TAFSIRI YA KISWAHIRI JUU YA AMRI 
HIYO YA MAHAKAMA KUU

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

·        Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
·        *Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

·         *Wajibu maombi, ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
·        *Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
·        *Kuwepo na makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.

Kwa misingi hii, Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini, na wanachama wake, inaamuru kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2012

    Inasikitisha kusikia mgomo huu wa madaktari kila siku! Tanzania ni nyumba yetu yenye mzazi na watoto wengi! inapofikia hatua mtoto mmoja tena ambaye jamii imejinyima na kumsomesha ili aje aisaidie anageuka na kudai haki zaidi bila kujali kuwa wapo wengine pia hicho kidogo kilichopo tunahitaji kitukomboe kama yeye inatia wasiwasi! Kama ni utu au fikra za ubinafsi au msukumo wa kisiasa na kiu ya madaraka! italiua taifa letu hili lililokuwa na amani miaka mingi! Mwanzo wa ngoma ni lele hii ngoma inaelekea kubaya! Sidhani baba mzazi atamkatalia mwanaye kumpa anachokitaka kama kipo cha kutosha! Mzazi hujua ndani ya chungu kuna nini na huwafikiria na watotot wengine! Kukubali tu kwa shuruti si busara! Je sis machinga sisi Askari sisi Walimu sisi wafanyakazi wengine tusemeje pia tudai kama wao hawa waliosomeshwa kwa kodi za watanzania masikini? Leo kujinyima kwao kunawatesa na kuwaua wakiwa Mahospitalini hawana msaada wa watoto na ndugu zao waliojinyima ili wasome na kesho walisaidie Taifa hili? Pesa kila siku hazitatosha hata ungelilipwa mamilioni! Busara itumike na pande zote. Watetezi wetu wengine wanashangilia lakini vita havina macho! Mtego huu wa panya unaweza kutuua hata tusiokuwemo na Taifa likageuka damu tupu na vilio kwani mwanzo wa ngoma ni lele! Eee Mungu tunusuru na hili kwani lina mkono wa mtu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2012

    Hivi mimi niulize, Rais Kiwete ameshindwa kutatua tatizo hili la madactari au ni nini hiki, wanamdai shilingi ngapi mpaka anashindwa kuwalipa tuambieni pengine tunaweza kusaidi serikali yetu, sisi wengine ni mamillionea huku hatutaki aibu iipate nchi yetu tuipendayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Hongera serikali... madaktari "came back to your senses!" don't act childish... mnajua serikali haiwezi kulipa mnavyotaka! sasa nini kujitutumua kipuuzi! kubaliani mliyotimiziwa, tena ni makubwa SANA! halafu mengine muendelee kuongea.

    Mnajifanya zaidi sana? Acheni ujinga.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2012

    Hivi nyie madaktari mbona mnakuwa kama hamjaelimika? mbona mnadai mambo ambayo mnajua kwa nchi yetu ni vigumu kutimilika, kama mlikuwa mnataka mishahara mikubwa namna hiyo mngesomea upilote au engineering ili muweze kuishi kifahari. Kwanza mlisomeshwa bureeeeeeeeeee sasa mnataka nini mbona hatuoni mlichozalisha na mnachokitaka. Ni watu wangapi wamepoteza maisha kwa hiyo migomo yenu hamna hata huruma jamani. Hebu geukeni mridhike na walichowapa sana sana hizo milion 3.5 mnazodai pamoja na 125% ya nyumba pamoja posho nyingine mtafanya kazi kweli? kwa ninavyowajua watanzania mataishia ulevi,ngono na uzembe kazini. acheni hizooooooooooooooooo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2012

    serikali nayo imezidi jamani eeh..sasa sijui hata cha kusema maana kuna wanaoneemeka na hicho kinachosemwa ni kidogo lakin wengine nao wakitaka wapewe chochote kutoka hicho kidogo wanaambiwa oooh,tumewasomesha, sijui sekta muhimu hairuhusiwi kugomaa, maneno kibao alimuradi dhulma mtindo mmoja tu..madaktari nawashauri kitu kimoja, fanyeni ziara nchi nzima waelimishemi watanzania juu ya madai yenu halafu hao wananchi watagoma kwa niaba yenu wakati huo nyie mnaendelea na kazi yenu kama kawaida.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2012

    THANKS TO GOD I LEFT THE HELL CALLED TANZANIA! MNAKAA HAMTHAMINIWI ANGALIENI RWANDA INAVYOWALIPA MADOKTA! sasa hv wadokta wanakimbilia huko, MIMI NI DR. NA NINAFANYA KAZI UJERUMANI NA SIJUTII KUONDOKA MAANA NI DISASTER, MTU UNAFANYA KAZI WAGONJWA WANAKUFIA KWASABABU TU YA UZEMBE WA SERIKALI! wenye kuona hao wanaogoma ni machizi basi wakajaribu wao kufanya hiyo kazi km wanadhani ni rahisi kuoina kila siku watu wanakufia mkononi kwasbb ambayo iko ndani ya uwezo wa serikali, NI VIZURI WAKAE TU NYUMBANI KULIKO KUKAA HOSPITAL WATU WANAKUFIA OVYOOVYO!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2012

    Hivi wabunge na watu wengine hamuwaoni?daktari na mbunge nani muhimu?daktari na mkurugenzi?nani anafanya kazi kwenye mazingira magumu na inayoonekana?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2012

    Kiswahiri?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...