Na Tamali Vullu

Mh Membe akiongea na wanahabari
RAIS Jakaya Kikwete amekataa kumpokea balozi mpya kutoka nchi moja ya kigeni baada ya kubainika kuwa amefunga ndoa na shoga.
Siri hiyo iliwekwa wazi jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe alizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Uingereza ya kuzitaka nchi zinazopokea misaada kutoka nchini humo kuhalalisha vitendo vya ushoga.

Membe alisema tukio hilo lililomshtua Rais lilitokea mwanzoni mwa mwaka huu, pale alipopokea barua kutoka nchi moja (hakuitaja) ikimtaka wampokee balozi wao mpya na mkewe, lakini walipobaini kuwa mke huyo ni mwanaume Rais Kikwete alikataa.

Alisema baada ya kugundua hali hiyo, Kikwete akiwa haamini kile alichokisia alitamka maneno mawili “Toba Yarabi” na kuagiza balozi huyo asikubaliwe kabisa.

Waziri huyo alisema hata baada ya nchi hiyo kukataliwa, ilibembeleza sana kwa siku kadhaa ikidai kuwa kusingekuwa na madhara yoyote kwa balozi huyo kufika nchini na mke wake (shoga) na kwamba angetimiza wajibu wake kikamilifu.
“Waling’ang’ania msimamo wao, lakini baada ya siku nne walituelewa na kusema kuwa sisi ni marafiki wao na hivyo waliheshimu msimamo wa Tanzania na kuahidi kuwa wasingemleta tena balozi huyo na mkewe,” alisema.

Membe alisema amelazimika kusema jambo hilo kuonyesha kuwa Tanzania inapinga kwa nguvu zote tabia za ushoga na kueleza kuwa haiko tayari kutunga sheria ya kuruhusu ushoga nchini.

Akizungumza kwa mkazo, Membe alisema Tanzania iko tayari kwa lolote na hata kubaki na umaskini wake kuliko kupokea misaada yenye masharti ya hovyo.
“Tunataka kutunza heshima yetu. Kama wanadhani misaada itatolewa kwa masharti hayo wakae na fedha zao, hatukubali kutekeleza jambo hilo,” alisema.

Akiungana na viongozi wa dini walioitaka serikali isikubali wala kutishwa na nchi hiyo, Membe alisema Tanzania haiwezi kutekeleza sharti hilo hata kama ni maskini na itaendelea kuheshimu misingi ya maadili ya taifa inayokataza mambo ya ushoga.

“Hii ni nchi inayofuata maadili na haiko tayari kupokea ushauri katika suala hilo...hata nchi ikiwa kubwa kiasi gani, linapokuja suala la utaifa, hatutakubali kuyumbishwa hata kidogo,” alisisitiza Waziri Membe.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, hivi karibuni alitishia kusimamisha misaada kwa nchi zinazopinga haki za mashoga na kuzitaka zile zinazopokea misaada kutoka nchini humo ikiwamo Tanzania zikubali sharti hilo.

Membe alisema kuwa staili ya sasa ya kuunganisha misaada na suala la ushoga ni tamko hatari ambalo linaweza kuvunja uhusiano na nchi nyingine.

“Tamko hili linaweza kuvunja Jumuiya ya Madola na ikitokea ikawa hivyo, Waziri Mkuu wa Uingereza anapaswa kuwajibika,” alisema Waziri Membe.

Aliongeza kuwa kati ya nchi 54 za jumuiya hiyo, 13 pekee ndizo zinazounga mkono suala hilo na kuonya kuwa suala hilo si la kushabikia hata kidogo.

Hata hivyo, waziri huyo alisema suala hilo halikuwa ajenda katika mkutano uliomalizika hivi karibuni nchini Australia, bali Waziri Mkuu huyo aliibua katika vikao vya viongozi wakuu wa nchi.

“Suala la ushoga halikuwa ajenda na wala halikuzungumzwa kwenye mkutano ule; alichofanya Waziri Mkuu huyo ni kuibua suala hilo katika vikao vya viongozi walipokuwa wakijadili haki za binadamu. Hii ndiyo sera ya chama chake cha Conservative.

