Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Bwana Eric F. Shitindi (kushoto) na Mhe. Zayed bin Rashid Al-Nayemi (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar wakitia saini Mkataba wa awali wa mashirikiano katika masuala ya ajira baina ya nchi hizo.
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania na Qatar wakiwa katika kikao cha mashauriano kabla ya kusainiwa kwa Mkataba wa awali wa mashirikiano katika masuala ya ajira baina ya nchi hizo.
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Serikali ya Tanzania na Qatar walioshiriki katika kikao cha mashauriano kabla ya kusainiwa kwa Mkataba wa awali wa mashirikiano katika masuala ya ajira baina ya nchi hizo.
braza michuzi naomba ufafanuzi wa kina kuhusu huu mkataba wa ajila, yaani watanzania ndo watapata fursa za kufanya kazi qatar au nikuwka urahisi kwa raia wa qatar kufanya kazi kwenye makampuni yao nchini tanzania?
ReplyDeleteYale yale wako kwenye mikutano.
ReplyDelete