Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa, kutoka T.O.T akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Mitikisiko ya Pwani Dar Live Jumamosi.
MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika vilivyo katika Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Tamasha hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo Jahazi, Coastal, TOT na mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times Radio wakiongozwa na Gardner G Habash na Khadija Shaibu 'Dida' walinogesha tamasha hilo na kulifanya liwe la kipekee.
Kiongozi wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf 'Mfalme', akiimba na mashabiki wake.Kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi', akiwapa raha mashabiki.
Maua Tego wa Coastal Modern Taarab akiwa stejini.
Wasanii wa TOT wakizidi kunogesha tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...