“Hata hivyo jambo hilo lilikataliwa na lilipofika kwenye mkutano walizungumza kwa mafumbo, lakini tulikataa,” alisema.

Alisema sheria za nchi za mwaka 1971 ambazo Tanzania imeziridhia kutoka kwa Waingereza zinakataza suala hilo na kutamka kuwa linapofika suala la ndoa au mahusiano ya kimapenzi linahusisha watu wa jinsia tofauti.

“Wote tunajua msingi wa familia ni mume na mke ambao wanaweza kuzaa watoto...pia sheria ya makosa ya jinai inaeleza msimamo ndio huo, hivyo kwenda kinyume ni makosa ambayo mtu anaweza kufungwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela,” alisema na kuongeza kuwa kwa msimamo huo serikali haivitambuia vikundi vya kishoga vilivyoko nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kunabidhaa nyingi duniani zimebuniwa na Mashoga, Je Watanzania wasinunue bidhaa hizo?

    Elton John ana nyimbo nyingi sana, Je Miziki yake haiuzwi Madukani?

    Hotel zinazomilikiwa na Mashoga, Je Watanzania wasilale

    Marekani ni Nchi inayotetea Mashoga, Je Serikali ikatae misaada yao? Kwa sababu wanatetea mashoga?

    ReplyDelete
  2. we mtoa maoni hapo juu kama unataka kuwa shoga endelea kivyako msimamo wa TZ ni kuwa hautaruhusu sheria ya kuwa na mashoga hataiwaje kama we unataka kuliwa kiboga poa tuu wacha watu wa kufaidi

    ReplyDelete
  3. I hope nchi zote zitakata misaada maana tangia tupate uhuru mpaka leo tumekuwa tukipewa hiyo misaada na hakuna maendeleo yoyote.

    Kwa mtaji huu ni heri ya Ushoga kuliko Ufisadi.

    ReplyDelete
  4. Bravo, Bravo Mheshimiwa Membe, bora kuwa maskini kuliko kuuza utu na heshima ya Mtanzania

    ReplyDelete
  5. DUH! INAONEKANA MTOA MADA WA KWANZA NINANIHII...........????????? MBONA KATAHAMAKI SANA. USIVURUGE UTARATIBU NA IMANI ZW=ETU ZA KIDINI. MUNGU WAUMBA WATU 2 MWANAMKE NA MWANAUME SASA IWEJE TUMKUFURU MUNGU? HATA WANYAMA NA WADUDU WAPO WAKIUME NA WAKIKE. HAO WAKAE NA MISAADA YAO SISI TUNA RASILIMALI NYINGI SANA NA WAO WAONDOKE KWENYE MACHIMBO YETU HARAKA TUONE WATAPATA WAPI MAFUTA NA DHAHABU.

    ReplyDelete
  6. Acheni kuukali utajiri!!

    ReplyDelete
  7. nyinyi mnadhani mashoga wote wanapenda kuwa mashoga, wengine wanazaliwa wakiwa mashoga na wengine wanaharibiwa wakiwa watoto, sasa je ukizaa mtoto shoga itakuwaje ? jiulize , akose haki kisa yeye shoga ?

    TAFAKARI HAKI ELIMU

    ReplyDelete
  8. NINA WASI WASI NA MTOA MADA WA KWANZA!!

    ReplyDelete
  9. Jamani tusitake kuwa wanafiki hapa.
    Ushoga Tanzania tunajua upo toka enzi, na hata leo hata baadhi ya wanasiasa na viongozi wetu tunajua ni mashoga(ingawaje wanajificha) na mbaya zaidi wameoa ili kuficha ukweli. Hii sio siri, tusitake kuwa wanafiki.
    Tofauti na wazungu ni kwamba wazungu hawajifichi ili waafrika wanajificha na hivyo kujidanganya hakuna mashoga wakati tunajua wako kibao bongo.
    Na pia tujue kuwa SHOGA maana yake ni yule mtu anayeingiliwa na pia yule anayemuingilia mwingine. Mtu yeyote nayefanya vitendo hivyo na jinsia yake basi ajue naye ni shoga.
    Watu wanakosea sana wanapofikiri shoga maanake ni mtu anayeliwa tu, LA SIVYO, na wale wanaokula nao ni shoga, na hiyo ndio maana yake.

