Wizara ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa barabara ambayo nchi ya Ujerumani imependekeza kuwa ingependa kuifadhili ni ile ambayo inaanzia Mto wa Mbu mkoani Arusha kwenda Mkoani Mara kwa kupitia nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kusini. Barabara iliyopendekezwa haitapita kabisa ndani ya Hifadhi hiyo.

Ufafanuzi huu umetolewa baada ya magazeti mawili ya hapa nchini yanayotolewa kwa lugha ya Kiingereza (toleo la tarehe 4 Septemba) kuandika kuhusiana na barabara hiyo bila kuweka wazi kuhusu ramani ya barabara ambayo Naibu Balozi wa Ujerumani aliitaja hivi karibuni alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii

Aidha, gazeti mojawapo kati ya hayo mawili, toleo la tarehe 5 Septemba 2012 liliandika tahariri iliyoonyesha kuwa barabara iliyopendekezwa itapita ndani ya Hifadhi ya Serengeti upande wa Kaskazini, hiyo siyo kweli maana Naibu Balozi hakusema hivyo.

Mazungumzo kuhusu suala hili la barabara ya Serengeti yalifanyika tarehe tarehe 3 Agosti 2012 wakati Naibu Balozi wa Ujerumani wa hapa nchini Bw. Hans Koeppel alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Khamis Kagasheki na kumwambia kuwa nchi yake iko tayari kufadhili upembuzi yakinifu na ujenzi wa barabara itakayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kusini kama nchi hiyo itaombwa kufanya hivyo. Waziri Kagasheki alilipokea pendekezo hilo na kuahidi kulipeleka kwa Waziri wa Ujenzi Mhe Dkt Magufuli.

George Matiko

MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe 8 Septemba 2012
Simu: +255 784 468047

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. As far as a FREE highway sponsored by one of the western nation my advised "Take the offer" hata wakitaka iwe inapitia Mtwara kwanza kabala kufika Serengeti - Mara "P'se take the offer" as they are pleased, hizo pesa mlizokuwa mjengee barabara sasa kajengeni shule za kutosha na madawati kama mtakuwa mmetia akili, otherwise endelezeni ufisadi wenu muile kama kawaida yenu serikali ya JK.

    ReplyDelete
  2. spinners at work.

    ReplyDelete
  3. Mnasema kufuatilia habari kupata uhakika ni gharama japo ni muhimu. Na hili je, mbona hata kwa mguu mngeweza kwenda wizarani? Lakini hata simu mkashindwa kupiga mnakurupuka tu? Mnadhalilisha taaluma yenu.

    ReplyDelete
  4. Wanawapeleke chaka. Mnajaribu kudai "dinosaur" ambaye huingiza taifa hilo zaidi ya 1bil USD kwa mwaka.... wanawapa ufadhili kwa kujenga barabara halafu msidai tena huyo mjusi wetu kutoka Lindi. ama kweli maliasili mnaopewa dhamana hamfikiriii kabisa... Dinosaur arejeshwe... tuuuu. tutaandamana.... nyie subirini tuuu

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau wa dinosaur, huyo mjusi na barabara lipi lipewe priority?

    Kwanza Ujerumani ndiyo kwa asilimia kubwa wanafadhili shughuli nyingi za humo kwenye hizo hifadhi. Unadhani mungekuwa nyinyi waTza si mungeshamalizia kuwagawa hao wanyama?

    Huu ni mbadala mzuri wa muafaka kwa barabara kupita nje ya hifadhi.

    ReplyDelete
  6. Ukisoma vizuri balozi hajasema kama watafadhili ila amesema kama wataombwa wataangalia uwezekano wa kusaidia barabara inayopitia kusini nje ya hifadhi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...