Ankal,

Leo nikiwa safari kutokea Dar es Salaam kwenda Arusha nimejihimu alfariji ila kufika Wami darajani saa moja asubuhi, nikakuta Gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba mkaa limepata ajali ya kugonga kingo za daraja na kunusufika kutumbukia mtoni. Kwa mujibu wa utingo wa gari hilo, ajali hiyo ilitokea mida ya saa tano usiku wa jana, na chanzo cha ajali ni dereva kutokuwa makini maana alikuwa anawasha sigara ndipo balaa hilo likawakuta. Kwa mapenzi ya mungu wote walitoka salama.

Ajali hiyo ilisababisha mateso makubwa kwa watu waliokuwa wanatumia njia hiyo leo. Imechukua muda mrefu sana hadi gari hilo kuondolewa darajani na magari kuanza kuruhusiwa kupita ilipofika saa tano mchana, ambapo pande zote mbili kulikuwa na mamia ya magari na idadi kubwa sana ya watu.

Nadhani pangekuwa na madaraja mawili ingeweza kurahisisha kuondoa hadha kubwa kwa wasafiri. Jambo lingine ni Breakdown iliyokuwa inavuta gari hiyo kutokuwa na uwezo, jambo ambalo limesababisha kazi hiyo kuchukua muda mrefu sana.

Mdau wa Kigambonino
Watu Mbali mbali waliokuwa safarini leo kwa kutumia barabara hiyo wakiangalia taratibu ya kuondolewa kwa gari hilo lililokuwa limeanguka katikati ya daraja la Wami.
Msongamano wa magari unavyoonekana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ndugu nawambia sisi watanzania hata tufanyeje ajari za barabarani azitakaa ziishe maana atuna sheria na hatushiki sheria sheria zingikuwepo haya mambo ya kutojari wakati unaendesha gari ya singetokea aiwezekani unafika sehemu ya hatari unaacha kuwa makini kama sehemu hiyo ya mto wami

    ReplyDelete
  2. ajari, kutojari mfyuuu!!! kiswahili gani hiki?

    ReplyDelete
  3. Tulivyo wajinga utasikia wengine wanasema ni mpango wa Mungu, kazi ya Mungu haina makosa blah blah blah badala ya ku-take responsibilities za ujinga wetu tunamsingizia Mungu kuwa ndo kasababisha hizi ajali,maumivu au vifo..

    ReplyDelete
  4. Ajiuzuru waziri wa wizara inayoshughulikia maswala ya usalama Barabarani.
    Waziri gani maajali kila siku ya uzembe,anafanya nini?
    Au yeye asafiri kwa gari?kama anasafiri kwa gari basi angejali na kuongeza nidahamu barabarani.
    Ajali zinazotokea zinasababisha Umaskini na majonzi kwenye jamii ya Kitanzania ambayo inaumizwa na kupoteza watu wao wanaowapenda tena kwa ghafla.
    AJIUZULU..apewe mtu anayependa kazi

    ReplyDelete
  5. tunakoelekea tutasikia mtu akiachana na mkewe, anadai waziri wa jinsia ajiuzulu!

    ReplyDelete
  6. MUWASILISHA MADA TUNASHUKURU KWA TAARIFA YAKO NZURI. ILA LILE GARI HALIITWI BREAKDOWN MKUU, NI RECOVERY VEHICLE LAKINI KIBONGO BONGO SAWA TU UNASOMEKA. SAWA TRAFIKI.
    ASANTE

    ReplyDelete
  7. Foleni kama kwa babu vile....Madereve wengi wavuta bangi

    ReplyDelete
  8. Wadau;Sio sehemu zote ministerial responsibility ina apply. swala kama hili ni uzembe wa mtu binafsi na sio kwamba katumwa ni waziri husika. tatizo hapa linakuja kwa matraffic ndio wanashindwa kufanya kazi yao kwa uadilifu. utingo wa gari hili akieleweka vizuri hawezi kufikishwa hata mahakamani, na ikitokea afikishwe mahakamani basi shitaka husika halitaandikwa hivyo kupelekea utingo huyo kutozwa faini ya elfu 5.

    ReplyDelete
  9. Duh hata ajali zipo kwenye maandishi. Mtu anaandika ajari azitakaa ziishe. Au kutojari, aiwezekani!! jamani kiswahili kimefundishwa kweli.?

    ReplyDelete
  10. Naomba nifahamishwe barabara ya kupitia bagamoyo unapotokea Segera ipo kabla ya wami au baada ya wami

    ReplyDelete
  11. breakdown hiyo ina majic power, uwezo inao, ila limetumika mchana, majic power inakuwa na uwezo kamili kwenye giza (usiku)!

    ReplyDelete
  12. Ujinga, atiwaziri ajiuzulu wakati ni uzembe wa watumiaji barabara. Alama husika zinawekwa kama wanashindwa kusoma au kuzingatia sheria ni jukumu lao sio la waziri.
    Comments za watu wengine hazina hata maana... mxxxuuuuu..

    ReplyDelete
  13. Huwezi amini nilikua na hamu ya kuona kwa karibu mandhari ya sehemu hii ya Wami darajani, jana ingawaje wengi wetu tulifadhaika na tukio lenyewe, mie nilipata fursa ya kufanya utalii katika sehemu hii; ni sehemu yenye scenery nzuri na ningekua na uwezo ningeanzisha kituo cha utalii ambacho kingeweza kutuletea mapato makubwa badala ya maafa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...