Ernest Makulilo (MAKULILO, Jr.)

Habari zenu ndugu wadau

Ni matumaini yangu mu wazima wa afya na familia zenu. Nina tangazo la kuwasaidia watu kuhusu mambo ya elimu ya juu na udhamini wa masomo hayo ughaibuni.

Kwa wale wote ambao wanatafuta nasafi za kusoma elimu ya juu na kupata udhamini, huwa nina huduma ya kuwasaidia watu wanaotoka nchi zinazoendelea. Msaada wangu ni wa taarifa (Information) za scholarships, na pia ushauri wa nini mtu ufanye na vitu gani uandae ili uweze kuwa mshindani na kuinuka kidedea. Huduma hii ni BURE 100%.

Mimi binafsi ni mfano dhahiri wa watu walionufaika na Scholarships. Nimeshapokea (i) Fulbright Scholarship (30,000 USD to teach at Swahili and African Studies at Marshall University, West Virginia 2008/2009), (ii) Rotary Ambassadorial Scholarship (24,000 USD to cover living expenses for 12 months of my MA Peace and Justice Studies at University of San Diego in California), (iii) Joan B Kroc Peace Scholarship (36,000 USD to cover tuition and fees for my MA Studies). Kwahiyo nimeshapokea zaidi ya dola 90,000 USD. 

Na sasa najiandaa kwa scholarship ya PhD in Conflict Analysis and Resolution ambayo itakuwa kubwa zaidi. Na si kwamba nina bahati, la hasha…ni kujua taratibu zitakiwazo na kuzifanyia kazi kwa juhudi zote.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 4 katika kutoa ushauri na taarifa hizi za scholarships. Maelfu ya watu wamenufaika na taarifa hizi. Ninapenda kutoa wito kwa watanzania wengi kupambana na kufuatilia maana ushindani ni mkubwa.

Jina langu ni Ernest Makulilo (MAKULILO, Jr.). Kwa kuweza kupata taarifa za scholarships unaweza ku-google MAKULILO au kutembelea moja kwa moja kwenye blog yangu na forum yangu. Tembelea
  1. MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG www.makulilo.blogspot.com
  2. MAKULILO SCHOLARSHIP FORUM www.scholarshipnetwork.ning.com hapa kwenye Forum hii kuna nafasi ya kuwa MEMBER ambapo mpaka sasa kuna zaidi ya members 2281. Unapokuwa member ni kwamba kila ninapo-post taarifa yoyote ile ya scholarship inakuja moja kwa moja kwenye e-mail yako na kuweza kuifanyia kazi. Pia unaweza kuuliza swali lolote kuhusu mambo ya scholarship na ukapata majibu yako bila usumbufu. Hivyo nenda kwenye sehemu ya SIGN UP na jiunge.
  3. MAKULILO SCHOLARSHIP SHOW www.youtube.com/makulilofoundation Hapo utaweza kuona videos mbalimbali zenye msisitizo wa mambo ya msingi ya scholarships
  4. MAKULILO SCHOLARSHIP FOUNDATION www.makulilofoundation.org
  5. MAKULILO SCHOLARSHIP FACEBOOK www.facebook.com/makulilo.scholarships
  6. TWITTER www.twitter.com/scholarshipssss Follow Scholarship Forum on Twitter to get scholarship updates
Unaweza pia kusoma baadhi ya interviews zangu kuhusu hatua za uombaji scholarships hapa MWANANCHI (CLICK HERE) na BLOG AWARDS (CLICK HERE)
Kwa maswali au ushauri, wasiliana nami kwa E-Mail makulilo@makulilofoundation.org Na kwa wale ambao watakuwa wanataka kuongea nami wanaweza kunitafuta kwenye skype, username yangu ni makulilo1 na pia kwa simu tutawasiliana na nitakupa namba ya simu endapo mtu akiihitaji kuongea kwa simu direct.
MAKULILO
California, USA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hizo hela zote za ma-schoarship si ungefanyia biashara tu. Kwa maneno mengine, is the "capital" or "investment" worth it!!?????

    ReplyDelete
  2. Wewe mdau wa kwanza, katika maisha kila mtu ana malengo yake mwenyewe. Huwezi kuanza hicho kiasi cha fedha amekifanyia nini zaidi ya degree zake. Yaani wenye wivu hawakosekani, lool!

