Na Mwandishi Wetu

ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.

Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.

Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.

“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Salute Madame Rittah! Nakukubali sana kwa jitihada zako za kuinua vipaji vya wasanii waliokosa fursa za kuonyesha vipaji vyao hapa Bongo. Master J na Salama; kazi kwenu kuwezesha mchujo uende vyema kupata cream safi. Mungu Awabariki Sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...