika maeneo yetu ambayo wameyageuza kuwa machimbo rasmi na kuhatarisha mazingira kama inavyoonekana.

Tulikwishatoa taarifa juu ya jambo hili polisi, serikali ya mtaa, kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kwa DC mwezi June. Lakini hadi hivi leo mwezi August watu hawa wanaochimba mchanga wanaendelea kuchimba mchanga na wamediriki hata kututishia sisi wananchi wa eneo hili la Mivumoni. 

Na miongoni mwa malori haya yamo pia yasiyokuwa na namba kwa kweli inashangaza kuona jambo hili la uharibifu likiendelea na wahusika ambao tayari wamepelekewa taarifa wakiwa hawajafanya kile ambacho kinahitajika ili kukomesha jambo hili la uharibifu wa mazingira na haswa katika makazi ya watu.

Hivi ni kwa nini katika jambo hili ambalo limekwishaleta madhara baadhi ya WATENDAJI wanashindwa kuchukua hatua za haraka na za kinidhamu kwa waharibifu hawa? Je Manispaa na wizara au ofisi inayoshughulika na mazingira ambazo tayari walikwishapewa taarifa wanafanya nini? Sisi wananchi na walipa kodi ambao hata kodi ya viwanja tunalipa ambavyo ndivyo vinavyoharibiwa inatushangaza sana kuona jambo hili bado uharibifu huu ukiendelea.

Sasa sisi wananchi tumeshaharibiwa mazingira yetu pamoja na barabara na sasa eneo hili limekuwa ni hatari maana halina barabara na pia transforma iliyoko katika eneo hili inakaribia kuharibiwa na wachimba mchanga hawa WASIOFIKIRI na wasiojua wapi pa kuchimba mchanga.
 
Ndugu Michuzi, tunaomba ututolee taarifa hii kwenye blog yako ili wahusika na UMMA uelewe jambo hili na kulifanyia kazi haraka.
 
Asante,
  Sisi wananchi wa Mivumoni Block 5& 6
 Hii ndio hali ilivyo leo Mivumoni na hakuna kinachofanyika kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hivi kwa nini hatuwatumii wanajeshi kwenda kuzuia vitendo kama hivi kwenye maeneo hayo? Maana inaelekea serikali za mitaa pamoja na polisi wameshindwa kufanya kazi yao na hao wachimba mchanga wana nguvu kuliko raia.

    Vile vile wanajeshi wetu wanakula na kulala tu kwa hivyo angalau tutawapatia kibarua cha kuwafanya wawe busy kidogo na kuacha kupiga raia bila ya sababu.

    ReplyDelete
  2. .... yaani inasikitisha sana!

    Sijui Watanzania tuna tatizo gani? Maana hapo huyo mchimba mchanga wala haitaji kuitiwa polisi ili ajue kuwa anaharibu barabara. Ni jambo la kufikiri tu! Hiyo barabara haipo tena, subiri mvua kidogo tu basi haipitiki. Kisha huyo huyo atailaumu serikali.

    poleni sana wakazi wa hilo eneo, lakini nadhani sasa mjikusanye kundi kubwa kisha mwende kituo cha polisi (ila bila furugu).

    Adau Amsterdam

    ReplyDelete
  3. Poleni. Mbunge wenu anashangialia kombe la ngao ya Jamii kwanza.

    ReplyDelete
  4. Aise!Kuna mdau mmoja humu alishawahi kutoa comment kwamba nchi yetu ilipofikia inastahili kutawaliwa na DICTATOR.Achana kwanza na viongozi wa serikali hivi hao wanaochimba mchanga hapo karibu na barabara hawaoni hatari ya kubomoa hiyo barabara na kuharibu hayo mazingira..Tunaweza kuwalaumu viongozi wa serikali kila siku..Hata sisi wenyewe tuna matatizo.Daresalaam mtu anatoka kwake anabeba maganda ya mihogo,viazi,nywele za Saloon,kokwa za nazi anaenda kumwaga barabarani!Ebu niambie hapo serikali ifanye nini?Mimi sishangai hao wanaotifua huo mchanga.Badilikeni Watanzania.

    David V

    ReplyDelete
  5. JAMANI MAISHA YA WATU NA MAZINGIRA WANAYOISHI NI MUHIMU.
    NA BARABARA HUTMIKA KUSAFIRISHA WATU NA BIDHAA ZAO VIKIWEMO CHAKULA NA MAVAZI, AMBAYO NI MAHITAJI YAO MUHIMU.
    BASI WAHUSIKA TIMIZENI WAJIBU WENU KUZUIA HUO UHARIBIFU.

    ReplyDelete
  6. Kwani nyie wananchi wa maeneo ya huko hamna umoja? Hivi kibaka akivamia nyumbani kwako utamuacha aendelee kukwapua mali huku ukisubiri polisi waje kumkamata?

    ReplyDelete
  7. Hapo wanadau wenzangu wa mivumoni ni kutumia umoja tu sasa kama serikali imeshindwa kusaidia na umoja huo unatakiwa kuwa kama sungusungu chini ya mwenyekiti wa serikali ya mitaa,kwa maana mnasubiri magari yameingia mnazuia yasitoke na mkiweza kuweka magogo na mawe makubwa au kupark magari ili wasitoke mpaka polisi waje au uwe mwsiho wa hiyo tabia,na mkiweza kumfundisha adabu dereva mmoja na wapakiaji wake basi itakuwa mwisho.Hapo msitaraji polisi wala serikali kusaidia ila wenyewe mjisaidie tu kwa umoja.
    Mdau wa mivumoni

    ReplyDelete
  8. Hiyo ndio bongo! kila mtu anafanya atakavyo! 50 yrs after independence, no development, no leadership and no responsibility! Bola liende!

    ReplyDelete
  9. Naona kwa nyuma watu wamejenga magorofa yao lakini watakuwa hawana barabara mda sio mrefu. wakiwa na umoja wao watazuia hou upuuzi lakini wakiaa chini na kulaumu serekali watapoteza kila kitu

    ReplyDelete
  10. poleni sana. kitu kama hiki mngetakiwa kuweka kwenye blogs, magazeti, tv nk mapema kabla hayo mashimo hayajakuwa makubwa hivyo. watanzania tumesoma tunatakiwa kuyashuhulikia mambo kama haya mapema na kwa nguvu sana. ninasikitika sana kuona uaribifu kama huu.

    ReplyDelete
  11. Kuna siku moja lori la mchanga liligonga gari langu na ilikuwa ni makusudi kisha halikusimama. Nikachukua namba nikaenda polisi kuripoti. Kesi haikuwapo kumbe lile gari lilikuwa ni la Mbunge nikaishia kutengeneza gari mwenyewe maana nilikuwa na bima ya third party. Hapo inawezekana hayo magari yanayochimba mchanga ni ya Vigogo wa TZ ambao sheria haiwagusi!!

    ReplyDelete
  12. upole wetu watanzania utatufikisha pabaya, na ni kupitia huo viongozi mafisadi wananyonya wananchi na kuwaacha bila msaada huku wakiwaimbia wimbo huu, "amani, amani, upole wa ujinga wenu udumu tuneemeke sie wachache. sinzieni, sinzieni, muda wa kuamka bado sinzieni na njaa zenu, msihoji, msihoji, epukeni vita! sie twala nanyi mwalala AMANI idumu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...