Mwanamuziki wa Nchini Uganda,Jose Chameleone (ambaye hivi karibuni alikuwepo hapa nchini kwa shoo yake moja) leo amefanya maandamano mpaka Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda akiambatana na wapenzi wa muziki wake,kwa lengo la kutaka kurudishiwa Passport yake inayodaiwa kuwa inashikiliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers,Erick Shigongo.hapa akizungumza na askari wa Ubalozini hapo.Inasemekana kuwa Shigongo aliamua kuchukua uamuzi huo wa kuchukua passport ya Jose Chameleone kwa kuwa Meneja wake alimtapeli kiasi cha dola 3500 kipindi cha nyuma hivyo ameamua kuzuia pasport yake mpaka atakapomleta Meneja wake huyo.
Mwanamuziki Jose Chameleone akipiga gitaa lake na kuimba huku wapenzi wa muziki wake wakiwa wamemzunguka kushinikiza Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kufanya taratibu za kuwezesha kupatikana kwa hati yake ya kusafiria (passport) inayoshikiriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers,Erick Shigongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Mrudishie pesa yake baba acha utapeli, ndipo utapata hiyo passport hapo mbona unahizalilisha tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    Wewe vipi! acha valu valu zako bana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2012

    hahahha kweli chameleoni dataz kaona aimbe na kuimba kbsaaa nje ya ubalozi duh ila hii ingeleta balaaa huko mbeleni kama asingerudishiwa nahisi nchi mbili zingeingia matatani!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    Huyu msani wa Uganda Bangi nyingi analetea utapeli Wasomi... Unacheza na Shigongo.... Chamelion kajiaribia akija bongo inabidi tumalizane nae. Aandike maumivu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    Frankly speaking, Shigongo hakutakiwa kuzuia hati ya kusafiria ya mteja bila kuwa na amri ya mahakama. Alichotakiwa kufanya wakati Cameleon akiwa Tanzania ni kumuitia polisi na kuomba court order ya kumzuia mwanamuziki huyo kuondoka nchini mpaka pale atakapolipa deni la $3500. Kwa mfanyabiashara kama Shigongo hii issue ina more negatives kwa foregn customers than getting back $3500.

    Tujifunze kufuata sheria kwenye mambo ambayo yapo obvious. Sasa huu uhasama wa mpaka kufika ubalozini ni mmbaya zaidi. Ni wakati sasa Shigongo akatumia mahakama kwenye hili suala, ubabe tufanyiane wenyewe wabongo kwani tunajua tutakavyomalizana kuliko kuwafanyia watu wa nje ya Tanzania, hata kama ni tapeli unatakiwa kutumia sheria kukabiliana nae.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2012

    NYIE mnaochangia naona hamjawahi kuwa na Passport,labda nyinyi mnazo pasipoti,Kwa kuwa passport yoyote dunia nzima imeandikwa kwa Pass za TZ kwenye ukurasa wa mwanzo za zamani,Nanukuu

    " Ni hati yenye maana saana,na hairuhusiwi kuchukuliwa na mtu yeyote asiehusika,hairuhusiwi kusafirishwa kwa njia ya posta..."

    NARUDIA TENA MTU YEYOTE AKIWA RAISI AKIWA KIONGOZI na ni makosa sana ndio maana balozi wanakata kutoa passport kwa niaba na ndio maana wanasafiri wenyewe kutembela kama Greece na nchi nyengine.

    Usikubali kuwa mpumbavu unaposafiri ukamuachia hata staff aseme nitakupa pass yako ukifika,nishaona watu wanaambiwa hivyo kwenye Ethiopian airlines....
    MSAFIRI LONG TIME

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2012

    Atunge wimbo mzuri, unaohusu sakata hili, halafu atuimbie atauza sana albamu hiyo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2012

    Nageria nao matapeli tu, hawana lolote, sikutegemea STAR kama Chamelion ananjaa ya $3500.Imenishangaza sana nipesa anayoweza kuipata kwa siku tena za kazi si weekend. Chunga Tamaa mbaya... kumbe nayeye inamgusa..hii kali.Asante 20%

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2012

    Passport hapati hadi afuate Mashariti ya Mkataba!

    Chameleone aelewe ya kuwa Wa-Tanzania tunasemekana hatukusoma lakini sisi ni werevu sana!

    Kwanza yeye Chameleone ana kosa namba moja ni kuondoka Tanzania na kusafiri bila Pasipoti.

    Amevunja Sheria za Uhamiaji inabidi afikishwe Mahakamani Tanzania ajibu makosa hayo ndio adai Pasipoti yake.

    Aache ujinga wake na bangi zeke za Kiganda.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2012

    Hao Waganda wenzake na Serikali yake ajieleze amerudi vipi nchini kwao Uganda bila kusafiri na Pasipoti?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2012

    Chameleone ajifunze kuwa Bongo tambarale asilete ujinga wake hapa!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2012

    ..kwani shigongo ametapeliwaje...stori haina details...watu wana comment bila full details la tukio.in any case...kesi ya $3500 imefikia hadi magazetini na kwenye blog....sijaona mahitaji ...kibiashara si nzuri kwa cameleon wala shigongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...