Gari linalosambaza magazeti ya kampuni ya Mwananchi Corporation katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, limepata ajali wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kusababisha vifo vya watu watatu hapo hapo na wengine watano kujeruhiwa, mmoja akiwa mahututi sana.


 Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Afande Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo Oktoba 26 majira ya saa 11 alfajiri katika eneo la Kirinjiko, wilayani Same, katika barabara kuu ya Tanga-Moshi.


 Kamanda Boaz alisema Gari hilo lenye namba za usajili T336 BFU Isuzu Pick-up linalosafirisha magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communication (MCL)  ililigonga gari lenye namba za usajili T 415 AAM/ T 411AAM Scania na  kusababisha vifo vya watu watatu papohapo.


 Kamanda Boaz amewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Mrutu (65)  mkazi wa wilayani Same, Abdalla Rajabu(49) mkazi wa Majengo Mkoani Arusha ambapo wote ni madereva wa Simba Truck pamoja na Robert Mnyeki (39).


 Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Rahim Bakari (28)mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, mfanyakazi wa kampuni ya Mwananchi,Juma Said (37)Dereva wa Simba Truck mkazi wa Arusha kwa Mrombo,Gasino Nguma(40) mwalimu mkazi wa Mlandizi jijini Dar es salaam, Hamza Omary (31) mfanyabiashara mkazi wa Buguruni jijini  Dar es salaam pamoja na Sekero Musa (30) ambaye hali yake inaelezewa kuwa mbaya.


 Watu hao walikuwa ni abiria katika gari lililokuwa likisafirisha magazeti ambapo Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya  Same na KCMC kwa ajili ya matibabu.

 Chanzo cha ajali hiyo kamanda alisema ni mwendo kasi wa gari dogo na kwamba dereva wa gari hilo Wambura Ramadhani anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi bado tuna safirisha magazeti kwa magari kwa umbali wote huo. Wakati sasa kuna technology ya kizichapisha hayo magazeti kwa kila mkoa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...