Muda mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini Dodoma,Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mh. Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria za Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Baada ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika,kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?


Mh. Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naomba tu nitoe shukran kwa taarifa. Ila nina shaka na neno "answered" kama ni sahihi. nadhani ni "Hansard".

    ReplyDelete
  2. Kupevuka kisiasa. Safi

    ReplyDelete
  3. mambo yote bunge la bajeti lijalo.mama atachanganyikiwa safari hii.ndio tutajua unavyoupenda umasikini wa bungeni anaousema huyo mama

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Makinda pliiz acha hili la kupiga liendelee.Hii itarudisha adabu kwa bahadhi ya viongozi wanaomuhujumu Rais wetu..Tunamsumkumia Lawama rais lawama bure..Na hii itatusaidia kusonga mbele kama nchi..nchi ina kila rasilimali..Tunataka discpline serikalini kwa sasa.Bora LOWASA...

    ReplyDelete
  5. Safiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...