Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wao dhidi ya Yanga
 Fashifashi zarindima kwa furaha
 Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu (kuume) akiwa na kocha wa Wekundu wa Masimbasi Moses Basena kutoka Uganda baada ya ushindi
 Mchezaji Patrick Mafisango wa Simba akipokea sh. 500,000 kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Iman Kajula baada ya kuwa Mchezaji wa Mechi leo
 Makamu wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani akimkabidhi nahodha wa Simba Juma Kaseja Ngao ya Jamii
 Kaseja akifurahia Ngao yao ya Jamii

 Furaha ya Ngao ya Jamii
 Ngao ikifunguliwa
 Hii ndio Ngao ya Jamii yenyewe...
 Kaseja akipokea Ngao ya Jamii
Mshambuliaji Emmanuel Okwi wa simba akijaribu kumpiga bao kipa wa Yanga Shabani Kado Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaaam usiku huu ambapo Simba wameibuka kidedeka kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Haruna Moshi 'Boban' na Felix Sunzu katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa Ngao ya Jamii kufungua pazia Ligi Kuu ya Vodacom inayoanza kurindima Jumamosi hii katika viwanja mbalimbali
 Kikosi cha Simba SC leo
 Kikosi cha Yanga leo
 kocha wa Yanga na benchi lake la ufundi
 Kocha wa Simba na benchi lake la ufundi
 Wachezaji wa Simba wakiwang'gong'a mashabiki wa Yanga baada ya Haruna Moshi 'Boban' kufunga bao la kwanza
 Furaha ya wachezaji wa Simba
 Mashabiki wa Simba wakishangilia kwa nguvu zote
 Simba! Simba! Simba! Simba!
 Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!
  Mshambuliaji hatari wa Simba Felix Sunzu akiwa kamwacha Manzese beki wa Yanga
 Haruna Moshi ajeruhiwa
 Wachezaji wa Yanga wakilalamikia refa kwa kutoa penati kwa Simba
 Haruna Moshi akitolewa nje baada ya kuumia
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili. 
Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Simba mmenipa raaaaaaaaaaaahaaaaaaaaaaaa,mbili kwa buyu,tanzania yote wanajua kua YANGA ni KOBE wa Juu Ya MTI[ANABEBWA TU]rejea miaka yote walio twaa ubingwa,wamewai kuwashawishi timu ya mji mpwapwa ijotee ktk ligi ili wao watwae ubingwa,karibun hivi walimkatia rufaa nyoso ili wawe mabingwa ila hawatuwez kwa NGOZI,ni hayo wadau
    wakatabahu maqqmuz tzSimba mmenipa raaaaaaaaaaaahaaaaaaaaaaaa,mbili kwa buyu,tanzania yote wanajua kua YANGA ni KOBE wa Juu Ya MTI[ANABEBWA TU]rejea miaka yote walio twaa ubingwa,wamewai kuwashawishi timu ya mji mpwapwa ijotee ktk ligi ili wao watwae ubingwa,karibun hivi walimkatia rufaa nyoso ili wawe mabingwa ila hawatuwez kwa NGOZI,ni hayo wadau
    wakatabahu maqqmuz tz

    ReplyDelete
  2. Wawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah! Mnyama umekata ngebe na kelele za Yanga. Walikuwa wanachonga sana jana kwenye facebook. Mpira hauchezwi kwa maneno bali uwanjani, yaani mbili bila, tehe hehe! Tena wajue kuwa hizo goli wameonewa huruma kwa mpira wa mnyama hata bao tano zingefika. Tuwazomee Yanga makopo (haooooooooooooooooo wachovu). Simba tuondeleze umoja na mshikamano kikosi ni kizuri sana licha ya hujuma za TFF za kumbania mchezaji wetu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Gervais Kago katika Ligi Kuu msimu ujao. Yaani nina hasira na Yanga!!

    ReplyDelete
  3. Penalty given to Simba really killed the whole game, vinginevyo tunge enjoy mpira mzuri leo wenye upinzani na mvuto. Lakini marefa wetu ndiyo hivyo tena.

