Mchezaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza katika mchezo wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inayomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa huku ikiwa tayari ni mabingwa wa ligi hiyo,


Mpira umeisha na Simba wanaondoka kidedea kwa bao 5-0 
dhidi ya mtani wao wa jadi Yanga.

Goli la pili la Simba limefungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache zilizopita tayari Emmanuel Okwi ameongeza goli la tatu. Kipa  Juma Kaseja ameongeza lingine kwa penati wakati Patrick Mafisango amepiga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2012

    wera wera

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2012

    Ohhh nooo hiyo ni Yanga ama Seychelles Mnyama kafanya unyama!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2012

    laana za walioitwa wazee wauza unga nini, mbona hainiingii akili yanga kuchezea kichapo kikubwa namna hiyo na hapo nasikia refa amejaribu kuwalindia heshima vinginevyo zingekuwa double digit, masikini yangaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2012

    Tusisikie machafuko ndani ya Yanga.Huo ni mpira tu, kumbukeni hata Man U alishawahi pigwa 6-1 na Man City. Kuweni wapole kwa sasa. Jipangeni kwa msimu ujao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2012

    Wewe acha kupunguza digits Man U alikula 6 - 0 dhidi ya Man City na sio 6 - 1 kama ulivyosema.

    ReplyDelete
  6. That's Mnyama, wooooooooWwwwww

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2012

    Mimi ni Simba damu tangu nikiwa mdogo, nimefurahishwa sana na ushindi huu na ubingwa kwa ujumla.

    Lakini kama mwana michezo, kuna fundisho hapo, migogoro ndani ya Yanga ndio iliyoleta kipigo kikubwa hivi. Sina maana wasingefungwa, kufungwa kulikuwa pale pale lakini ingekuwa 2-0 au 2-1 hivi.

    Yanga wamekuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu na amefungwa kule kanda ya ziwa na hata juzi tumesikia wazee na viongozi wakiitana wauza unga. Kwahiyo katika mazingira hayo kipigo hiki ni kitu kisichoshangaza kabisa.

    Lakini, pia tutegemee mgogoro uliopo kupanuka na kuwa gogoro. Sijui kama Nchunga atapona. Haya yote yawe mafundisho kwa timu nyingine ikiwemo Simba tunaocheka leo. Wote tunaelewa mpira fitina ni sehemu ya timu zetu Bongo.

    Hongera sana wanasimba na poleni wanawayanga. Jipangeni vizuri kumaliza mgogoro uliopo na kusuka timu nzuri kwa michezo iliyoko mbele na ligi ya mwakani.

    Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...