JAMANI HIVI WATANZANIA TUTAACHA LINI KUWA MATAPELI???HUYO DADA "MAGGIE R  MUNTHALI" AMEVAA MISS TANZANIA JE MNAMTAMBUA KWAMBA ALIKUWA MISS TANZANIA MWAKA GANI?AU ALISHIRIKI KATIKA MASHINDANO GANI YA KUMTAFUTA MWAKILISHI WA TANZANIA?SISI KAMA WATANZANIA TUMESIKITISHWA SANA NA KUTAPELIWA HUKU.
TUMESAHAU KUWA ULIMWENGU HUU WA MITANDAO UONGO UONEKANA MARA MOJA.DADA HUYU ALIONEKANA JUMAMOSI WASHINGTON DC KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS AFRICA USA.WASHIRIKI WOTE WALIOSHIRIKI NI WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI KATIKA NCHI ZAO WALIZOTOKA....AU WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI NDANI YA USA YA KUZIWAKILISHA NCHI ZAO.SASA HUYO DADA HAJAWAHI KUSHIRIKI MISS TANZANIA NA KUSHINDA KULE TANZANIA WALA HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA NDANI YA USA...JE IMEKUWAJE AMEVAA UMISS TANZANIA NAKUIWAKILIKSHA TANZANIA JE HASHIM LUNDENGA ANAELEWA SWALA HILI?..JE LUNDENGA ALIMRUHUSU HUYU DADA KUIWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI?..KAMA ALIMRUHUSU ALITUMIA VIGEZO GANI KUMCHAGUA?..TUNAPENDA KUWAKIRISHA NA TUNAMSAPOTI MTANZANIA YEYOTE ANAYETUWAKIRISHA NJE YA NCHI LAKINI APITIE KATIKA NJIA ZILIZO SAHIHI SIO KUGUSHI KUJIITA MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA KUTAFUTA MISS TANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI?...KAMA TUMEKOSEA ALIISHA WAHI BASI BWANA LUNDENGA TUNAOMBA PICHA ZAKE AKIWA KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA POPOTE PALE NDANI NA NJE....
NA TUNAOMBA UTWAMBIE JE ALISHINDA NA KUTWAA TAJI HILO?.....WAPO MAMISS WENGI AMBAO WANAFANYA KAZI KUBWA SANA KUWEZA KUFIKIA KUITWA MISS,WAMEVIJA JASHO KUPITIA VIKWAZO HADI KUSHINDA NA KUIWAKIRISHA NCHI VYEMA....TUNAOMBA MTU ANAPOAMUA KUIBEBA BENDERA YA NCHI ASIWE MTU WA KUFOJI.....HUU NI WIZI WA KUMUITA MTU MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUWA..TUNAOMBA PIA SWALA HILI MHESHIMIWA LUNDENGA KAMA SIO LA HALALI BASI LIFIKISHWE KWA WAANDALIZI WA MISS AFRICA USA KWANI INAWEZEKANA KABISA WAMERUBUNIWA..AU LABDA WANAVIGEZO VYAO.TUNAOMBA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI MSITUDANGANYE NA KUTUIBIA KWANI WATANZANIA SIKUIZI TUKO KWENYE MITANDAO....HABARI HIIZI PIA TUTAZIPELEKA WIZARA YA MABO YA NJE KWANI HUWEZI KUIWAKIRISHA NCHI PASIPO HALALI..!
AHSANTE.....MUNGU IBARIKI TANZANIA !

WADAU WASHINGTON

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. But mbona namuona kama anavigezo vinavyotakiwa?Wakati kujitolea katika kuiwakilisha nchi katika masuala halali,mie sioni tatizo.Maana inawezekana alitafutwa mshiriki kutoka TZ akakosekana na kisha mzalendo huyu akaona maadamu vigezo anavyo kulingana na masharti ya waandaji,aliwakilishe taifa.Kwa hiyo mie sioni tatizo madamu hajatuabisha wala kuvuja sheria za nchi.Big up mrembo!

    ReplyDelete
  2. Umelalamika utadhani ulinyimwa nafasi ya kushiriki. Aliyekuambia ma miss wote lazima wapite kwa Lundenga ni nani? Umetapeliwa nini sasa? Aghaaaaa!

    ReplyDelete
  3. Swala ni mnyama. Suala ni "issue" au jambo au mada inayozungumziwa.
    Kuwakilisha na si Kuwakirisha.
    Watanzania tukienzi Kiswahili chetu kwa kukijua.

    ReplyDelete
  4. Hata wewe inaonekana sio Mtanzania, rekebisha kiswahili chako kutuwaki"RI"sha , kutuwakilisha, yaani siku hizi kiswahili imekuwa mzigo kwa taifa hili kwenye L watu wanatwanga R na kwenye R wanatwanga L sehemu ya kuweka a mtu anaweka H kama endeleza mtu ataandiha HENDELEZA .

