Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration).

Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhika kwamba madaktari hwote ambao majina yao yameorodheshwa katika Taarifa hii, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.
Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.

Imetolewa na:
Dkt Donan Mmbando
MWENYEKITI- BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA
11 Julai, 2012.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2012

    Tanganyika ndio nchi gani???

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2012

    MICHUZI MIMI NI MUKUFUNZI WA MEDICAL HEALTH CARE HERE IN CANADA I AM DOCTOR IN MY PROFESSIONAL AND VERY SMART IN DEED. I AM VERY PREFERABLE SHOCKING THIS IS VERY SAD WHY DO NOT THEY DO LIKE HERE IN CANADA? BECAUSE HAVING GOVERMENT CONTROLLING HEALTHCARE THIS IS VERY CUMBERSOME AND INDEED DANGEROUS ALSO I CAN NOT SERIOUSLY UNDERSTOOD WHY WE CONTINUE TO WORK AND INSTEAD PEOPLE SHOULD PRACTICE WHATEVER IS AHEAD OF THEM AS FAR AS MEDICAL RESPONSIBLE IS CONCERNED. VERY VERY TOUGH FOR THEM WHEN THEY CAN NOT WORK OTHER JOB WHEN NEEDED BY SOCIETY AS LARGE.I AM VERY TICKLED BY THIS SITUATION WHICH IS UNCONTROLLABLY AND TREMENDOUS DANGEROUS TO THE ECONOMY AND PEOPLE HEALTHY GOVERMENT SHOULD THINK AND FOCUS ON THESE MATTERS.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2012

    Is this true? I can't believe on wot am reading. Serikali siyo ya kuchezea bwana, itawabana hao madaktari mpaka wakione. Look the MPs get Tsh 400,000 a dat just to sit in Dodoma, kima cha chini wala hakikaribii hiyo allowance ya MP.
    I remember in the early 1970s sisi tulifukuzwa Dar Uni kwa kupinga mishahara ya wabungu, oooh God, KAMATA na mapolisi walitupeleka kwetu,we stayed for 3 months.Na leo hii wanaofanya yaleyale wengine ni wabunge na hat mawziri. Government siyo ya kuchezea. Poleni wana bongo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2012

    Sipo katika mada kuu kama ilivyoelezwa na M/kiti wa baraza la madaktari, bali nipo katika kuuliza ili niweze kufahamu, hivi hili baraza la madaktari "TANGANYIKA" hili neno (TANGANYIKA) hapa linawakilisha madaktari wa Tanzania bara tu au lina maana nyingine ambayo ningeomba nami nifafanuliwe ili niielewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2012

    du!
    Jamani wadau mmeona hyo nembo?
    Hao madaktari mi sichangii chochote.
    Kwa anaefahamu maana na saili ya hiyo nembo pls share with me(us)

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2012

    Mbona Simwoni Dr. STEVEN ULIMBOKA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 11, 2012

    Mjomba tupe Brealing newzzzz ya Hukumu ya Kesi ya Wizi Ubalozi wa Tanzania Italia.

    Leo unatuletea Migomo ya Madakitari iliyokwisha pata suluhisho tayari!

    Mbona Ankal unatukwaza hivi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 11, 2012

    Mimi nadhani wakati umefika kwa serikali kuonesha kuwa ipo!

    Tumechoka kuona kikundi cha watu wachache wenye chuki na ajenda zao za siri wanatuharibia Nchi huku wakijifanya kua wao ndio wenye uchungu na nchi peke yao.

    Serikali ikumbuke hawa watu, wamejipanga na wanatumia kila sekta ambayo inawezekana.

    Baada ya kuviteka vyombo vya habari, wanaharakati na Taasisi fulani za dini, sasa wanaanza kuingilia sekta nyeti kama matibabu.

    Kiburi kimezidi sasa wanamdharau mpaka mkuu wa nchi, baada ya kuona wamefanya vibaya, sasa wanajishtukia eti wanataka kudhuriwa na vyombo vya usalama!

    Serikali onesheni uwepo wenu nasi tupo nyuma yenu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 11, 2012

    Kwa kweli, tumeanza kufarijika, angalau sasa serikali inaanza kuchukua hatua.

    Serikali lzima ioneshe uwepo wake sio kuwaacha watu wachache na wenye nia mbaya watuharibie Nchi.

    Ukweli ni kwamba kuna watu wanataka kuihujumu serikali kwa kushawishi migomo ili kukipatia umaarufu 'CHAMA FULANI'cha siasa!

    Walianza kushawishi wanafunzi, viongozi wa Dini, baadhi ya vyombo vya habari na sasa Madaktari.

    Mimi nasema upole umetosha, kwani sasa baadhi yao wanaanza hata kumdharau mkuu wa nchi.

    Serikali iwe makini, sasa hivi hata ktk baadhi ya maofisi tunashindwa kufanya kazi kwa siasa za chama fulani!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2012

    Safi sana! Watanzania tusikubali kuwa blackmailed na wahuni na wauaji wanaogoma.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 12, 2012

    I hail Medical Council of Tanganyika for taking some necessary steps as a professional body. Sheria zinazotawala fani hii ya utabibu ni muhimu ikafanya kazi zake vizuri na kuwakumbusha madaktari kuwa hakuna haki inayokwenda bila ya wajibu. Ni sawa kudai haki zao lakini walitakiwa watambue wajibu wao kama professionals.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2012

    Hii kasi na nguvu ya serikali ingekua hivi na kwenye wizi wa mali za umma na country resources ingekua rahisi hili somo kueleweka.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 13, 2012

    hawa ni vijana waliomaliza chuo mwaka jana! majina mengi ni watu niliosoma nao! Uonezi mtupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...