    ReplyDelete
  3. Wewe mdau wa kwanza hapo, inaitwa SCHOLARSHIP ikiwa na maana ni kwa ajili ya masomo. Mara nyingi (na sijawahi kusikia tofauti, mdau mwingine anirekebishe kama nimekosea) hizi hela za scholarship huwa zinalipwa moja kwa moja na masponsor kwenye shule uliyosema unaenda wakati unaomba scholarship. Hii ni kuzuia watu kama wewe wanaowaza kutumia hiyo hela kinyume na sababu ulizoombea. Labda tu kama kiasi ni kidogo ndio utapewa wewe mwenyewe mikononi.

    Zaidi ya hayo, hamna investment kubwa duniani kama elimu ... Kwa nini sponsors wasingekuwa tu wanawapa watu hela wafanye kama mitaji? Ni kwa sababu wanajua investment itakayokusaidia zaidi ni elimu. Mimi naomba usiweke mawazo mabaya kwa wananchi wengine, wakachezea bahati zao na mwisho wa siku kuona hamna hela iliyobaki na wamekuwa maskini zaidi. Tunachotakiwa kufanya ni kushukuru na kupigania maisha yetu since hamna sponsor anayedai hela zake baadae, wao wanatoa tu na kujiondokea zako wakiomba tu kuwa wewe utakuwa na akili ya kuitumia hiyo nafasi vizuri.

    Kuna watu kama sisi tuliosoma na scholarship na tumefikisha mbali sana, tusingekuwa huku bila hizo scholarship so wadau wengine, tumieni hizi nafasi na zitumieni vizuri..

    ReplyDelete
  4. mi ndio mtoa hoja ya kwanza, najua maana ya scholarship mimi mwenzenu mfanyi biashara kwa hiyo naangalia tu utility value. hizo dola 94,000 alizotumia huyu bwana ni kama shs. 160 million hizi zingejenga madarasa mengi tu. Kwa hiyo na put into question utility value ya mtu mmoja kupata ma-scholarship mengi na si kwamba watu wasipate scholarship..lengo lake la kusaidia wengine naliunga mkono

    ReplyDelete
  5. Nina mashaka na IQ ya mtoa comment wa kwanza, yani huyu mwenzetu ana uzalendo wa kutusaidia Watanzania wenzake tupate elimu wewe unaongelea biashara? unataka tu kuchafua hali ya hewa hapa? is there any business without BRAIN? what a shame comment!

    ReplyDelete
  6. Kulwa, kata nwele nyoa na hizo ndevu, vinakuharibu. Unaonekana hama bonge la mlevi wa pombe zilizoharamishwa.

    ReplyDelete
  7. Mdau #6, kila mtu huishi anavyotaka huku mamtoni...unaweza usitambue kama uliyepishana naye ni Mtz mwenzio, mara minywele, midevu balaa...hahaa, mambo ya kuiga hayo na kutafuta kuwa 'UNIQUE'....ila ukienda Bongo wenye ofisi zao na wasio na kitu wako Smart kuanzia nywele hadi kiatu...utadhani wote wana hela!!..lol! Mamtoni kuvaa vizuri au usmart si indicator ya 'feza'..upo hapo?

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza ungekuwa umesoma au unataka kusoma na unajua value ya elimu usingeandika pumba tena kujitetea mara ya pili.

    duh kweli wewe IQ finyu kabisa. Endelea na biashara yako hata uwe millionea bado utahitaji wasomi na utawalipa kama sasa I hope una accountant au wewe nyie ndo mnajifanya mnajua wakati pesa mnaliwa.

    Wewe na pesa zako umejenga MADARASA MANGAPI?

    acha wenye kutaka kusaidia watu kusoma watoe nawe katoe unapotaka, nyie ndo warudishaji maendeleo nchini eti madarasa nani atawafundisha? WAFANYA BIASHARA KAMA WEWE? NA ELIMU IPI KAMA HUJAENDA SHULE?

    acha wivu kasome kusoma hakuna umri hata ukiwa miaka 90 bado waweza soma hata waliosoma bado wanajiendeleza kwa kusoma wakitaka kupanda juu.

    ReplyDelete
  9. Thank you brother Makulilo.

    Wewe ni mfano wa kuigwa! I wish every brother from back home had your standard of love and integrity to their people.

    Mungu akubariki na akuzidishie zaidi.

    Dennis B.

    Buckinghamshire

    ReplyDelete
  10. asante kaka makulilo nimekuelewa nafanyia kazi suala hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...