Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda akimjulia hali Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya alipomtembelea katika hospitali ya Apollo nchini India ambako Profesa Mwandosya amelazwa kwa matibabu.  Hali yake inaendelea vyema
 Kutoka kushoto ni Emmanuel Mwandosya;Dr Kheri Goloka(Mwambata wa matibabu, Ubalozi wa Tanzania,India; Mama Lucy Mwandosya, spika Mhe.Anne Makinda na Waziri wa Maji Mhe Mark Mwandosya ambaye hali yake inaendelea vyema.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Seif Shariff Hamad akiwa katika mazungumzo na Prof. Mark Mwandosya na Bwana Rodhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo alipofika kumjulia hali Prof Mwandosya ambaye amelazwa hapo kwa matibabu baada ya kuhitimisha ziara yake India iliyomchukua katika majimbo ya Andhara Pradesh, Kerala na Karnataka.
Kutoka kushoto ni Mhe. Mohamed Aboud (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili, Zanzibar), Mama Lucy Mwandosya, Bw. Radhey Mohan, Meneja Mkuu wa Hospitali ya Apollo, Mhe. SEIF Shariff Hamad na Prof. Mwandosya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Pole sana Prof. Familia ya Mkami iko pamoja nanyi kwa maombi. Mungu atakupa ahueni.

    ReplyDelete
  2. MUNGU AKUTIE NGUVU UPONE NA UREJEE KATIKA HALI YA KAWAIDA NA URUHUSIWE
    KURUDI NYUMBANI NA KUENDELEA NA MAJUKUMU YAKO YA UJENZI WA TAIFA LETU TANZANIA.
    POLE SANA MUNGU NI MWEMA UTAPONA!

    ReplyDelete
  3. Ankal
    Prof Mwandosya anaumwa nini??
    Nafikiri ni haki yetu kujua siyo tunaona mikanda tu, tujue huyo ni kiongozi wetu na kwa vile wewe umeweka hoja hii hapa basi ieleze kwa uzurim isiache maswali.

    ReplyDelete
  4. You look sooo well indeed. Keep your preps for Dar Marathon.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...