Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Maandanamo yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye basi aina ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa Wildaf wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula na Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu.
Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya aina mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na tatizo la Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi ya Vipengele Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya maumbile ya majeshi yetu wangeyapata wachezaji wa timu ya taifa tungekua tunatisha sana maana kila anayetia mguu ingekua kichapo tu kwenda mbele.

    ReplyDelete
  2. Kila siku naona wanawake tu?
    Wanaume nao wana kitu gani?
    Naomba jibu jamani mana wanaume naona wametengwa sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...