Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana alitembelea Kampuni ya Kilombero Plantations Ltd (KPL) inayomiliki shamba la Mngeta lenye ukubwa wa hekta 5818. Shamba hilo liko katika kata ya Mngeta, Tarafa ya Mngeta wilayani Kilombero.

Katika ziara yake, Mheshimiwa Rais aliongozana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mh. Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera na viongozi wengine wa Kitaifa.

Katika ziara hiyo, Rais Kikwete alijionea uwekezaji Mkubwa uliofanywa na katika shamba hilo linalojishughulisha na kilimo cha Mpunga. Rais alitembelea maeneo ya shamba, mashine za kukausha mpunga Pamoja na Kiwanda cha Kukoboa mpunga.

 1.       Rais Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya jinsi mashine za kusafisha na kukoboa mpunga zinavyofanya kazi. Anayempa maelezo ni Bw. Carter Coleman ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, akiwa na Meneja mkuu wa shamba la Mngeta Bw. Graham Anderson.
 1.       Rais Jakaya Kikwete akitoka kuangalia mashine za kukaushia mpunga (drying silos) zilizopo ndani ya shamba la Mngeta linalomilikiwa na Kampuni ya Kilombero Plantations Ltd.
  Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo jinsi Mpunga unavyohifadhiwa kwenye mifuko maalum (silo bags) kabla ya kukobolewa. Mfuko mmoja una uwezo wa kuchukua tani zaidi ya 100! Mifuko hiyo ya kuhifadhia mpunga ni moja ya teknolojia mpya zinazotumiwa na Kampuni ya KPL katika uhifadhi wa mazao.

 1.       Rais Jakaya M. Kikwete akipata maelezo ya kuhusu kampuni ya kilimo ya Kilombero Plantations Ltd kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Carter Coleman (Mwenye shati nyeupe). Mh. Rais alitembelea shamba hilo la mpunga kujionea utekelezwaji wa sera ya kilimo kwanza kwa vitendo. Shamba la Mngeta linaaminika kuendeshwa kisasa kuliko mashamba yote yaliyopo Tanzania. Uwekezaji wa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 5818 umefikia kiasi cha Dola za Marekani million 30. Shamba la Mngeta lina mashine za kumwagilia jumla ya hekta 215 mpaka sasa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelekezo kutoka kwa Meneja mkuu wa kampuni ya Kilombero Plantations Ltd (KPL) Bw. Graham Anderson (mwenye kipaza sauti) kuhusu shughuli za umwagiliaji zinazofanywa na kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Carter Coleman. Rais Kikwete alitembelea shamba la Mngeta lililoko kata ya Mngeta, wilaya ya Kilombero – Morogoro.
Picha na mdau Frederick Jailos.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunaomba huo mpunga/mchele unapouzwa nje ya nchi uwekwe lebo inayoonesha kwamba unatoka tanzania. Manake wageni wamekuwa wkaizalisha mali kwetu halafu wanazipiga labo za nchi zao. Mfano ni Tanzanite.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...