Naibu Katibu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Selestine Gesimba (katikati) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu kuhusu mgogoro wa shule ya Sekondari Ndanda iliyoko Masasi mkoa wa Mtwara leo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine serikali itawarudisha shuleni mwaka huu wanafunzi wote 62 waliohusika na mgogoro wa shule hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Sheikh Musa Kundecha, Amir wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Bw. Samweli Kusaga kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari.
Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania wakiongozwa na Sheikh Musa Kundecha (pili kutoka kulia) ambaye ni Amir wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania wakijadili jambo na Rais wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) Jaafar Mneke (katikati) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliojadili makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za kiislamu kuhusu mgogoro wa shule ya sekondari Ndanda.
Rais wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) Jaafar Mneke (kulia) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya kusitishwa kwa maandano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchini nzima kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kuhusu mgogoro wa shule ya sekondari Ndanda.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndanda waliosimamishwa masomo kufuatia mgogoro wa shule hiyo wakifuatilia tamko la makubaliano ya viongozi wa dini ya kiislamu na Serikali lililotolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Selestine Gesimba kufuatia mkutano wa pamoja uliofanyika tarehe 7 mwezi huu.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndanda waliosimamishwa masomo yao kufuatia vurugu zilizotokea katika shule hiyo wakitoka ndani ya jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kusoma makubaliano uliowahusisha viongozi wa dini ya Kiislamu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na waandishi wa habari ambapo makubaliano hayo yameeleza kuwa serikali itawarudisha shuleni wanafunzi wote 62 waliosimamishwa,kuhakikisha kuwa shule ya sekondari Ndanda ina mazingira mazuri kwa wanafunzi wa dini zote kitaaluma na kuwawezesha kufanya ibada zao, shule zote zilizotaifishwa ni miliki ya serikali kiuendeshaji, ardhi na majengo vyote ni mali ya serikali na serikali kufanya utaratibu wa kuwepo vikao na viongozi wa asasi za dini zote.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. suala doooogo limechukua muda kulitatua,maamuzi ya busara wakati muafaka ndio inavyotakiwa si mpaka watu waandamane muogope ndo mchukue maaaamuzi,kama sasa mponda na nkya wataondoka baada ya mgomo wa wiki nzima why not now

    ReplyDelete
  2. Nyie watoto wajinga sana. Badala ya kusoma mnaendekeza migogoro ya udini shuleni. Mtaishia hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  3. alhamdulillah

    ReplyDelete
  4. tatizo ilikuwa kufanya ibada au vurugu tu a hao vijana na mambo ya kuiga kwenye tv...

    ReplyDelete
  5. Wakristo wameweka nidhamu ya hali ya juu sana shuleni, ndiyo maana wanafunzi wao wanafaulu. Haki ya Mungu ingekuwa ni wakristo waliocheza mchezo wa ovyo kama hawa, wasingerudishwa. Serikali inawaogopa sana Waislamu. Angalia hata hukumu ya Dibagula ilivyofutwa! Lakini wenye akili wataomba hawa waendelee hivi hivi wakati wenzao Wakristo wakipeta kwa nidhamu na kupata ufaulu mzuri. Ukitaka kuamini, pitia matokeo ya form 4 uone. Waislamu wenye nidhamu wachache kama Michuzi ndo wamefanikiwa kwa sababu wanajua nini maana ya elimu na kuheshimu mamlaka. Hawalalami kama wenzao. Bravoo!!!

    ReplyDelete
  6. Tunashukuru limekwisha kwa amani.

    ReplyDelete
  7. Hongereni sana kwa kufikia muafaka murua kabisa.

    Vijana sasa rudini shule na mukaze buti musome kwa bidii ili muweze kufaulu.

    ReplyDelete
  8. Someni, acheni visivyo na msingi. Dini ina wakati wake na Masomo yana wakati wake.

    ReplyDelete
  9. Kila nchi inasheria zake na wananchi wote wanapoaswa kufuata sheria zote za nchi bila kujali wana rangi gani, dini gani, wafupi, warefu nk, la sivyo sio nchi.

    ReplyDelete
  10. Ni vizuri tatizo limetatuliwa na wanafunzi wanaweza kurudi madarasani.

    ReplyDelete
  11. Vijana hao wanaonekana manunda tu! watatimuliwa tena! Kwa mara nyingine serikali imeonesha udhaifu wake kwa mijitu isyo na nidhamu. Mini ni muislamu lakini siwafagilii hata kidogo.

