Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM),Mh. Omary Ahmed Badwel (43) akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi,Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM),Mh. Omary Ahmed Badwel (43) akipelekwa kusomewa mashtaka yake leo Mahakama ya Hakimu Mkazi,Kisutu jijini Dar es Salaam.

Picha/Habari  na Francis Dande wa Globu ya Jamii.


MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel (43) leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa makosa ya rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Jonathan Liana.

Wakili wa Takukuru,Janeth Machullia na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa.

Wakili Machullia alidai kuwa kosa la kwanza ni la rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam , Badwel akiwa ni Mbunge wa Bahi na Mjumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wakati huo akiwa ni ofisa wa serikali kwa maana ya sheria ya Takukuru, alitenda kosa la kushawishi ili apewe rushwa ya jumla ya Shilingi milioni nane toka kwa Sipora Liana ili kiasi hicho cha fedha aweze kuwapelekea wajumbe wenzake wa Kamati hiyo ya Bunge ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya mwaka 2011/2012 ya Halmashauri hiyo.

Wakili Machullia alidai shitaka la pili ni kwamba kati ya Juni 2 mwaka huu, katika Hoteli ya Peacock,mshitakiwa akiwa na nyadhifa zake zote hizo alipokea rushwa ya Milioni moja kutoka kwa Liana ili aweze kwenda kuwashawishi wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya Halmashauri ya Mkuranga huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Hata hivyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki alikanusha mashitaka yote na wakili wa Machullia alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi Kahamba alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni nne na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani, sharti ambalo lilitimizwa na mshitakiwa huyo na akapata dhamana.

 Hakimu Kahamba aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    mbona wabunge wenginewe na viongozi wenginewe wa serikalini hawajafanyiwa haya na bado wako mitaani na katika mikoa yao yakitamba na kufanya shughuli zao kama kawaida

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2012

    Hii yote ni tamaa, hawa jamaa pamoja na madiwani walizoea hadi ikaonekana ni kawaida sasa vijisenti hivyo vinamuumbua mbele ya dunia!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2012

    Kama ni kweli huyu mheshimiwa atakuwa kaivalia njaa kibwaya..milioni moja tu imemtoa imani??siamini lakini ndio kakamatwa na tonge mkononi...aibu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    Duh!Money will never be enough!!!Kweli Mbunge mzima na mshahara wote,sitting allowances na marupurupu mengine bado tu uridhiki unaenda kupokea rushwa ya 1M???Aingii akilini.Anyway lets wait for the court ruling.Ila kama ni kweli ni aibu kubwa kwa familia yake na Bunge kwa ujumla.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2012

    yaani pesa zote hizo mnazopata bado mnaomba rushwa, tena huna hata aibu kuwa mwislamu kuomba rushwa!, au sio mwislam bali jina tu linanitatiza mimi?...mwislam kakatazwa kuchukua riba achilia mbali rushwa...bora upelelezi umekamilika ili uwahi kwenda gerezani na ubunge apatiwe mtu mwadilifu..watanzania tuchitahidi kutafuta riziki zetu za halali tu lakini hii nchi imeoza kwa uchufu wa kila aina,wizi,ufisadi,rushwa,biashara ya ngono,madawa ya kulevya,ushoga n.k bora yao wanzn wanaomba wajitenge...

    aaahh!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2012

    Mmewanyima sitting allowance matokeo yake ndiyo haya sasa(just saying)

    David V

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2012

    Kazi nzuri Sipora Liana. Umethihirisha kwamba Wanawake ni Jeshi Kubwa. Ukweli utawaweka huru kweli kweli. Mwisho wa Ufisadi/Uovu ni Aibu!

    Thadei Richard

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2012

    Mmmmh! Ni hapo Tz au?

    ReplyDelete
  9. Mwangwitwa ChrisJune 04, 2012

    ccm oyeeeeeeeeeee,kweli ccm mtapambana na rushwa si rahisi,mbunge wenu huyoooo na kesi ya rushwa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2012

    Mhe. Omary Ahmed Badwel,

    Na wenzako halafu ohhh Bungeni umasikini hakuna fedha!

    Sisi tunakula kwa bahati mlo mmoja ni mashaka,tunatembea kukata mbuga na kuchacha kila siku.

    Kwa dalili hizo inawezekana hata hicho Kiti cha Madaraka umekipata kwa njia hizo hizo za kutenga 'mafungu' ya fedha!

    Leo wenzetu mnahomola bao moja Tshs. 1,000,000/= hivi kwa mabao kama ya miezi mitatu (3) gharama ulizotumia kuhonga ili upate hicho kiti hujarudisha?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2012

    Aaah. Sasa naanza kuona mwanga wa tunakoelekea. Safi sana Mkurugenzi na naomba wengine wafate nyayo zako. Yaani kweli wabunge mnaotukomba kwa kulipwa posho nene bado na nyie mnaomba na kupokea Rushwa. Mungu yupo mtakamatwa wengi siku si nyingi. Huyu mkurugenzi apewe u RAS aiseee. He/she is one of the kind!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2012

    Mnhhhh kwa Mibao ya kiwango hicho cha Shs. Milioni 1 kazi moja tu?

    Kama ni hivyo ina maana Bungeni ni zaidi ya SACCOS !!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2012

    Hahahahahaha,

    ASSALAMA LEKKO zako Mhe. Sugu hadi sasa ukiwa Mheshimiwa Mbunge kwa kuijali kazi yako ya Taaluma ya zamani ya Muziki!!!

    Ndio maana kila mtu anaacha Taaluma yake anakimbilia kwenye Ubunge !

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2012

    Tunataka na hao wenzake wafikishwe mahakamani kama kweli.
    Waliohusika wote tunawahitaji,maana makachero wetu wanawajua wote na wameanza na huyu.
    Kumbe ndio bajeti zinavyopita?
    Yupo wapi yule jamaa aliyechangisha pesa kuwalipa wabunge wengine kupitisha bajeti yake???????

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2012

    Mwislamu anaonewa jamani!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2012

    Ndivyo ilivyo hata mambo yanaweza kuwa mazuri ukaandikiwa vibaya au isipitishwe mpaka chapaa

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2012

    Huyo ni mmoja kati ya mia na themanini!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2012

    Nakubaliana na mdau Na 1 hapo juu, wengi wako mitaaani. Ni serious case naona lakini huyu anaonewa tu. Why him only? The only solution in JK kuvunnja Bungu ili tuchgue new MPs. Na itakuwa makosa yetu if we vote for law makers who break the laws. Wake up wabongo he is not alone!!! Angalieni jinsi ubunge unavyogombewa siku hizi, kuna chakula huko ndani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2012

    sasa kazi imeanzaaaaaaaaaaaaaaaa safi sana milion moja imemponza

    ReplyDelete
  20. Ndugu yangu ulio weka ujumbe 'muislam anaonewa huyo' kama kejeli au tashtiti ni vizuri uwemakini na vitu kama hivi kwani kudhalilisha jamii kunaleta madhara makubwa. Tujihadhari sana na amani tuliyonayo Tanzania,Labda ugeni tulionao wa kuwa huru kueleza mawazo yetu unatufanya tushindwe kufikiri na kujua uzito wa tunayo andika. Ningeomba tumuone Mheshimiwa mtuhumiwa kama ni yeye mwenyewe binafsi anae daiwa kufikwa na tamaa ya ufisadi na wala sio kabila,rangi au dini yake iliyomtuma. Ubaguzi wa aina yeyote ile ni hatari sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...