Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa gatini kabla ya safari.
Chama cha Kampuni za Utalii (ZATI) kimeandaa mkutano wa Harambee kuchangia wsalioathirika na ajali hiyo mbaya kutokea visiwani Zanzibar. Mkutano huo utafanyika hoteli ya Zanzibar Beach Resort na unaratibiwa na Mwenyekiti wa ZATI Bw. Abdulsamad Said. Wote mnakaribishwa kuchangia ndugu zetu.
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akiongoza zoezi la uokoaji Nungwi toka mapema asubuhi
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akiwafariji walionusurika
Mmoja wa abiria 525 waliookolewa akifikishwa ufukweni Nungwi.
Picha na mdau Othman Mapara
Picha na mdau Othman Mapara
Na Salama Njani
- MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohammed Shein, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba mkubwa ulioikumba zanzibar kutokana na ajali ya meli iliyokuwa ikitokea Unguja ikielekea Pemba , iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya vyombo vya habari leo jioni, huko Ikulu mjini Zanzibar DK Shein amesema Serikali inatangaza siku tatu za maombolezo kuanzia kesho tarehe 11 September, aidha katika kipindi hicho sherehe na tafrija zote hazina budi kusitishwa sambamba na bendera kupepea nusu mlingoti.
Akielezea mikakati ya Serikali katika msiba huo amesema serikali itashughulikia kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwatambua waliofariki,kuwasaidia waliookolewa na waliopata maumivu, itashughulikia maziko kwa wale wote waliofariki kwa wale watakao tambuliwa.
Aidha DK Shein amesema kwa wale ambao hawatatambuliwa na jamaa zao Serikali itachukua jukumu la kuwazika katiaka lililotengea huko KAMA wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais alivipongeza vikosi vya ulinzi kwa kazi nzuri waliofanya katika harakati za uokozi wakishirikiana na Wananchi, pamoja na vyombo vya habari ambavyo vimefanya kazi ya ziada ya kuwajuulisha wananchi matokeo yote ya ajali hiyo.
Aliwataka wananchi wote na zaidi waliofiwa kuwa wastahamilivu kwa msiba huo uliowafika na waone kuwa hayo ni majaala ya Mwenyezi Mungu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mara baada ya kuzungumza na vyombo vya habari alitembelea eneo la Maisara ambapo maiti za wahanga hao wa ajali ya meli wanapofikia ili kutambuliwa na jamaa zao.
Wakati huo huo mpaka hivi sasa watu wapatao 620 wameokolewa wakiwa hai na watu 189 wamefariki dunia hata hivyo hali ya uokozi inaendelea.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
10/09/2011
nimasikitiko makubwa sana ambayo yametukuta sisi watanzania kwa ajali hii iliyotokea,sote kwa pamoja mungu atatupa subita ma uvumilivu kwa haya yote na wale ndugu zetu waliofiliwa na ndugu zao tunawapa pole sana tu,jambo lengine naomba kujua ikiwa tatizo kubwa limetokea ktk nchi na serikali ikatangaza maombolezi ya siku 3,je kuna nafasi ya kuendelea na mashindano ya u miss kwa sasa?ya ulazima sana hayo kwa wakati huu ikiwa rais mwenyewe amesitisha ziara yake ughaibuni
ReplyDelete