Askari Polisi wa Kikosi cha Ulinzi wa Doria wanaotumia Pikipiki kwa jina la ‘ Chita’ ama ‘ Vodafasta’ wakilisindikiza Gari lenye namba T 747 ANJ aina ya Nissan Patrol baada ya kulikamata Jioni ya Augost 3, mwaka huu wakati wahamasishahi wake walipokuwa wakipita mitaani kuutangazia umma juu ya kufanyika kwa maandamano na mkutano wa kitaifa wa hadhara eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege , Manispaa ya Morogoro ambao ulipangwa ufanyike Augost 4, mwaka huu.

Mkuu wa Kituo Cha Usalama Barabarani Wilaya ya Morogoro aliongoza opapreshi ya kukamatwa kwa magari yaliyokuwa yakitumiwa na Chama hicho kupita mitaani kutangaza kufanyika kwa mkutano huo wakati Jeshi hilo likiwa limetoa amri ya kupiga marukufu kufanyika kwa maandamano na mkutano huo kutokana na sababu za kiusalama , kukamatwa kwa gari hilo na jingine namba T 622 CAY aina ya Ford Ranger ni baada ya kukaidi amri hiyo.

Hata hivyo majadiliano na mazungumzo kati ya Viongozi wa ngazi ya juu ya Jeshi la Polisi pamoja na wale wa Chadema ngazi ya kitaifa walifikia muafaka wa kusitishwa kwa mkutano huo na mandamano na Chama hicho kuruhusiwa kuendelea na mikutano yake Augoti 8, mwaka huu wakianzia Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa na Morogoro Mjini Augosti 18, mwaka huu, ambapo baadaye magari hayo yaliachiriwa pamoja na vijana kadhaa walliotiwa nguvuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. akina Ras Makunja si tuliambiwa wanapokea award ? Sasa inakuaje wapo morogoro

    ReplyDelete
  2. Hawa polisi wanachekesha kwelikweli. Sasa mlisema mnazuia mkutano na maandamano kwa kuwa hamna askari. Na hao waliotanda hapo kuzuia maandamano wametoka wapi?

    ReplyDelete
  3. Njaa tupu maskini hawa maaskari.....hata akiamuriwa kukamata mama zao wataenda ilhali mkono unendakinywani

    ReplyDelete
  4. Yaani ninyi polisi mnachakesha kuliko kiasi. Hao polisi si wangetumika kulinda maandamano badala ya kuzuia halafu mnawapeleka ili wapambane na waandamanaji. Nyie ndo mnaosababisha fujo katika nchi yetu. Acheni hizo. Kama mlisema hamna polisi wa kulinda maandamano na mikutano, hao wanaojiandaa kupambana na waandamanaji mmewatoa wapi?

    ReplyDelete
  5. Che GuevaraAugust 06, 2012

    Kusema kweli huu ni uonevu uliopitiliza! kwanini wazuiliwe? wangekuwa CCm wangezuiliwa?
    Huu wote ni woga ambao CCM wanawatumia vibaya jeshi la polisi kukidhoofisha CHADEMA!
    SAUTI ZA WENGU NI SAUTI YA MUNGU!
    People's powaaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...