Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi.
Picha na  mdau Ahmed Muhamed Ahmed wa Zanzinet
Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mh Issa Haji Ussi akithibitisha tukio hilo amesema ajali  imetokea milango ya saa 8:30 za usiku wa kuamkia leo, na kuongezea kuwa  meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.


Mh Ussi  amesema meli hiyo iliyokuwa imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Naibu Waziri  huyo  amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi  vya boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unaohitajika, huku Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta yake kwenye eneo la tukio.

Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Dah watu mia sita... Jaman mungu awape furaha ya millele marehemu wote.. Inahuzinisha sana.. Poleni wafiwa wote.

    ReplyDelete
  2. Nani wakulaumiwa, abiria au wamiliki? Lkn ndo ishatokea,kulaumu haitarudisha maisha ya watu wote hao, ila tujifunze kutokana na makosa. Mungu awe pamoja na familia za waliopoteza ndugu na marafiki zao.

    ReplyDelete
  3. why was there no communication between the boat and the harbour, how come it took our side till morning to send the rescue teams in??? the harbour should track boats travelling at night and if the communication is lost, they should immediately send securities to check,if this was done lots would have been saved. its a big loss to our country and a mourning period. after mv bukoba the government dint take any step, its high time they should do something about this....may god rest the souls of the departed ones in eternal peace ameen.

    ReplyDelete
  4. ALHAMDULLILLAHI LADHI A'AFANIY MIMABUTALLAKAH BIHI WADHIHI DHALLANI ALAA KATHIYRIN MIN MAN KHARAQA TAFDHIYLAA,,,,,!!!YA'ARABI INNA LILLAHI WAYNNA ILLEYHI LAJU'UN!!!MUNGU WANGU IMENISTUA MNO!SINA MAZOEA YA KUFUNGUA COMPUTER ASUBUHI KULI NIMEKUMBA NA HII BREAKING NEWS MBAYA SANA,,MWENYEZI MUNGU AWAREHEMU WOTE MASIKINI,,HUWA NASIKIA KINA CHA PEMBA NI KIREFU MNO,,MELI HUWA ZINAYUMBA SANA!!!JAMANI WATU 610 NI WENGI,,MASIKINI INGEKUWA KAMA NCHI ZILIZOENDELEA LABDA KIDOGO WACHACHE WANGEOKOLEWA,,,IMEKUWA KAMA MELI YA MV BUKOBA,WATU WANAKUFA WENGI BILA MSAADA WA KUTOSHA,,,,POLENI WAFIWA JAMANI,,AHLAM UK

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wazanzibari, kwa kweli ni msiba mkubwa sana! Hili limetokea tena kabla hata makovu ya MV Bukoba hayajaondoka mioyoni mwetu! Serikali lazima iwajibike kwa hili kwa sababu ina vyombo vingi ambavyo vingeweza kuratibu usafiri wa majini na kuhakikisha kwamba idadi ya abiria na kiasi cha mzigo unaosafirishwa na chombo husika ni sahihi na katika uwezo wa chombo. SUMATRA mnafanya nini kuhusu maisha haya yanayoteketea! NAVY hamkuona haya yote jamani? Usalama katika bahari yetu ukoje? Kuna jambo viogozi wa serikali wanatakiwa kuwaeleza watanzania! Kuna kitu hapa, si kawaida! Nchi imelala, waroho wa fedha wanateketeza wananchi! Mzigo Mkubwa + Abiria kuzidi kipimo = Tamaa ya Fedha= kukosa ubinadamu= ukatili kwa watu na taifa kwa ujumla!
    Poleni sana wazanzibari.

    ReplyDelete
  6. mbele yetu nyuma yao mungu awalaze pema peponi amen...

    ReplyDelete
  7. INNALILLAHI WAINNA ILLAIHI RAJIUN. MWENYEZIMUNGU WAJAALIE MAKAZI MEMA PEPONI NA WALIO HAI AMBAO HAWAJAPATIKANA MUNGU AWANUSURU. WAKULAUMIWA SERIKALI NDIO CHANZO CHOTE HIKI HAWAKO MAKINI NA SEFTY.

