Madame Rita Paulsen akimpoza Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2012 Walter Chilambo ambaye amehemewa kwa furaha baada ya kushinda mtanange huo usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es salaam.  
Mashabiki wakishangilia
Mshindi wa EBSS 2012 Walter Chilambo akikabidhiwa mkwanja wake wa shilingi milioni 50 cash hapo hapo jukwaani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. pandisha suruali hiyo!

    ReplyDelete
  2. Fainali za 2912 zimefanyika jana jamani? Au mimi nasoma vibaya maelezo yaliyo chini ya picha. Nina uhakika kwa mwaka huo hakuna aliye hai sasa atakayekuwa anaishi. Na wewe mdau wa kwanza kuchangia, haujui kuwa staa lazima avae hivyo?

    ReplyDelete
  3. Samahani lakini siyo 'kuhemewa' lakini ni 'kuemewa'.

    KUHEMEWA (source: hema) ni kama vile mtu akikukupumulia pumzi kifuani kwako.

    ReplyDelete
  4. sipendezewagi na hii tabia ya kumpa mshindi hela zote na hao wengine hata kifuta jasho jamani,aah haipendezi.

    ReplyDelete
  5. Usimwambie apandishe Suruali, kwasababu hiyo ni moja ya vitu vilivyo changia ushindi wake, huo mtindo wa uvaaji wa Suruali hapa Marekani tunauita Hipuhopu.
    Usijali, ninacho taka kusema ni kwamba kumkabidhii hizo hela zote hapo jukwaani ni kumuua na kesho mtamzika kama mimi nadanganya subirini,kwanini msimwekee bank?

    ReplyDelete
  6. Picha ya chini mwaka huo 2912 ni miaka 900 kutokea sasa mwaka 2012!

    2912-2012=900 !

    Nani atakuwa hai hata vitukuu vyake kama wooote hatutakuwa makaburini miaka mingi tu?

    ReplyDelete
  7. Hehehehehe!

    Mambo ya Mamlaka ya Bandari kilipia Cash madirishani yamezukia tena EBBS ?

    Kwa nini msiandae Hundi?

    Ni nje ya taratibu na kanuni za kifedha kwa kiasi hicho kulipwa kwa Fedha Taslimu (Cash) !!!

    ReplyDelete
  8. Ohooooo!,

    Tsh. Milioni 50 mkononi?

    Je, mlimpatia ulinzi?,hakunusurika kukabwa?, alifika kwao salama?

    Haya mambo ya kulipana Fedha Taslimu ktk kiasi kikubwa namna hii ni ya huko Minadani kwenye mauzo ya ng'ombe na mbuzi Itigi na sio Mijini!

    ReplyDelete
  9. Nafikiri Mshindi wa EBSS dogo Walter Chilambo atanunua suruali mpya na atajifunza kupandisha vizuri suruali akivaa kwa pesa aliyopewa Tsh. 50 Mil.

    ReplyDelete
  10. Kupewa hiyo pesa mkononi hakuna tatizo. Mbona Big Brother Africa mshindi upewa dola 100,000 mkononi? Dola 100,000 na mil 50 za kitanzania ipi pesa kubwa? Jamaa alikabidhiwa sanduku lake. Kisha akasafirishwa na mabaunsa waaminifu mpaka mahali anapojua kuwa ni salama. Kisha atajua mwenyewe kama aipeleke benki au aendelee kuimega hivyo hivyo. Kuhusu uvaaji mimi naona poa. Mlitaka avae kama anaenda kanisani au msikitini? Burudani ni pamoja na vituko kama hivyo. Big up Walter

    ReplyDelete
  11. naomba jina la mtangazaji wa kike.... kanikosha kwa sauti yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...