    ReplyDelete
  5. Du hii KALI, Sikutarajia ila sasa nimeamini WIZI upo wa namna nyingi. Anko Lundenga shughulikia hio maana linaweza kutuletea sifa mbaya. Ila kikulacho ki nguoni mwako, kwa sehemu naamini waliofanya hivyo ni WATANZANIA WENZETU!

    ReplyDelete
  6. Binti mzuri amependeza kwa sana tu, kama yeye ni mtanzania hiyo tosha sana, we mdau unachuki binafsi au roho ya korosho, get used to it mate.

    ReplyDelete
  7. Kwanza umekosea kumuita Lundenga mheshimiwa .ki-ufupi Lundenga hana hadhi ya kuitwa mheshimiwa. ukimuita Lundenga mheshimiwa na mimi utaniita nani?.

    ReplyDelete
  8. Mimi sioni tatizo, inawezekana waandaaji walimuomba ashiriki baada ya kukosa mtu kutoka Tanzania maana watanzania wengi huku nje wanapenda kujiweka nyuma nyuma. Sasa kaka huyu dada ni mtanzania basi ana kila haki ya kutuwakilisha kwani huyo Lundenga ni nani mpaka awe ndio pekee mwenye kuruhusu watu kushiriki mashindano ya kuwasilisha nchi yao wakiwa nje ya nchi.
    Mwandishi unaelekea una chuki binafsi. Watanzania tupendane jamani. By the way mwakilishi wetu umependeza sana tena una kila kigezo.

    ReplyDelete
  9. who ces? kwani hao wote wanaowakilisha huwa wanachaguliwa na watanzania wote? si wanakuwa wanachuguliwa na watu wachache wenye akili finyu na wasio na la kufanya kama wewe?

    Eti tumetapeliwa? umetapeliwa nini hasa hapa? grow up and move on.

    ReplyDelete
  10. Wewe mleta mada ni mnafiki, kwani hayo mashindano umeambiwa ni ya kumtafuta miss world ? Mashindano kama hayo yanafanywa sana nje, ni sehemu tu ya burudani na si lazima mshiriki awe aliyeapata taji tanzania na wala Lundenga hausiki na wala hana uwezo wa kufanya chochote. America na ulaya mashindano haya yapo sana, mataifa mbalimbali huingia kwenye mashindano kama football na hayo ya umiss. mfano sweden kuna timu inayoiwalisha tz kwenye mashindano ya kimataifa ( The Kilimanjaro ) lakini hakuna mchezaji wake yoyote yule aliyecheze ligi ya tz wa taifa stars, lakini kwenye mshindano kwa mujibu wa sheria za sweden inatambulika. So acha watu washiriki na wachukue vikombe, sifa itakuwa ni Tanzania.

    ReplyDelete
  11. huu ndio tunhita ulimbukeni...yani mi nikijiamulia kushiriki u miss majuu kwa ticketi ya Tz ni lazima nipate kibali cha Lundenga????????????? who is he by the way?

    ReplyDelete
  12. Ukiwa kama Raiya wa Nchi yako unauwezo wa kuiwakilisha Tanzania Popote pale.Mdau umelalamika huna mpango hata kidogo,wacha wivu.Mtz yoyote ana haki ya kuipeperusha bendera ya Nchi yake popote pale Duniani.Tuitangaze TZ yetu.Asingeshiriki Mtz then ungesikia oooh hata hakuna Mtz aliye kuwepo,tunashindwa na Wakenya leo Mtz kajitolea tunaanza majungu.Usi lalame kisa ni Washington DC yamefanyika.Watu tunaiwakilisha Tz popote hata Vichochoroni pande zote za Dunia.No wonder Tz haijulikani kwa mpango huu wa majungulization

    ReplyDelete
  13. Jamani Watanzania mbona tunapenda kujirudisha nyuma, yaani mtoto wa watu kajitolewa ili jina la nchi yetu angalao lionekanike kwa hilo, lakini mnachonga sana. Sasa mlitaka nchi yetu isiwakilishwe? Hivi kwa nini tunapenda kuwa na negativity nyingi kwa kila jambo linalofanywa hasa kuhusu nchi yetu? Tubadilikeni na kumuenzi yeyote Mtanzania ambaye anataka kuiwakilisha nchi yetu kwa namna mmoja au nyingine.

    ReplyDelete
  14. VUTA PUMZI WEWE MUANDIKAJI, KWANI UNAVYOMUONA HAFAI, AU MPAKA MKATOE DENDA NDIO MPATE UPENDELEO NYIE.

