Jengo la nyumba ya walimu ya skuli ya Sekondari ya Kusini, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja yenye uwezo wa kubeba familia mbili kwa mpigo ambalo bado halijakamilika.

Jumuiya ya Maendeleo ya Watu wa Mzuri Kaja (Mzuri Kaja Development Society – MKDS) kwa heshima kubwa inawaomba Watanzania kusaidia kukamilisha jengo la nyumba ya walimu linaloonekana kwenye picha. Jengo hili limekusudiwa kukaliwa na walimu wa nje na ndani wanaotaka kujitolea kufundisha Skuli ya Kusini katika masomo ya Kiingereza, Hisabati, Biologia, Fisikia na Kemia. 

Mradi huu ulioanzishwa na wananchi wa Mzuri ulipata baraka ya kuwekwa jiwe la msingi na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein wakati huo akiwa Makomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. (Angalia picha kwenye mtandao wetu www.mzuri-kaja.or.tz).

Mchango tunaoumba kwa Watanzania wenzetu ni kwa ajili ya kupiga plasta ukuta wa nje unaohifadhi jengo lenyewe, kununua mlango wa geti, rangi, vifaa vya umeme pamoja na gharama ya kuunganisha umeme ambao upo mbali kidogo na jengo lenyewe. 

Jumuiya yetu iko tayari kupokea vifaa au fedha ambazo zimekadiriwa kufikia Milioni kumi –Tsh 10,000,000. Akaunti yetu ipo katika BENKI YA WATU WA ZANZIBAR na inajulikana kwa jina la Mzuri Kaja Development Society. Akaunti na. 021208000729

Wananchi watakaopenda kuchangia vifaa tunawaomba wawasiliane na mimi Mohamed Ameir Muombwa, Simu 0773539504 barua bebe mmuombwa@hotmail.com.

Nyumba yetu ya familia mbili ina vyumba sita, kila upande vyumba vitatu. Kuna vyumba viwili vya master, kimoja kila upande; kumbi mbili za kulia kila upande ukumbi mmoja; kumbi mbili za kupumzikia mmoja kila upande, vyumba viwili vya majiko, kimoja kila upande; sehemu mbili za ua kwa ajili ya kuanikia nguo. Vyumba vyote na vyoo vimewekwa taili.

Tunaomba mtuunge mkono ili tuweze kukamilisha azma yetu ya kupeleka mbele gurudumu la maendeleo ya elimu.

Tunatanguliza shukrani zetu kwenu ndugu zetu Watanzania.

Mohamed Ameir Muombwa
Mratibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mzuri-kaja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Kodi tunazotoa zinafanya kazi gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...