Naibu Waziri wa Nishati na Mani, Adam Malima ( kushoto) mwenye kanzu, akiwaelezea  Waandishi wa Habari leo sehemu ya dirisha ambapo  wezi walivunja na kuingia Chumbani na kuimba vitu mbalimbali katika chumba alichopanga katika Hoteli ya Kitalii ya Nashera ya Mjini Morogoro.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Adam Malima ( kati kati mwenye kanzu) akifanua jinsi alivyolizwa na wezi  mabegi matatu wakiwa na vifaa mbalimbali baada ya dirisha la chumba chake kuvunjwa katika  Hoteli ya Kitalii ya Nashera ya Mjini hapa, ( kulia ) ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh Innocenti Kalongeries na (kushoto ) ni Meneja wa Hoteli hiyo, Eustusi Mtua .
Mchezo wote ulianzia hapa, anasema Mheshimiwa Malima.
 Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii, mji kasoro Bahari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Yaani wavunje dirisha wewe upo ndani, wasombe mabegi yote wewe bila kusikia. Haiwezekani. Hupo serious. Sema vizuri tukuelewe. Hiyo hoteli haina mlinzi au inakuwaje?

    ReplyDelete
  2. Dola 4000 Cash kaibiwa????
    Yaani hiyo ni trip ya Morogoro tu, je akienda nje ya nchi anabeba dola kiasi gani?
    Ama kweli siasa bongo ni mtaji tosha!

    ReplyDelete
  3. Wezi walifunja na kuingia chumbani? Wakaiba kila kitu mpaka nguo zake laini wakaacha bastola na bunduki? Hata mtoto mdogo hadanganyiki kwa haya.

    ReplyDelete
  4. I like this, mheshimiwa hayo yaliyokutokea wewe sisi yanatutokea kila siku - ujumbe umefika KILA JAMBO LINATOKEA KWA SABABU

    ReplyDelete
  5. Viongozi wetu Tanzania bado tu hawajaelewa kuwa kutembea na pesa ni hatari badala yake wanatakiwa kubeba visa au master cards. Kwakuwa Tanzania inaongozwa na viongozi wasomi duniani (PhD's) nilitegemea kuwa wangelielewa hilo.

    ReplyDelete
  6. Adam, mbona binafsi sijisikii kucheka wala kukupa pole....mbona dirisha linaonekana lilifunguliwa kwa ndani?......chezeya mji kasoro bahari weye!

    ReplyDelete
  7. none sence...hoteli gani ya kitalii ambayo mpaka vibaka wanaingia kwa ajili ya kuiba bila kuonwa wachilia mbali kukamatwa..hakuna ulinzi hapo?.

    inavyoelekea ni zile hoteli zenye masharti ya "kabidhi mali zako zenye dhamani pamoja na pesa taslimu kwa mhudumu au meneja kwa usalama zaidi" na nalazimika kuamini kuwa mheshimiwa malima alipuuzia hilo na wao wakaamua kumkomoa...hoteli zenye masharti hayo ni zile zenye wafanyakazi wezi...aliyeandika hii habari na au kui-edit kakosea sana kuipa hadhi ya kitalii ambapo hadi vibaka wana uwezo wa kuingia kirahisi bila kuonwa..maana ingekuwa ni majambazi sawa mtu unaweza kuamini...lakini hiyo ndo hali halisi ya wananchi wa Tanzania mzee malima, usijisahau sana kuwa hapa ni bongo hata kama unaamini upo katika hoteli unayoamini ni ya kitalii.

    ni mtazamo tu
    ahsante

    hsm

    ReplyDelete
  8. Mhe. Malima pole na mkasa!

    Hili ni tukio la Madai ya kufanyiwa Uhalifu hivyo tusihoji sana mazingira yake mfano:

    1.Kiasi cha fedha alizokuwa nazo,

    2.Alikuwa anafanya nini huko,

    3.Ni namana gani vimeibiwa vitu vingine lakini Silaha hazikuibiwa,

    Hayo matatu (3) hapo juu ni masuala Binafsi (Private affairs),,,Hebu angalia mazingira hayo matatu yanaashiria Mashaka dhidi ya Wahusika wa Hoteli kushiriki kwa namna moja ama nyingine.(1.) walijua anaweza kuwa na fedha au chochote kwa vile yeye wanamjua ni Bosi na kiongozi nchini(.2)walikuwa na upekupeku kujua amefuata nini Morogoro(3.)Waliogopa kuiba Silaha walijua itakula kwao!,,,wa nini waibe vingine lakini waache silaha?

