|
Ankal akimtambulisha mwasisi wa Bongo Fleva nchini Saleh Jabir (kati) kwa msanii Ferouz wa Daz Nundaz jijini Dar leo. Saleh, anayeishi Uingereza, yuko nyumbani kwa vekesheni ya mwezi mmoja ya mfungo wa Ramadhani. yeye ndiye msanii wa kwanza wa kizazi kipya aliyeimba Hip Hop kwa Kiswahili na wimbo wake wa Ice Ice baby uliompa ushindi katika mashindano ya Yo Rap Bonanza yaliyoandaliwa na Kim & The Boyz , kabla ya vikundi vingine kama Kwanza Unit, Diplomatz na vinginevyo kufuatia. |
Mpiga picha wa Daily News na Habari Leo Fadhili Akida akila pozi na Saleh Jabir (kulia) na Ferouz wa Daz Nundaz
Mkuu wa Rap Cartoon Naruka kama Ninja na Paa kama ndege dah zamani kweli.
ReplyDeleteJe hakutoa album hata moja huko jikoni ukerewe?
ReplyDeleteopipiiiii yeyunoliiii....ice ice bebiiiiiii, dah niko form two wakati huo dah!
ReplyDeleteSaleh Jabri,umenikumbusha mbali sana, enzi hizo za ...
ReplyDeleteKitu kimenikaa moyoni, sasa naamua kukitoa mdomoni
Yooh, I do know, kusema mengine, naona choo
To the stream nataka mike ya umeme, niko kwenye stage nayakata madebe
Ngoma hii ya ajabu inawafanya watu wawe kama deadly,
inapodunda redioni, tega sikio sikiliza kwa makini
Ipende usiipende take your way, na mimi ninadunda kama kid & play
Kama hunipendi yoo kaa pembe sitopenda wengi kama Maumba
Ice Ice baby ..... too cold, too cold
Huyu akiwa mwasisi wa bongo fleva lile kundi la KWANZA UNIT chini yake marehebu Adili Kumbuka (Nigger One) na Marehemu Robert Mwingira (D-Rob) bila kuwasahau akina Ramson (Rhyme-Son) utawaweka wapi? KUMBUKUMBU YANGU INANIAMBIA KWAMBA, ADILI KUMBUKA NDIO MWANZILISHI NA KUNDI ZIMA LA KWANZA UNIT.
ReplyDeleteAlbum ya Saleh Jabil ilitwa Swahili Rap(1991). Na Kundi la Kwanza Unit lilianza 1993. Nakubaliana ni mwanzilishi wa bongo flava. Alipata umaarufu kwa sababu alikuwa anaimba kwa kutumia kiswahili.
ReplyDeleteSaleh Jabirni mwasisi wa Bongoflava kwa mantikiya kwamba ndiye alikuwa wa kwanza kurekodi kikamilifu wimbo mzima kwa kutumia Kiswahili.
ReplyDeleteEnzi zile, wasanii karibu wote walikuwa wanarap kwa Kiingereza.
Nakumbuka fika tamasha ambalo Saleh alirap kwamara ya kwanza na kushinda pale New Africa ghorofa la saba.Wasanii wengine waliduwaa, watu waliokuwepo walishangaa na baadaye kushangilia sana!
Kwa kweli ilikuwa ni mapinduzi makubwa!
Marehemu Adili alikuwa mkali nakubali, lakini kwa kweli, Saleh anastahili Taji maalumu la kukuza Kiswahili na kubadilisha kabisa mwelekeo wa rap Tanzania daima!
Taji
sasa hizo nyimbo zako king fanya utaratibu uziingize kwenye mtandao kama vipi watu turuke majoka .
ReplyDeleteNamkubali sana huyo jamaa.Kuthibitisha kuwa namuenzi ni kuwa hadi leo hii tape ya album ya Swahili rap ninayo.N
ReplyDeletenaitunza kama vyeti vya taaluma.
Mkuu ninashida na hiyo albamu. Ninafanya utafiti kidogo. Tafadhali naomba tuwasiliane kupitia barua pepe - kidojasper@gmail.com
DeleteNtazipataje hizo nyimbo zake?mwenye nazo aniuzie kwa gharama yoyote ile
ReplyDelete