    ReplyDelete
  8. Its really painfully, nothing to Say. Lets just pray for our fellow citizens.

    ReplyDelete
  9. Yani sina la kusema,kufa c neno gani lakin ukisikia umati huo kwa wakati mmoja mwili lazma usisimke kwa kweli.Kuhusu kulaumiwa wanaohusika na hiyo ship.abirie msiwatie kabisa wao hawajui sheri muhim wafike safari yao.Na pengine sio wingi wa watu ni hili mbona vnazama vmashua itakua mail?AJALI HAINA KINGA.Alipangalo Mola hakuna wa kulipangua.Mama Mimah

    ReplyDelete
  10. da;;poleni sana wafiwa na majeruhi woooooooote jamani kwani inauma sana mungu awape afya wete walionusuruka.

    ReplyDelete
  11. Luggage + 610 passengers? To me this looks like an overload!

    May the Almighty God rest the souls of our dear departed brothers & sisters in eternal peace - Amen.

    ReplyDelete
  12. poleni sana, we ll be 2gether in prayers

    ReplyDelete
  13. Nina sikitika kusikia meli imezama tena Tanzania. Nina chukia kusikia habari ya kujaza meli kupindukia! Huo ni shauri ya uchu wa pesa! Nani atawajibika hapa? Kwa nini meli iliruhisiwa kuondoka bandarini Dar?

    Poleni wafiwa.

    Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Amen.

    ReplyDelete
  14. Mwili umenisisimuka na machozi kunitoka. Poleni sana wafiwa, Mungu awarehemu wote waliokufa na awape nguvu majeruhi. Msiba huu sio wa Zanzibar tu bali ni Tanzania nzima.
    Muda si mrefu nilikwenda Zanzibar, boat halikuwa limejaa sana ila siku (ilikuwa Jpili) narudi Dar es salaam na boat la Kilimanjaro huwezi amini humo ndani tulivyojazana hata sehemu ya kusogeza mguu haikuwepo, bado mizigo ilisheheni hadi sehemu ya kupita haionekani. Mteja/masafiri sio wa kulaamuniwa sana kwa hili kwani unapokata ticket yako huwaambiwi kuwa boat/meli imejaa kwani wenye chombo na mawakala wao wanauza ticket hadi dakika ya mwisho. Mteja/msafiri unapoingia ndani ya chombo ndio hapo unajionea mwenyewe na pesa tayari umeshalipa.

    ReplyDelete
  15. huu co muda wa kulaumiana bali ni tyme ya kutafakar ni jinsi gan tunatakiwa tuwaombe wezetu waliofarik ili waweze kupumzika kwa AMANI! Naamini sisi tulikua tunawapenda xana ila mwenyezi mungu kawapenda zaid.

    ReplyDelete
  16. polen xana kwan ss tuliwapenda sana ila mwenyezi mungu kawapenda zaid

    ReplyDelete
  17. ...Kama ilishatokea itatokea tena na tena.la msingi hapa ni kuangalia namna tunaweza kuwa proactive na kupunguza idadi ya vifo kwa matukio ya kesho ya namna hiyo.watanganyika huwa hautna tahadhari mpaka litokee maana hatuna viona mbali vichwani mwetu-hovyo kabisa hovyo

    ReplyDelete
  18. Poleni sana Watannzania wote. Mola aziweke roho za wote waliotutoka mahali pema peponi, na kuwapa afya njema mapema wale wote walionusurika na ajali hiyo ya kutisha. Baada ya MV Bukoba tulidhani kuwa idara za Serikali zinazohusika zingechukua hatua kuhakikisha ajali kama hii ambayo ni wazi kuwa imesababishwa na uzembe wa khali ya juu na tamaa ya pesa bila kujali maisha ya binaadamu. Nimesafiri mara kwa mara kwenda na kurudi Kisiwani na jambo hili lipo wazi kuwa wapo abiria wanaoingia na tikeki kwenye chombo na wapo wasiokuwa nazo, hivyo inadhihirisha kuwa idadi kamili ya waliotutoka na waliopotelea baharini haitapatikana kamwe. Ni jambo la kusikitisha mno kwa viongozi wote wanaohusika. Ni vigumu mno kwa chombo (vessel) kupinduka kwa jinsi kilivyoundwa, iwapo ujazo wake utazingatiwa, au labda itokee dhoruba kali mno baharini. Ni wakati wa Tanzania kutekeleza sheria za 'manslaughter' na kuwawajibisha kwa wale wote wanaohusika na mambo kama haya ambayo ni aibu mno kwani watu wamepoteza baba, mama, watoto, wake, waume n.k sababu ya tamaa ya watu wachache.