    ReplyDelete
  12. Sisi sote twamwamini mungu, lakini ninachokiona hapa ni ushabiki na misimamo ya kidini ya watu Wazima ambao si wanatunzi kwa maslahi yao. Wanafunzi wajue kuwa hawa watu wanaowachichea hawatawasaidia pindi wakipata zero na kubaki kuuza soksi mbili mtaani. Tukazanie elimu, ndio ukombozi pekee wa mtanzania. Dini zimeletwa tu Na watu Wa nje!

    ReplyDelete
  13. mdau uliondika tarehe Thu Mar 08, 05:34:00 PM 2012. Unalosema sio la ukweli, sababu ya wakristo wengi kupasi ni kwa sababu ya source ya ukoloni. Waislam wengi wamesoma baada ya uhuru. Na wale wachache waliosema kabla ya uhuru ilibidi waingie ukristo, kama wazee wangu wengi tanga( ikitaka maelezo nitakutajia majina ya watu wengi sana). Nikiwa na familia kubwa ambao ni wakatoliki, baadhi ya family member wangi walipata free ride ya wakiingia mlimani kupotea mkono wa kanisa.swala la udini, sio kigezo cha perfomance.watoto wawili ambao wamekuwa mazingira pamoja, religion will not be a factor on their perfomance. Even ethiest will perfom the same.naelewa swala hili ni nyeti.Na kutaka kuweka picha kwamba dini moja are more smart more than others is wrong. Mbona Nigeria mostly are more educated than christians.Mbona Indonesia, wako mbali sana in technology na nchi amabayo in a waislam wengi duniani.A lot of wagunduzi wa mwanzo walikua waislam, mfano algebra.Napenda kurudia tena dini sio kigezo cha perfomance in school, kama uwanja ukiwa fair kwa kila mtu.Ni kama kabila hamna kabila smart then the other.Although kuna makabila yamesoma zaidi kupita mengine in population. Napenda nieleweke sipendi kufungua mjadala wqa malumbano ya dini.Naamini na mimi ambaye nina familia wakristo na waislamu nina hali ya kusikika pia.Wengi wa familia yangu ni wakristo, 80% to 20% waislam.Mdau kwa maelezo zaidi send me your email nitakuelewesha vizuri with evidence.Kwa nini wakristo wengi wamesoma , compare na waislam in Tz.Ni kama amerika ni kwa nini wamerikani weusi wengi ni maskini compare to white.Ni kwa nini red indians wengi wako kwenye makambi in usa, na wengi ni maskini sana. Ni amjibu amabayo ibabidi urudi kwenye historia ndio upate jibu.Nitakuelewesha mingi ukinitumia elimu yako.I will explain you the source of the problem.Ni kwa nini viongozi wengi waislam wa kidini hawakusoma elimu ya dunia? Je uislam unakataza kusoma elimu ya dunia?Ni kwa nini leo in europe and states islam is the fast growing religion? kwa kuongezea sijazaliwa muislam.Na naishi usa.sijafika nchi yoyote ya kiarabu.Na kuna wazungu wengi sana waislam na weusi waislam huku.media za huku haizoneshi, waislam ni wengi sana.Kaka Michuzi naomba ujumbe huu uchapishwe na mimi nisikike, mawazo yangu.

    ReplyDelete
  14. Aisee..humu kny comments ndio unapata kuono Bongo za watu zilivyooza.
    Yani mtu anasema bila wasiwasi eti Dini ina wakati wake na Masomo yanawakati wake,Hivi ww unamkataba na M/Mungu kwamba atakuacha mpaka umalize masomo ndipo uje umuabudu?
    Twende mbele,mm ninaetoa mchango huu nilisoma shule ya vipaji maalum tz kuanzia form one mpaka form six na hivi sasa napiga Masters Ulaya(ALLAH aniepushe na Ria hapa najitolea mfano tu na sio kujisifia)..ni muislam namshukuru ALLAH kwakuniongoza na shuleni kwakipindi chote nilikua miongoni mwa viongozi wa wanafunzi wakiislam kuanzia ngazi ya shule mpaka mkoa..Je,kujituma katika kumtumikia ALLAH na kumuabudu ni ujinga?Mwenye kujitahid kufata dini yake hufeli?
    Kuna wangapi wasiofata dini na hwafaulu?
    Acheni kukurupuka na comments zenu zachuki na zisizo na mashiko.
    Mimi msimamo wangu nikwamba vijana lazima wapewe mazingira yakuafata dini zao na wapewe mazingira yakusoma kwa utulivu na umakini ili waandae futere zao na za taifa kwa ujumla.
    Nawakilisha..

