JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, imemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda Issa.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda maalum,Suleiman Kova, alisema kuwa Ponda amekamatwa kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya Serikali iliyoko madarakani.

 Makosa mengine ni uchochezi wa udini kati ya waislamu na wakristo na ndani ya waislamu wenyewe,kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini.

 Tuhuma nyingine ni kulazimisha watu kufanya maandamano hasa wanawake na watoto,kumtisha kumuua sheikh Mkuu Mufti Issa Shaaban bin Simba, kujisifia kuingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi bila ruhusa na uvamizi wa kiwanja.

 Tuhuma nyingine ni kuingilia uhuru wa Mahakama, umwagaji wa damu, uchomaji wa makanisa zaidi ya nane, uharibifu wa magari, wizi, upotevu wa vifaa vya makanisa. “Sheikh ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa Mahakamani waachiwe mara moja kabla ya siku saba”alisema.

 Ponda alikamatwa juzi majira ya saa 4:30 usiku akiwa kwenye pikipiki kuelekea katika maficho yake maeneo ya Temeke.

 “Juzi usiku sijalala kabisa kuhakikisha oparesheni ya kumkamata inakwenda salama, Ponda ni mjanja sana ila Serikali ina mkono mrefu kabla ajaingia katika maficho yake Temeke,alijaribu kukimbia ili atoroke lakini akakamatwa”alisema.

 Kova pia alisema kuwa mnamo Oktoba 12,mwaka huu Ponda aliwaongoza wafuasi wake na kuvamia kiwanja namba 311/2/4 block T chang’ombe mali ya kampuni ya Agritanza kwa madai ya kulikomboa.

 “Ponda akiwa na wafuasi wake walivamia kiwanja hicho cha agritanza na kudai kuwa wanakomboa mali za waislamu zilizouzwa na Bakwata,uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kiwanja hicho kina hati miliki namba 93773 iliyotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbalimbali ya kuuziana”alisema

 Aidha Kova alisema kuwa uongozi wa Bakwata ulipeleka mashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho na kusema kuwa watu waliovamia wanakabiliwa na shitaka la kuingia kwa jinai pamoja na uharibifu wa mali.

 “kati ya watu 38 tuliowakamta wanawake ni saba na wanaume ni 31 na tuliwakuta na silaha mbalimbali kama visu,mapanga,sururu na vifaa vya kuvunjia na vya ujenzi,jenereta na kujenga jengo la haraka”alisema Kova.

 Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa limemvumilia Ponda kwa muda mrefu na kuwataka watu wanaoandamana kinyume cha taratib kuacha. “Nawasifu sana wakristo ni wavumilivu,wanabusara kwa tukio la mbagala la kuchoma makanisa la sivyo hali ingekuwa ya hatari na hata hivyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu haijasajiliwa kisheria”alisema.

 Kova amewataka wafuasi wengine wajisalimishe kwani oparesheni inaendelea na watawachukulia hatua za kisheria. Pia amewaasa wananchi kutumia akili zao binafsi na kuacha kufuata mkumbo watashughulikiwa.Jeshi la Polisi linatarajia kumfikisha Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. jana vitu vingine vinachekesha kweli bila kuwambana watu wa aina hii mwisho wake ni umwagaji wa damu,ndiyo mama nyerere wakati mwingine alitumia nguvu ya dora alipewa ya kuwa amiri jeshi mkuu,kwani hata kuna msemo rais ni mungu wa pili wa dunia .huyo jamaa kaachwa kwa muda mrefu ,anahitaji kupata kichapo cha nguvu au kifungo cha muda mrefu,tumechoka na vituko kukisha udini,udini,huku umaskini unazidi ,yote hayo yanaletwa na serikali kutokuwa wakali kwani kama wakipata kichapo safi hutaona hayo,mbona nyerere alikuwa akihutubia tu kwenye redio huoni hata mtu wa kuguna?siku hizi raia watanzania wanadhumbutu hata kuteka kituo cha polisi du kweli tunakwenda kusiko,kazi kweli

    ReplyDelete
  2. Mmmh

    Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firaun

    Anayekwenda mafichoni anapanda pikipiki?

    ReplyDelete
  3. Mmmh

    Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firaun

    Anayekwenda mafichoni anapanda pikipiki?

    ReplyDelete
  4. nini maana ya neno ashikiriwa?

    ReplyDelete
  5. Kukimbilia mafichoni siyo lazima uchimbe shimo, ukikutana na Gaddafi ukamuulize ilikuwaje akaingia mtaroni?

    ReplyDelete
  6. Uncle Michuzi, wewe ni mtoto wa mjini na Kiswahili chako kimekubuhu, acha kutumia cheap labour ambayo hata lugha yetu ya Taifa haipandi,"Ashikiriwa" toka lini?