    Naomba wadau mpate kusoma zaidi katika Link hii ili kupata picha halisi:
    http://uk.news.yahoo.com/zanzibar-ferry-sinks-600-aboard-250-saved-062548433.html

    Ahsante.

    Mdau.

    ReplyDelete
  19. Inasikitisha na uchungu Mungu.
    Inashangaza inaonekana kulikuwa hakuna mawasiliano wakati ajali inatokea, inamaana kama kwa bahati hilyo melin nyingine isingepita wakati huo basi kusingekuwa na waliookolewa.
    Dunia ya leo iliyojaa teknolojia ya mawasiliano hii ilikuwakuwa vipi?
    Na hii nchi ya Tanzania hivi kweli ajali zinazotokana na uzembe zitaisha lini kuokoa maisha ya watu??? Juzi mabom katika makazi ya wananchi, jana ajali za barabarani, leo meli, kesho ndege.....???
    Ni cha ajabu na aibu hutasikia aliyewajibika wala kuwajibishwa.
    Huu msemo wa ajali haina kinga jamani umepitwa na wakati, inabidi tuwajibike vilivyo.
    Mungu awafariji wafiwa na marehemu aziweke roho zao pema peponi.
    Amen.

    ReplyDelete
  20. Mwezi Mungu awape raha ya milele marehemu wote na awape nguvu ndugu jamaa na marafiki walio poteza ndugu zao katika kipindi hiki kigumu.

    mdau Houston, Texas USA.

    ReplyDelete
  21. hii yote ni matokeo ya kuwa na watendaji wasiofanya kazi zao. Hebu tusugue goti na kujinyenyekeza, tuziache njia zetu mbaya tumrudie Mungu ili apate kutenda jambo kuhusu hii nchi jamani! Believe me God is Able!Tatizo ni sisi wanadamu hatuchukui nafasi zetu kwa kadri ya maagizo ya Mungu. Baba Mungu tunaomba uingilie kati katika nchi yetu hii imbayo imeghubikwa na uchoyo/ubinafsi na ulafi (selfishness and greedy)ya viongozi wetu wengi

    ReplyDelete
  22. Mola azipokee roho za marehemu wote katika mikono yake mitukufu, awajalie majeruhi kupata nafuu na awafariji ndugu zao..Amen

    Tanzania Tanzania, when shall your burden lessen? Whom shall we blame this time?

    ReplyDelete
  23. Ishatokea, na yote ni mambo ya Mungu. Tumshukuru Allah!

    ReplyDelete
  24. mm lawama natoa kwa serikali sababu haitilii manani ktk mambo ya maana wao focus yako ktk pesa sababu kila kitu kina utaratibuke moja meli zenyewe hazina ubora hazina insurance alafu izo meli zenyewe hakuna idani kamili ya watu wanajaza kama matenga ya nyanya alafu life jacket akuna life boat akuna ya ku save linapotokea tatizo kama ili pia vifaa vya uokoaji akuna cost guard akuna wanaoangalia usalama baharini dah inasikitisha sana watu wanakufa kifo kibaya sana kwa uzembe.pia uzembe mwingine meli imeonekana inamatatizo kwanini imeruhusiwa kupakia abiria iyo inatembea majini sio nchi kavu jamani.pia serikali inatakiwa ifatilie aya mambo kiukaribu wasiwe wanapokea rushwa alafu hatma yake watu wanakufa kiuzembe kwa nini meli iwe inabeba abiria na mizigo alafu hakuna idadi ya tani ina load dah inaniuma sana sina uwezo wowote wa kusaidia ina nawaombea kwa MUNGU MAREHEMU WOTE AWAONDOLEE ADHABU YA UMAUTI..BY HAJIEZ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...