    ReplyDelete
  10. Mtoa maoni wa kwanza kama wewe ni shoga endelea hukohuko uliko na ushoga wako. Usitake jambo hilo likawa ni shria ili wengine nao waige. Mtoa maoni mmoja ametoa mfano mzuri wa wanyama. Kwamba mbona haijatokea hata siku moja mnyama akampanda mnyama mwenzake wa jinsia moja? Ina maana wanyama wana akili kuliko binadamu?

    Pia unaonekana unapenda sana misaada ndio maana unaona ni heri kuingiliwa kinyume na maumbile kuliko kukosa misaada. Huku kupenda misaada kwako ndiko kumekusababishia kuwa shoga. Ungejifunza kujitegemea tangu ukiwa mdogo usingejiingiza kwenye uchafu kama huo.

    ReplyDelete
  11. Ushoga ni nuksi kabisa atakaye patikana apewe adhabu kali sana hiyo miaka 30 na kiboko kimoja matakoni hapo anapofanyiwa uchafu wake kwa mwanaume anayekula kiboga cha mwenzake apigwe kwenye bomba lake kila siku kimoja

    ReplyDelete
  12. Mheshimiwa Membe uko sawa ushoga ni tofauti na mila zete,pia misaada tumepewa toka tunapata uhuru lakini bado maskini kwa hiyo hata wakitoa wasipotoa hali zetu ni zile zile mpaka kufa.

    ReplyDelete
  13. Hivi wewe uliyetoa mifano ya eton john namashoga wengine unasikiliza vizuri kweli habari?au ndio mambo yakutofautiana IQ,mbonaunachangia vitu haviusiani na mada?hao mashoga hawajasema kama unataka kutumia bidhaa zao uweshoga,ila uingereza wanasema mkitaka kupewa msaada nawao mpitishe sheria ya kuhalalisha ushoga sijui umeelewa tofauti sasa,kama nimwanaume nakuonea huruma maana huna uhakika na jinsia yako unaweza kubadilika maramoja.

    ReplyDelete
  14. Msimamo kwa mdomo unaonekana ni madhubuti pamoja na sheria iliyorithiwa ya mwaka 1971 kutoka kwao huyo kinara wa mashoga DAUDI njoo chumbani lkn mashoga wameenea mitaani mbona hatuoni sheria ikichukua ukali wake tangia hapo tuliporithi sheria hii zaidi ya kuengezeka.

    Sheria imekua domat na kuwalea na kuwapa nafasi miaka yote hiyo na sasa wamefika kudai haki ya kuolewa kimataifa. kama hata hili linagusa human right ni kwanini kila mmoja asiishi atakavyo ama kwa kuvuta unga bagi na mengineyo duniani.

    Kesho na keshokutwa kutaletwa madai ya haki za kijinga kama hizi hivyo tukae tayari na vita vya kimaadili na haki ya utu wa mwanaadamu dhidi ya human abuse za ushoga na ndoa za jinsia moja.

    Watanzania kamwe tusikubali human abuse from disorder orders

    ReplyDelete
  15. Tunakubali kuwa binadamu wote ni sawa (bila ya kuvuka mipaka ya kidini na ya kitamaduni), lakini pendekezo lolote lenye kuleta mpasuko nchini kwetu, hatutokubali kuwa ndio urithi wa taifa letu kwa thamani yoyote. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  16. Msisahau walimu wataendelea kufanya kazi yao. Kwa undani zaidi fikiria swala la walimu wa kishoga watakaoFUNDISHA WANAFUNZI mahali popote nchini. Maswali zaidi yanahitajika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...