    Cha Msingi ni kuuhoji Uongozi wa Hoteli kuhusu Usalama na kwa nini yeye Mbunge kama mteja mwingine yeyote yamtokee hayo ktk Hoteli inayojiita ni ya Kitalii?

    ReplyDelete
  9. Naona ka kamchezo ka kuigiza vile! Anyway na hayo maslaha yote ya nini yote baba Malima?

    ReplyDelete
  10. Hapa kuna maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Kwa mfano, Malima alikuwepo au hakuwepo chumbani wizi huo ulipotokea saa 10 alfajiri? Na kama hakuwepo, alikuwa wapi?

    ReplyDelete
  11. ....hizi sliding windows mafundi wakikuwekea vibaya wala hayana kazi kuyaondoa kwenye frame na kuyarudishia...

    ....na mafundi wasivyo waaminifu siku hizi, ukiibiwa wa kwanza anzana na mafundi....

    ReplyDelete
  12. Hiyo Hotel haina usalama kabisa. Yaani hakuna hata walinzi? Kituko hiki kimeiharibia sana jina Hotel hiyo. Nilikuwa na msafara mkubwa wa wageni kutoka nje na tulikuwa na lengo la kukaa kwenye hotel Morogoro. Kwa bahati nzuri tukio hili limetupa nafasi a kuikwepa hiyo hotel.

    ReplyDelete
  13. Hoteli za kitalii
    1. Zinakuwa na safe boxes vyumbani.
    2. Zinakuwa na ulinzi wa kuaminika hususan kwa watu wenye hadhi fulani.

    Wasiwasi wangu upo kwenye hizi siasa zetu za siku hizi zilizoanza kuingia umafia, kama kibaka unprofesional anaweza kupenya mpaka ndani kwa kiasi hiki na kfanikiwa kukwapua, atashindwa kupandikiza sumu na kuua kiongozi.


    Tuangalie mbali zaidi ya wizi.

    ReplyDelete
  14. mh usiangalie swala la wizi hiyo ni indicator ya kukata tamaa kwa vijana tunapoteza akili na nguvu kazi ya vijana wetu matukio ya vibaka huku site tumeacha hata kuongelea hebu tuanzishe jkt kwa nguvu zote.pole kwa mkasa.

    ReplyDelete
  15. Kweli wezi wameimba na sasa Mhs abaki kuitikia Coras. Pole sana.

    ReplyDelete
  16. dolaa 4000,millionn 2,pete zenye thamani ya mil 2,laptop,yeye mwenyewe ni mwizi tu,angalia maisha ya mtanzia yalivyo magumu ,unatafuta hiyo 100o kwa jasho kweli,wewe una dola 4000 na mil kadhaa,wala sijakasirika wamefanya vizuri tu,sisapoti wizi kwa situatin hii ni poa tu

    ReplyDelete
  17. Alikuwa peke yake au na 'familia' yake? Pole, mwenzio hakudhurika??!!!

    ReplyDelete
  18. Adam!kaka wewe umeenda shule,mbona unatoa maelezo yasiyo tuingia kichwani! Dola 4000?
    kwani?ulikua unaenda kufanya biashara gani?

    ReplyDelete
  19. Sidhani kama mwizi anaweza kuiba hadi chupi uliyovaa!

    ReplyDelete
  20. yaani silaha zote na kuiba wameiba next time bora uende mikono mitupu chezea wajanja wa MORO

    ReplyDelete
  21. Wewe mdau namba tano, unadhani visa na mastercard zinafanya kazi huko vijijini kama Kilosa alikotokea huyo Mheshimiwa? Au umesahau mfumo wa maisha yetu uko Ulaya kwa muda mrefu?

    Hata hivyo Mheshimiwa madola yote hayo kutembea nayo kwenye briefcase mhhhhhhhhhhhh!

    Mdau wa kwanza kama umechoka sana unaweza kulala na wataalamu wakafungua madirisha na kuondoka na vyao. Imewahi kututokea sisi, tulipoamka asubuhi tukajikuta wezi wameondoa vitu mpaka chumbani na sisi tumelala fo fo fo.

    ReplyDelete
  22. Waandishi wa Tanzania sio MAKINI kabisa. Yaani hii ripoti inasema ameibwa $4000 mara $400,000 yaani nyie mnajua $400,000? Dola laki nne hizo ni hela za Chenge itakuwa jambo la ajabu kama alikuwa na DOLA LAKI NNE mfukoni.

    ReplyDelete
  23. Aina ya wizi huu imekithiri sana Morogoro na mikoa mingine, unaamka asubuhi unakuta auliyekuwa naye keshaku-search na kasepa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...