HALI IMEKUWA SI SHWARI MAENEO YA KATIKATI YA JIJI KARIBU KABISA NA KITUO CHA POLISI CHA KATI (CENTRAL POLICE) HIZI SASA BAADA YA LUNDO LA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WAISLAM WENYE IMAN KALI WALIOFIKA KWENYE KITUO HICHO CHA POLISI KUSHINIKIZA KUACHIWA HURU KWA KATIBU WA JUMUIYA NA TAASISI YA KIISLAM,SHEIKH ISSA PONDA AMBAYE ALIKAMATWA JANA MAJIRA YA SAA NNE USIKU.

ASKARI POLISI WAMETANDA KATIKA ENEO HILO HUKU WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WANAONEKANA KUKATAA KUONDOKA ENEO HILO MPAKA KIONGOZI WAO ATAKAPOACHIWA.

SHEIKH ISSA PONDA NI MMOJA KATI YA WATU 38 WANAOSHIKILIWA NA POLISI KUTOKANA NA TUHUMA MBALI MBALI ZIKIWEMO ZA UCHOCHEZI KWA SERIKALI IYOPO MADARAKANI NA KUCHOCHEA VURUGU ZA UDINI BAINA YA WAISLAM NA WAKRISTO IKIWEMO ILE ILIYOTOKEA HIVI KARIBUNI ENEO LA MBAGALA.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA ITAENDELEA KUTOA TAARIFA KADRI ZINAVYOENDELEA KUPATIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hilo ndilo bomu analosema Mzee Lowassa,ni ajira!watu wamekata tamaa na maisha na haki hawapati,huku nyuma napo BAKWATA haitakiwi bado watu wanalazimishwa waikubali....Ipo haja serikali kukaa na waislam hao kujadili kasoro mbalimbali ambazo zinatatulika.

    ReplyDelete
  2. Watu kama huyo inabidi Polisi wajifunze wame wanaenda kuwahifadhi/kuwafunga kituo kilicho mbali na makazi ya watu au sehemu ambayo waislamu hawawezi kukusanyika kirahisi. Kama huko mkoani (Utafutwe mkoa ambao si rahisi watu kukusanyika sana)

    POLISI JIFUNZENI KWA MAREKANI OSAMA ALIVYOKUFA WAMEMZIKA BAHARINI...kwa sababu WANGEMZIKA SEHEMU INAYOFIKIKA WAISLAMU WENYE MSIMAMO MKALI WANGEWEZA KUKUSANYIKA HAPO NA KUFANYA VURUGU AU KUANZISHA HATA MSIKITI.

    NI MUHIMU WATU WACHOCHOZI KUWAFUNGA MBALI NA MAKAZI YA WATU....KUONDOA HALI YA WATU KUTAKA KULETA VURUGU.

    ReplyDelete
  3. NI MUHIMU KWA WATU KAMA HAWA KUWA WANAFUNGWA/HIFADHIWA MBALI NA MAKAZI YA WATU ILI KUEPUKA ILE HALI YA WAISLAM WENYE KUANDAMANA KUSHINDWA KUANDAMANA KWA SABABU MTU WAO WANAOMTAKA YUKO MBALI NA SEHEMU WANAYOANDAMANA.

    POLISI IJIFUNZE KWA MAREKANI OSAMA ALIVYOKUFA, ALIZIKWA BAHARINI...KISAIKOLOJIA WAISLAM WENYE MSIMAMO MKALI HAWAWEZI KUKUSANYIKA BAHARINI/KUANDAMANA

    LAKINI ANGEZIKWA NCHI KAVU WANGEKUWA WANAKUSANYIKA NA KUFANYA MAANDAMANO AU HATA KUJENGA MSIKITI KARIBU NA ALIPOZIKWA NA HIYO SEHEMU INGEKUWA SEHEMU YA KUANZISHIA UGAIDI MBALIMBALI

    ReplyDelete
  4. Sasa tunaelekea wapi jamani? Huu utaratibu wa kulazimisha watu kuachiliwa umeanza lini? Naomba tufuate taratibu na kuheshimu Mamlaka zilizoko kwa ajili yako.....

