Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mh. Mohammed Dewji (mwenye miwani katikati) akipokea msaada wa Baiskeli Tano za Walemavu kutoka kwa Mkuu wa Club za wanachama wa Lions Club Tanzania na Uganda,Bw.Satish Sharma.
Mh. Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na baadhi wajumbe wa Lions Club.

Na.Mwandishi wetu.

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji amepokea msaada wa baiskeli 5 za walemavu kwa ajili ya jimbo lake zilizotolewa na Taasisi ya Lions Club Tanzania.

Mh. Dewji amekabidhiwa msaada huo leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Club za wanachama wa Lions Club Tanzania na Uganda Satish Sharma, katika makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Gerezani.

Mh. Dewji ameshukuru msaada huo akisema utakua faraja kwa wananchi wa jimbo lake ambao wanamatatizo ya ulemavu wa viungo.

“Nawashukuru Lions Club kwa msaada huu na utakua chachu kwa wananchi wa jimbo la Singida hususani walemavu wakiwemo wale wa viungo walio na mahitaji maalum, kwa kuwa baiskeli hizi zitawasaidia sana hivyo nawashukuru” amesema Mh. Dewji.

Kwa upande wake Satish Sharma amesema licha ya kukabidhi msaada huo wa baiskeli za walemavu, Lions Club wametoa misaada mbalimbali kwa nchi za Tanzania na Uganda, ikiwemo baiskeli hizo na vifaa mbalimbali vya shule.

“Kwa sasa Lions Club tunaendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii vikiwemo vifaa vya mashuleni na michango mingine ikiwemo baiskeli na baada ya hapa tutaazunguka mikoa ya Morogoro na kisha kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Msoma, Bunda na Shinyanga” amesema Satish.

Lions Club mpaka sasa ina wanachama 1600 na Club 48 kwa nchi za Tanzania na Uganda, ambapo wamekua mstari wa mbele katika kusaidia misaada ya kijamii kwa nchi mbalimbali zilizo na wanachama Duniani kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivyo ndivyo jinsi ya kununua kura.

    ReplyDelete
  2. watu wengine sijui wana nini kichwani. sasa kila mtu anatoa misaada kwasababu anatafuta kura. kama huna la maan la kusema please nyamaza. misaada kama hii inahitajika sana. kuna walemavu wengi wana teseka kwa kutokuwa na baiskeli halafu wewe unaropoka kama vile utawasaidia. mo asamte sama kwa harambee zako unazo fanya kusaidia wananchi. endelea na juhudi zako na usiwasikilize wajinga wenye kukuonea wivu. wqtu wq singida wako na wewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...