Kufuatilia mtiririko wa ajari ikiwemo za barabarani na za majini na mwisho wa siku tunashindwa kutambua idadi kamili ya abiria waliosafiri na chombo husika, ni kaona niwakilishe kwa wadau wa globu ya jamii kisa hiki.

Nilikuwa nasafiri toka Morogoro kwenda Dar siku ya ijumaa tarehe 16 Sept 2011 kwa usafiri wa basi la Aboud, tulipopanda pale kituoni Msamvu tiketi zilikuwa zinagaiwa kama pipi, yaani unampatia pesa kondakta naye anakupa tiketi ambazo zimejazwa kila kitu kasoro jina la abiria ambalo halijazwi, hakuna cha manifest ya abiria wala nini, nilizua kaubishi kidogo mpaka wakaniandikia jina katika risiti yangu, lakini hawakuja popote. 

Kama hiyo haitoshi, bus liliongeza abiria wengine 6 ambao wengine walikaa na wengine kusimama, cha ajabu bus likapita mbele ya trafiki pasi na kuulizwa chochote. Tulipofika Mwidu ambapo basi la Glazia lilipopata ajari askali trafiki akasimamisha bus, cha ajabu bila kuhoji chochote nae akaomba lifti akawa miongoni mwa abiria waliosimama, kama picha inavyoonyesha. Yule askali trafiki alikuja shuka Kibaha na kutuacha tukiendelea na safari mpaka Dar.

Je kwa utaratibu huu tutafika ? ama ndiyo yale yale mazoea yetu, mpaka ikitokea ajari ndiyo tunaanza kufuata taratibu na sheria ?

Nawakilisha
Mdau mwenye uchungu na Nchi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. HII NDO TANZANIA YA LEO.... KWAKWELI TUNAPOKWENDA KM TUNABAHATISHA...KIUFUPI WATANZANIA HATUJUI HAKI NA SHERIA ..SO MWENDO KUBURUZWA INSTEAD KUBURUZANA.

    ReplyDelete
  2. ebu huko ajari, ajari ndiyo kiswahili gani hicho. ni AJALI

    ReplyDelete
  3. Usijali ndugu yangu sie tumezoea ajali itokee ndio tuanze piga porojo:
    WEKA MATUTA,WEKA GAVANA,NANI KATOA RAMBIRAMBI,FUNGIA GARI FULANI,TUMEAGIZA MITAMBO YA KISASA............. ili muradi wananchi tumezoea kupewa na kupokea porojo.Hali kama zipo maeneo mengi ya nchi ebu angalia sehemu kama pale Ubungo watu wanafanya biashara katika mazingira hatarishi lakini hatua hazichukuliwi.
    Huyo askari unafikiri kwanini hakuchukua hatua? Anajua watu haohao ambao angejaribu kuwalinda wangemjia juu na kumwona ovyo, ni bora akapata lifti yake aende kuona familia yake.

    ReplyDelete
  4. ACHA KELELE WEWE UNAFIKIRI HAPO UGHAIBUNI? USAFIRI HAKUNA WA KUTOSHA, SASA UNATAKA WATU WASISAFIRI WAKATI WANAWEZA KUSIMAMA? KAMA NAFASI YA KUSIMAMA IPO PAKIA, HATA UKEREWE KWENYEWE KUNA MABASI WATU WANASIMAMA. KITU MUHIMU DEREVA AENDESHE KWA TAHADHARI NA SIO MBIO KUBWA AKASHINDWA KUMUDU BASI. BIASHARA YA USAFIRI INAFANYWA NA WATU BINAFSI AMBAO WANATARAJIA KURUDISHA GHARAMA ZAO ZA UENDESHAJI NA KUENDESHA FAMILIA ZAO. SHIRIKA LA SERIKALI MMELIFANYIA UFISADI MPAKA LIMEFILISIKA.

    ReplyDelete
  5. AM SPEACHLESS KWAKWELI

    ReplyDelete
  6. Ajali ni AJALI...Wanasema Ajali Kazini...Kama We ulikuwemo ndani, Kwa nini Hukushuka, Na Kupinga Kitendo Cha Kuongezwa Watu.....Wananchi wangekupa Mzinga Wa heshima...AJALI KAZINI...Wewe Ulikuwa unataka Utengeneze habari, sio Kuwasaidia wananchi...UNGESHUKA NA KUONYESHA UZALENDO...Mimi Ningekuwa wa Kwanza Kuwa nawe....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...