    ReplyDelete
  4. WADAU MBONI RAHA!!
    Nimekula futari kwa kutanuuuua leo hapa ukerewe!!
    Niliposikia FAT wameng'ang'ania kifaa chetu kipya kisishuke dimbani nitahisi tu mbinu zile zile za kiyangayanga zinaanza kutumika kukwepa mkong'oto.
    lakini leo wamemjua mnyama ni kiboko kiasi gani.
    Leo vipopoo vyangu nimevila kwa raha tupu, sasa jangwani kimyaaaa.
    Hao yanga, samahani sana wadau, nawafananisha sana na hawa man u, kubebwabebwa tu. Ubingwa wao huwa na mikingamo kibao, kabumbu hasa hawaliwezi.
    Kama unadhani sina ushahidi, mpenzi wa man u, rudisha kumbukumbu za man u vs barcelona, utaelewa nasema nini.
    kisha kumbuka ile picha ya refarii mwenye jezi ya man u.
    Kubebwa tu.
    Yanga mbeleko, man u mbeleko!!
    Lakini leo ukweli umedhihiri.
    HOYE MWANA SIMBA HONGERA, SIMBA SPORTS CLUB!!!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  5. simba akishinda umeme hauzimwi hii balaaa kumbe tanesco ni simba ujuma
    mpaka mpirani bongo hoyeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  6. watu wazima wanatoka jasho kisa hiyo ngao, ngao haijatulia utazani jeneza bwana

    ReplyDelete
  7. Mangi wa KiboshoAugust 18, 2011

    Barca hureeeeeeeeeeeee! Oh sory jamani, Simba hureeeeeeeeeeeee!!!!!

    ReplyDelete
  8. Supu: Hicho kichwa cha habari mie kimeniacha mataani. Nilisoma na kuelewa kuwa SSC ndio waliofungwa tungi mbili. Kumbe kiswahili tu kinanishinda. Kweli kiswahili chetu cha Dongo kuinama na Dudu Proof kimepitwa na wakati!
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  9. Kudaaaadeki! Mtu anapigwa chenga mpaka anakaa chini anakuwa mtazamaji.

    Bora amani irudi mtaani. Yanga wakishinda ni kelele tupu. Mara bungeni, safari hii huenda wangetaka kuvamia Ikulu kabisa. Hata maji watu hamnywi.

    Heko wana Lunyasi!

    ReplyDelete
  10. Jamani rahaaaa!Raaaahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
    Simba OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE""" KUBWA SANAAAAA!

    ReplyDelete
  11. Siku zote Yanga haina kitu. Wao mpira wanauweza kwenye vyombo vya habari tu. Ni sawa na mpira wa Uingereza. Wanapambwa na magazeti tu lakini wakija uwanjani weupe.

    ReplyDelete
  12. kwanza lingao lenyewe jekundu! afadhali tumeligomea kimtindo! maana tungeshinda tukagoma kulibeba TFF mngeanzisha zengwe. sasa wapeni hao hao mliowakusudia na kuwawekea rangi zao. kwenye jengo letu hakuna nafasi kama mijezi mliyoleta. mtavaa wenyewe!
    Tutakutana mbele ya safari!

    ReplyDelete
  13. Mimi Yanga ila naipongeza simba kwa Ushindi..Naipongeza simnba kwa sababu baada ya kufungwa na Yanga kwenye kombe la kagame walirudi kwenye ubao wa kuchora/kuchorea?(drawing board) na kujipanga upya..wakarebisha makosa,ufundi na matokeo yake tumeyaona.Yanga sasa na nyie mjipange Upya angalieni wapi mlikosea ili mparekebishe..Hakuna cha Uchawi hapo..mpira siku hizi ni ufundi.


    David V

    ReplyDelete
  14. Simba hawana lolote,waliumia sana wakati Yanga walipopata mwaliko bunge,mechi ya jana yamejituma kufa na kupona ili nao waalikwe Bungeni,kwa taarifa yenu hamtaalikwa ng'ooooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  15. hicho kingao hakina mpango mbona kwenye kombe la ukweli(afrika mashariki na kati) mulizima umeme .... lol

    ReplyDelete
  16. picha zimetulia, mi nilitaka kudhani kuwa mmefanya maphotoshop kumbe sivyo. Hongera mpiga picha. Kwa Simba..Eee kidedea!

    ReplyDelete
  17. Yanga bado tuko juu,kufungwa na simba tena kwenye ngao(Mninga) wala kwangu hainiumizi kabisa,sie yanga yetu ni Ndoo ndo huwa tunacharuka kama wehu!......YANGA NI MABINGWA TU!

    ReplyDelete
  18. Bonge la uwanja! Hapo ni Dar kweli embu tufamisheni wenzenu.

    ReplyDelete
  19. jamani rahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa simba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee yanga puhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh simba simba simba simba,AUNGURUMAPO SIMBAAAAAAAAAAA OH OH OH OH SIMBA IYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  20. waooo simba hongereni sana kwakweli tulifuraia ushindi japo tulikuwa giza mwanza tuliposikia tulifarijika UNCLE MICHUZI MWANZA GIZA SIKU YA 5 NA MAJI YANI TABU TUPU!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Mungu amjalie michuzi apate habari za maana ili hizi picha zipotee kwenye hii page ya kwanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...