    ReplyDelete
  7. acheni kukamata watu. sasa hivi serekali ina makusudio mabaya na waislamu. leo zanziba wamemkamata Sheikh faridi na huyo mnamsingizia nini.?? mtu akisema mambo bayana basi anaikasifu serekali. HUU NI UONEVU WADHAHIRI NA na serekali ibadilishe strategy yake kwa islamu au KWANAMNA HII DAMU ITAMWAGIKAAA.

    ReplyDelete
  8. HUYU PONDA NI UMASKINI TU...MATATIZO YAKE YA KIMAISHA ANAYATAFUTIA SULUHU KWENYE UISLAM...SHULE HANA...AJIPAGE UPYA...AENDE SHULE AELIMIKE...!

    ReplyDelete
  9. M/Mungu msamehe kila anayekukosea na muongoze kila anayepotea..

    ReplyDelete
  10. Watu wengine mwana wewe unasema serikali inaagenda? Kweli hata kiwango chako cha kufikiri ni kidogo kabisa. Tena serikali imecheza na hawa wajinga for a long time. Naongea kama Muislam na Mtanzania. Usalama wa Taifa ulitakiwa kuwa umewashughulikia hawa watu long time ago.They have their mandate very clear tena hawaitaji ruksa ya Ikulu kuanza kukusanya information zao. Leo eti kova hakulala? Baada ya hali kua mbaya Zanzibar walitakiwa kuwa wamedha wadhibiti viongozi wakule na hawa kina mponda baada tu ya maandamano kwenda Home affairs wange malizana nao. Leo Makanisa, klesho nini? Huyo mtoto aliye kojolea msahafu alisha kamatwa...anatakiwa ahojiwe na kama alitumwa then walio mtuma wakamatwe wapelekwe mahakamani na wapewe adhabu kali ambayo itakua ni fundisho kwa nchi nzima. I don't care funga hata 30-40yrs bila msamaha hata kidogo. Religious tolerance ni muhimu sana katika nchi yetu. Ujinga huu hauruhusiwi.
    God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli ni wakati wa Serikali na taasisi zake kuamka. Kuna watu wanafanya vitendo vya uchochezi na uvunjwaji wa sheria bila uonga, tena kwa kutumia jina la dini, hii haikubaliki. Discipline lazima iwepo, na mtu ukiaminiwa na kupewa heshima basi uitumie kwa mambo mema siyo vinginevyo. Tanzania inaelekea kusiko, Serikali lazima idhibiti makundi ya fujo,wahuni, uchochezi, uvunjaji wa amani na uhalifu wa namna zote. Tufuate kweli maagizo ya mwenyezi Mungu, tuache maovu watanzania jamani! Wakristo na waislamu wote ni ndugu moja sisi, tusiruhusu watu wachache wakateka akili zetu, tutakaokuja kupata madhara ni sisi wenyewe, wale wanaotuchochea watajificha mbali.

    ReplyDelete
  12. cheza na waislam wewe nchi tumempa wenyewe nyerere kwa msaada wetu waislam ponda atatoka tu huyo kova hawawezi watoto wa mjini.

    ReplyDelete
  13. hivi kwani udini ni jinai? sheria ipi?

    mi naona umekuwepo tangu mkoloni mpaka leo. na unalindwa na wanaofaidika nao, hawataki udini uwe jinai kwani wote ni ukonga.

    ReplyDelete
  14. Kukimbilia mafichoni siyo lazima uchimbe shimo, ukikutana na Gaddafi ukamuulize ilikuwaje akaingia mtaroni?

    Ponda alikuwa anaenda MTARONI kwa kosa gani alilofanya mpaka aende mtaroni?

    ReplyDelete
  15. Yeyote atakayeleta uchokoraa kupitia mlango wa dini yeyote ile shurti aminywe kama vile unavyovunja chawa au akanyagwe barabara kama vile unavyo ua mende!!!

    ReplyDelete
  16. acheni kutetea ujinga. badala watu wafanye kazi wamekaa chini kupanga mikakati isiyo na tija wala faida kwao. acheni uvivu, chapeni kazi. Mngekua na kazi ya kufanya msingekua na muda wa kuandamana na kufanya vurugu zisizo na maana. afu mnaishia kusema wakristo wanapendelewa kumbe wenzenu wanachapa kazi na kusoma nyie mnaishia kukaa vijiweni kujadili swala la udini na upendeleo. amkeni sasa

    ReplyDelete
  17. mara nyingi kweli inauma...upendeleo upo nanyi wakiristo ndo mnapeana kazi kwa upendeleo tumeshajua kuwa mna idara za ajira makanisani...
    uchochezi kwa viongozi wa kiislamu tu? mara ngapi viongozi wa chadema wametoa kauli za uchochezi na uvunjifu wa amani mbona hawakukamatwa? maaskofu je walishasema nchi ikijiunga na oic damu itamwagika...acheni kuwa na sera za nyerere kuwa ukweli usisemwe, ukisemwa usisikike

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...