TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
         Bw. Asah Andrew Mwambene (pichani juu) ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012.  
Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). 
Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar. 
Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini. 
IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
   NA MICHEZO
 AGOSTI 1, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera Asah,

    Nenda Kapige kazi, usituangushe.

    ReplyDelete
  2. Congratulations mr assah. Rais kafanya uamuzi mzuri.Lazima vijana tuoate nafasi .sisi ndio taifa la kesho .Jama ni mchapa kazi ile mbaya.Big up

    ReplyDelete
  3. Usilete aibu kama Zitto; kapige kazi ofisini, fungia magazeti ya kihuni yote. Kataa rushwa kabisa kabisa. Shemeji yangu Zitto kashanyea kambi.

    ReplyDelete
  4. Hongera ila pana njaa sana pale na katibu mkuu wako ni mjeuri mnooo unaenda kufa njaa. All the best kijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...