    ReplyDelete
  15. Du, hawa wenzetu (sio wote)kwa kweli we acha tu serikali iwaogope!

    ReplyDelete
  16. Tunaelekea kubaya, tumefika mambo ya dini shuleni! Makundi, udini, ushoga, uchangudoa kuanzia umri mdogo sana na mashuleni, tumekwisha!!!

    ReplyDelete
  17. Kuna bwana hapo ambae ameomba apewe email ili aweze kueleza kwa undani kuhusu suala la elimu baina ya waislamu na wasiokuwa waislamu na inaonekana ana taarifa nyeti sana. Namshauri aiweke tu hapa kama comments hata kama ni taarifa ndefu na sie wote tutafaidika.

    ReplyDelete
  18. Naipoingeza serikali na waislam kwa kuonesha ustaarabu katika kuhakikisha kuwa suala hili linapatiwa suluhu. Ila nashauri serikali iangalie suala la ubaguzi si kwa Waislamu tu hata kwa watu wa madhehebu mengine ambao wanahisi kutengwa katika mfumo wa utawala na serikili kwa kuwa tu ni watu wa dini na madhehebu magodo.

    ReplyDelete
  19. Kwa kuwakumbusha tu Tofauti za kidini zitakuwepo tu siku zote kwa kuwa uislam ni njia ya maisha kwa ujumla wakati wengine ni kwa msimu, kwa hiyo misukosuko hii ipo tu siku zote (wao wana dini yao nanyi mnadini yenu),maoni yao hapo juu yanathitisha.

    ReplyDelete
  20. Penye ukweli oungo hujitenga! kwani ninini hakieleweki katika hili!? ibada msikitini, kanisani....shule darasani! Tuache kuwadanganya wadogo zetu,,,tuwashauri katika njia iliyo sahihi!

    Eddy
    Vancouver

    ReplyDelete
  21. AlhamdulilLah, wewe mdau unaesema kuwa waislamu eti wanfeli kuliko wakristo, mbona tunasikia mashule yenu ya kikafiri huwa yanawafanyia mtihani wanafunzi ili wafaulu na kuonesha shule inafanya vizuri, Serikali imeamua kwa busara na sasa watoto warudi wakasome..ALLAh awafanyie wepesi Amin

    ReplyDelete
  22. Bokoharam tu hawa, next year muangalie matokeo ya Ndanda Secondari, kwani ukiwa kwenye mazingira ambayo huwezi kusali kama nyumbani ukisali Alla hasikii sala zako?

    ReplyDelete
  23. Ndiyo, shule ilijengwa na kanisa na ikataifishwa, hivyuo ni mali ya serikali na kanisa halina nafasi ya kupenyeza sera zake.

    serikali ina jukumu la kuhakikisha usawa katika shule zake. ukiwemo usawa wa ibada. kama wakristo wanaabudu kwa amani na waislamu pia ni haki yao. kwa nini kuwa wabadilishe haki kwa elimu kwa
    vyote ni haki yao.

    kama vile shule za kiislamu zilivyotaifishwa hakuna maswala ya dini wala kunyanyaswa ndugu wa kikristo, vivyo hivyo inatakiwa kwa shule zilizokuwa za kikristo kwa wanafunzi wa kiislamu.

    ReplyDelete
  24. tatizo dogo serikali inashindwa kutatua mpaka maandamano ya nchi? hivi muafaka huu si uliwezekana mwaka jana? mbona wamekubali walichokataa wakati huo?

    inabidi wafanyakazi wa serikali wafuate miongozo za kazi na sio hisia za imani bila kujali dini.

    ReplyDelete
  25. tatizo dogo serikali inashindwa kutatua mpaka maandamano ya nchi? hivi muafaka huu si uliwezekana mwaka jana? mbona wamekubali walichokataa wakati huo?

    inabidi wafanyakazi wa serikali wafuate miongozo za kazi na sio hisia za imani bila kujali dini.

    ReplyDelete
  26. Safi sana! Hatutakubali kabisa Waislamu tunyanyaswe au kuiachia nchi hii iongozwe na kanisa kama vile chama kimoja cha upinzani kinavyotaka.

