Taifa Stars

Na Shaffie Dauda
Kwanza ningependa kuwapongeza Taifa Stars kwa kazi nzuri waliyoifanya.Kiwango cha soka cha timu ya taifa kinaonekana kimeongezeka na hiyo inaonekana sana kwenye baadhi ya matokeo ya timu yetu.
Tumetoka kule ambako tangu mechi ya kwanza tunajua ni miujiza pekee itakayoweza kutupeleka kwenye fainali za kombe la mataifa ya bara la Afrika, na sasa tupo pale ambapo katika mechi ya mwisho tunaamini miujiza pekee ndio inayoweza kutupeleka kwenye AFCON.
Huu ni mwaka wa nne au wa tano ambao tumekwama kwa kutegemea miujiza ya mechi ya mwisho.Ingawa kama Mtanzania ningefurahi miujiza itupelekee kwenye AFCON, kwa upande mwingine nashukuru kwamba hatukufanikiwa maana naamini hiyo ingetupa mtizamo ambao sio wa ukweli.Kutolewa kwetu ni changamoto kwa Taifa letu kuachana na kutegemea miujiza itufikishe mbali. 
Kutokana na hilo inabidi tujijenge kwa kuweka mipango ambayo itatuwezesha kuwa na uwezo wetu binafsi pasipokutegemea miujiza ili kumpa Mtanzania imani ya kwenda CAN au kwenda kwenye fainali za Kombe La Dunia bila kutegemea miujiza ya mwanzoni au mwishoni.
Tukiangalia kalenda yetu ya taifa kwa miaka mitano ijayo:
2012 – Tumekosa AFCON
2013 – Tulikuwa na nafasi ndogo ya kwenda CAN kutokana na mfumo wa kuingia
2014 – Tuna nafasi ndogo sana ya kwenda kombe la dunia kutokana na kundi tulilopangiwa.
2015 – Hakuna AFCON
2017 – AFCON ipo
2018 – Kombe la Dunia
Draw ya kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2014 ilivyotoka tulipiga yowe la ndani,maana tulijua kufika Brazil ilibidi tupitie njia ndefu inayokutana na miamba kama Ivory Coast.Kama kawaida yetu,wanahabari na wadau walirudia tena kusema “huwezi jua, mpira ni wa duara na unadunda kwa hiyo lolote linaweza kutokea na tukapita”. 
Hapo tunarudia tena kusubiria miujiza kabla hata ya kucheza mechi yetu ya kwanza.Kwa imani yangu kutokana na mpira wetu ulivyo kwa sasa mashindano ya karibu ambayo tunaweza kuondokana na mategemeo ya kufuzu kwa miujiza ni yale ya CAN 2017 huko Libya lakini ambayo ni ya uhakika zaidi ni fainali za kufuzu AFCON 2019 na kama ni kufuzu fainali za kombe la dunia ni za mwaka 2022.
Tuna kama miaka 5 ya kujiandaa kwenda Libya bila kutegemea miujiza. Kwa hiyo la maana kabla ya yote ni kwa taifa kukubali kwamba tusijipe imani ya kucheza mashindano yoyote makubwa kwa miaka 5 ijayo.
Kutimiza hayo inabidi tufanye maamuzi magumu sana kwa siku hizi za mbeleni. Maamuzi magumu yanalipa lakini yanahitaji uvumilivu, na uvumilivu uanze kwa yule shabiki wa kawaida wa mpira mpaka kwa wale wanaotuwezesha kwa hali na mali.
Kwanza ninawashukuru wachezaji wa sasa wa Timu ya taifa, sanasana wale waliotupa miaka yao mingi sana kulitumikia taifa letu. Jasho lenu na nguvu yenu tumezitambua na mmetusogeza mbele hilo tunalitambua.Lakini Ukweli ni kwamba ukiangalia kiwango kilichooneshwa kwenye mchezo dhidi ya Morocco utangundua , kiwango chetu kilikuwa chini sana kulinganisha na cha wenzetu Morocco.
Pale ndipo uwezo wetu ulipokomea.Ili kulenga huo mwaka 2017, inabidi tuistaafishe timu yetu ya sasa Inabidi pia tuwashukuru na kuwaaga wachezaji wasasa wa Taifa Stars. Tuunde timu mpya ya vijana (U-23) timu ambayo itashiriki katika mashindano ya kufuzu World Cup 2014 na CAN 2013.Hivyo basi naamini si timu itakayotupeleka CAN kwa uwezo wao lakini ni timu itayojenga misingi ili sasa wale wa chini yao tuwakuze na kuwalea ili kuhakikisha wanafikia kwenye level ya kutupeleka tunapotaka kwa miaka mingine mingi ijayo.
Hatuna jinsi inabidi tuanzie chini kabisa, tujenge mfumo mpya wa kucheza soka ikiwa ni pamoja na mfumo wa kuibua vipaji na kutengeneza vijana wapya hasa timu timu yetu ya U-17, tujenge na kuimarisha mashindano ya soka la watoto, kuanzia mashuleni sana sana ( Hii ni topic tofauti na ina muda wake ).
La maana sana ni kwanza tukubaliane kufanya maamuzi magumu ya kutoa kabisa tegemeo la kwenda South Africa 2013 au Brazil 2014. Tukikubaliana hilo inamaanisha taifa litakuwa tayari kutekeleza mikakati ya kujenga mpira wetu kuanzia chini.
Mtembelee Shaffie Dauda BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ninakubaliana na Shaffie kwa kiasi fulani. Inabidi tuweke nguvu ktk timu ya vijana wa miaka 17 na 18 tuwatafutie waalimu wazuri na wawezeshwe kwenda nje kufanya majaribio kama alivyofanya maximo ili baada ya miaka 5 iwe ndio timu ya taifa. Kwa kipindi hicho timu hii ya wakubwa tuendelee nayo na apewe kocha mzawa ili kupunguza gharama kubwa kwa timu ambayo tunajua haina uwezo na tuendelee na mashindano tukijua kwamba matumaini yetu ni timu tunayoijenga itakayokuwa tayari baada ya miaka 5. Suala kubwa ni kuwekeza ktk timu ya vijana wadogo.

    ReplyDelete
  2. Shafii kiasi fulani umejitahidi kusema. sasa hao wanaotuongoza wana masikio?! maana haya unayoyasema mtu kama KAYUNI alitakiwa awe anayajua ukizingatia nafasi yake katika TFF. lakini yuko tu kama nguruwe aliyelishwa mkate wenye kinywaji aina ya gongo! kwa kiasi kikubwa sana Kayuni na wale waliopo katika ofisi yake ndio wametufikisha hapa. kifupi angalia mashindano ya copa coca cola, yamefanyikia mara ngapi?! tumefaidika kwa kiasi gani?! mi nadhani ipo haja ya sisi tunaohusika na mpira (wadau) tufanye maandamano mpaka TFF na kuwaomba waachie viti. Namkumbuka ndugu yangu kaka yangu Coach Mziray alikuwa anasema wazi kuhusu Kayuni hana uwezo wa kushikilia nafasi hiyo!

    ReplyDelete
  3. bakubaliana na wote.. niliangalia mpira online kwa kweli hakuna kigumu kwa Taifa Stars , nna uhakika kama tukiwekeza kwa vijana in 5 yrs time basi hatutofungwa kijinga jinga tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...