    ReplyDelete


  5. Hayo ndo matunda ya elimu inayotolewa na CCM watu wangekua na kazi zao wala wasingepata muda wakwenda kuleta fujo yyote hayo yanatokana na kukosa kaz na pia kutokwenda shulee jamani

    ukweli ni kwamba shule muhimu sanaa watanzania tusomeee jamani tuache kukaa vijiweni kujadili maswala ya dini

    ReplyDelete
  6. naungana na na anony wa kwanza hapo juu...Serikali ikae chini na ijadiliane na waislam. na jinsi ya kuwapata viongozi wa BAKWATA watakao tetea haki za waislam na si viongozi abao ni vibaraka...agrrrrr!

    ReplyDelete
  7. Mara nyingi utakuta watu wanaokusanyika hivi na kujifanya wanatafuta haki ni wale wasiokuwa na ajira na cha kufanya. Siyo kuwa wana uchungu ila wakipata ka mwanya ka kukusanyika siku zinasogea. Wewe nenda ufuatilie kama utaona watu wenye kazi zao au biashara zao watakuwa hapo. Hao ni wale wazungu wanita ma hooligan..hawana cha kufanya, hawana pa kwenda kwa hiyo vurugu kama hizo ndo furaha yao. Acheni vyombo vya dola vifanye kazi yake na kama hawana hatia wataachiwa acheni kuiga mambo ya Middle East ati kwavile ninyi ni waislamu. Jifunzeni kuwa wastaarabu. Najua siyo waislam wote wanao-support upuuzi huu lakini hao wachache lazima tuwafundishe kutoiga upumbavu wa Syria, Libya, Tunisia na kwingine. Mdau, USA

    ReplyDelete
  8. si mara yakwanza kwa waislamu kukamatwa kwa uonevu huohuo tunaousema kila siku, kisa anatetea haki za waislamu anaonekana mchochezi.Inshaallah ataachiwa mda si mrefu (kabla ya ijumaa) na harakati zitaendelea mpaka kieleweke..

    ReplyDelete
  9. Ndugu zangu Watanzania sikilizeni wimbo huu;

    http://www.youtube.com/watch?v=z8nBz0fESwk

    ReplyDelete
  10. Uchochezi sio mzuri hata kidogo, huyo anapaswa kupambana na mkono wa sheria...mambo ya watoto wadogo yanafika je hadi kuchoma makanisa? Na kama tatizo lilikuwa ni Quaran, mbona wao wamechoma na kuharibu biblia? Kwan walishindwa kuwa wavumilivu sheria za nchi zichukue mkondo wake? Ponda and his fellows they must take responsibility on this!

    ReplyDelete
  11. MICHUZI usinibanie comment yangu ila kiukweli sidhani kama kuna kituo cha polisi kati bali kuna kituo kikuu cha polisi, kuna shida nyie watu wa habari kutafsiri maneno kama jinsi yalivyo, ikiwa central police inaitwa kituo cha polisi cha kati kwahiyo serikali kuu ambayo ni central government watakuja waandishi wengine

    ReplyDelete
  12. Mutabaruka IIOctober 17, 2012

    Wewe anony unayekuja na habari ileile "shule muhimu bana,,,eeeeee shule muhimu banaaaa na tena eeeh shule muhmu bana..."

    Shule ingekuwa inatusaidia kiasi hicho basi watu wasingekwenda Loliondo, kwa sababu loliondo ilijaa "wasomi".

    ReplyDelete
  13. mpaka kielewe masuala ya uonevu sasa yanakaribia mwisho,tumesubiri sana yametuchosha sasa mbele kwa mbele hadi kieleweke

    ReplyDelete
  14. sidhani kuwa kamatakamata ni suluhisho la mgogoro huu. Waziri asiye na Wizara Maalum Stephen Wassira kazi yake ni Uratibu hii ndiyo dhamana yake kuvikutanisha vikundi mbalimbali na kutafuta maridhiano bila kutumia nguvu, haya mambo mbona yanaongeleka!!!. Nguvu hazijengi, hali ikiwa hivi nadhani Ijumaa itakuwa balaa.

    ReplyDelete
  15. jamani watanzania hivi kweili tunajua thamani ya kuishi kwa amani ya kukuwezesha kufanya mambo yako bila hofu??sasa tunataka kwenda wapi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...