    ReplyDelete
  27. Mdau wa America na Ulaya nawaunga mkono sana kwa Comments zenu nzuri mno mno,,haziitaji kuishia hapa katika blog!
    Inatakiwa mjitahidi sana sana baadae mrudi nyumbani kuelimisha Umma wa kitanzania na jamii nyingi zilizopotea kwa kudhani eti Wakristo ndio wasomi,,Kweli ndugu yangu wa America umesema vizuri sana,ni kweli kwani hapa UK makanisa mengi yamekuwa misikiti,,na wasomi wa kikristo mapadri baada ya kusoma wameona ukweli,wamekuwa waislam,,,shuhudah tu kidogo andika katika Google ADHANA IN THE CHURCH something like that,utaona baadhi kidogo nikwambiayo,,,,
    Siko hapa kurumbana mambo ya dini ila wewe mdau uliyesema waislam mbumbumbu umenikasirisha sana,na wakati unajuwa sababu wa waislam wa kitanzania kuwa nyuma kwa ilim ya kidunia ni nini!Nafikiri mdau hapo juu kakueleza vizuri,,na mimi pia niko katika chimbuko la kizazi cha upande wa babu na bibi wakristo.
    Mdau hapo juu tena ukae uelewe Bila Mungu hapo usingekuwepo unaclick katika blog ya Michuzi,,kwanza Mungu Elimu baadae,,,sio utenge Dini na Elimu mbali,'IBADAH NDANI YA ELIMU'Mambo yatakwendea mswano,sio lazima watu waone,,Mungu tu akikuona inatosha!
    michuzi Ahsante kunirushia Comment yangu!
    JazzakAllahu Khairan

    Ahlam UK

    ReplyDelete
  28. Huyo anayesema Waislamu hawakupata elimu kutoka na historia, anadanganya. Je, anajua kuwa Waarabu ndiyo wa kwanza kuweka himaya huku pwani ya Afrika Mashariki? Nasema kuweka himaya, na si kupita!!!

    Pili, Waislamu walijali tu misikiti na kuwapumbaza watoto kushindia madrasa. Hawakujali kuwapa elimu dunia. Angalia, watoto wa Kiislamu wanashindishwa madrasa, wakati wenzao wakristo watoto wakisoma elimu ya dini na hapo hapo kuna huduma ya elimu, afya,michezo na kadhalika. Hivi unaweza kumsaidia vipi mtoto wa miaka minne ashiriki michezo wakati anashinda kwenye hijab na bulka? Mtoto mwenye hijab, aliyefunika uso, atakaguliwa vipi usafi? tena kwa taarifa yako ni kwamba siku hizi wanaokaguliwa usafi shuleni ni wakristo, maana watoto wa kiislamu ukiwatoa ushungi au hijab, ni balaa! Wazazi wataandamana hadi Ikulu!!! Bila kubadilika, Haki ya Mungu mtabaki mkilialia kila siku.

    ReplyDelete
  29. anaesema waisalam hawajasoma ni muongo.Bin laden alikuwa ni engineer, na ni organizer mzuri sana katika mamboya kigaidi. Mimi ni boko haram na nimekwenda shule. so what ?

    ReplyDelete
  30. Kama walifanya vurugu walikua na haki ya kuadhibiwa lakini kama hawakufanya vurugu walikua na haki ya kutetewa ili warudi shuleni na si kwa sababu ni waisilamu bali kama raia wenye haki ya kupata elimu. Kwa hiyo tusije tukaweka misingi ya kuteteana tu kwa sababu hawa ni wadini hii na wengine sio wa dini hii. Tunahitaji amani "tusilete udini"

    ReplyDelete
  31. MBONA WAMEVAA SURUALI NDEFU?SIWATAJITENGUA UDHU JAMANI?WAARABU WALITANGULIA PWANI KAZI IKAWA KUJENGA MISIKITI NA KUFANYA UZINZI TU WAAFRIKA HADI WAKAZALIWA WAKINA NANI HII WENYE NANIHII, SHULE KUJENGA HAKUNA

    ReplyDelete
  32. DINI ZOTE NI SAWA NA MUNGU NI MMOJA,ACHENI KUTOA MAWAZO FINYU,KAMA HAWA HAPA JUU,WANAANDIKA BARUA NDEFU ZISIZOKUWA NA MAANA YOYOTE.

    ReplyDelete
  33. minasema kwamba wote ambao mmetoa comments za hovyo au za dharau nadhani hamjui nini kinacho endelea humu nchini, kwakuwa nyie mijikristu mnafaidika na kudeka kwa serikari kwa kupewa hvy imekuwa nongwa anye kuku akinya bata kahara si ndivyo, wakristo wa tz acheni uzuzu wenu wa kupenda kupendelwa waislam pia wameamka wanataka haki zzao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...