MKUU wa wilaya ya Nachingwea,Mkoani Lindi,Bi Regina Chonjo amewataka wananchi wa wilaya hiyo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kumpa ushirikiano wa karibu ili aweze kusimamia kwa ukamilifu fursa zilizopo wilayani humo kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo yao.

Chonjo alisema hayo wakati akizungumza na  waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo katika hafla iliyofanyika katika manispaa ya Lindi kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hakuna sababu ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea kuendelea kuwa masikini hasa ukizingatia fursa nyingi zilizopo katika wilaya hiyo ikiwa ardhi nzuri isiyohitaji kuwekewa mbolea za viwandani,mvua za kutosha zinazowezakustawisha mazao,misitu na kuwapo kwa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Dhahabu na Nikel.

Alisema kuwa atatumia changamoto za mkoa huo zikiwemo za elimu,afya na kilimo kama kipaumbele chake katika kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye mipango yote ya maendeleo ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.

''Ninayo taarifa kuwa wananchi wa wilaya yangu ni watu wanaopenda kujituma katika shughuli za kuwaletea maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kilimo ambacho huwafanya wananchi wa wilaya jirani kutegemea mazao ya chakula kutoka Nachingwea mimi kwa hakika sitawangusha kama iivyompendeza mhe Rais na kuniona ninafaa kumsaidia''.

Jitahada za kujitolea na kuhakikisha utawala bora unakuwepo Wananchi wa wilaya hiyo wameweza kujenga jengo la ghorofa kwa ajili ya ofisi ya mkuu wa wilaya na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa nguvu na pesa zao.

Katika hafla hiyo wakuu wapya wa wilaya tano za mkoa wa Lindi waliapishwa ambao ni Agnes Hokororo (Ruangwa),Dk Nasoro Hamidi (Lindi),Abdala Ulega (Kilwa),Mfinga Mmbaga (Liwale) na Regina Regnald
Chonjo mkuu wa wilaya ya Nachingwea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...