    ReplyDelete
  15. Hapo ndio mtambue Bongo Tambarale!

    ReplyDelete
  16. KATIKA BUSATI LA UREMBO:

    Makalio,Kope za macho,Kucha na midomo inaghushiwa na wa China,,,itakuwa kitu rahisi kama kumsukuma Mlevi ''UWAKILISHI KWENYE MASHINDANO'' ???

    ReplyDelete

  17. Hakuna cha wizi wala nini

    MBONA UNAIFANYA LIKE IT IS TREASON???

    SIYO KILA MTU ANAMJUA LUNDENGA HUKO NJE KAKA, BESIDES, KAMA MMOJA ALIVYOSEMA, KUTOKANA NA UKIRITIMBA WETU, MPAKA APPROVAL YA LUNDENGA OR WHOEVER IPATIKANE INGEKUWA NEXT YEAR!!! ANGEAMBIWA ARUDI HUKU KUJA KUJAZA FOMU, KIBALI GANI SIJUI, KULIPA USHURU GANI SIJIU, NA VINGINE KIBAO!

    KWELI 'KATUWAKILISHA' MAANA SHE HAS GOOD LOOKS AT LEAST, SHE REALLY LOOKS TANZANIAN.

    YOU ARE JUST MAKING A MOUNTAIN OUT OF A MOLEHILL.

    UMECHUKIA KUWAKIRISHWA?!

    ReplyDelete
  18. Mtu yoyote anaweza kuwakilisha taifa ktk ishu kama hizo, hata kama ni wewe ungeweza kuwakilisha basi wabongo wote tungekuunga mkono kwa moyo moja, acha majungu wangu, mi naona huyo dada ana vigezo tosha .....

    ReplyDelete
  19. Kwangu mimi sioni tatizo kwa watu kuwakilisha kama Miss Tanzania au Mr. Tanzania katika matukio mbalimbali. hili ni jambo ambalo linatokea katika maeneo mbalimbali kulingana na hafla zinazotayarishwa...Kama hili linawakera watanzania, ni vipi basi watanzania wangepaswa kukerwa na tatizo la wasio watanzania wa kuzaliwa wala wa kuishi Tanzania lakini wana passport za Tanzania? Kinachoniacha hoi ni pale ninapoitwa na Polisi wa nchi hii kwenda kumtafsiria mtanzania aliyekamatwa na hatia fulani...nikifika pale namsalimia habari yako kaka? ananijibu kwa kimombo...I don undestran' ooo brothor help me oooo....Duh! Naishiwa nguvu. Passport ya Tanzania, lugha haipandi..unafanya nini hapa Nawakilisha Tanzania kwa uovu...HIyo imekaaje wadau? Anayewakilisha Tanzania kwa u miss na kwa tabia njema..mwacheni jamani anatutangaza vema...vita yetu iwe kwa maadui wa ndani wanaoiuza nchi bila kujua madhara ya miaka 50 ijayo....

    ReplyDelete
  20. roho mbaya tu, sasa wewe inakuhusu nini? Hao ma-miss wa Ludenga wameshindikana tunasoma kila siku habari zao ktk magazeti. Kama ana vigezo na ametoka Tanzania sioni tatizo la kujiita miss Tanzania.

    ReplyDelete
  21. Huyu mdau aliyetoa malalamiko page nzima kweli yuko Washington? Mbona anaonekana mshamba wa ajabu! Hata hapa ninapoishi tuko Miss Africa. Mashindano yanashirikisha waafrika wanaoishi hapa. Mimi huwa naenda tu siku ya fainali, lakini sijui kabisa jinsi mshiriki anayewakilisha nchi husika anavyopatikana.

    Lakini washiriki wote ni washikaji wa mitaani tu, hawajawahi kushiriki hata mashindano ya vitongoji kwa kule Tanzania.

    Lakini siku ya fainali mtu anatinga mkanda uliochapwa MISS TANZANIA.

    Kwa hiyi acha ushamba. Usifikiri kuwa kuitwa Miss Tanzania, lazima uwe umevaa Taji la Lundenga!!

    Samahani kama nitakuwa nimekuudhi. Lakini mimi sijakutukana wewe bali nimetukana ujinga wako.

    ReplyDelete
  22. Mi naona huyu alieandika hapa ana chuki, gubu au wivu fulani, au ndo wale ambao walishindwa ktk mashindano. Mimi sioni tatizo, yaani ulitegemema nchi km marekani kuwa na watanzania ambao wameshawahi kuwa Mamiss jamani huo si upumbavu wako wewe dada/kaka, hata km wapo je kama wameshazeeka au hawataki!. Wewe mwenyewe tuambie ni nani huko US angeingia hayo mashindano km unae tutajie jina. Kati ya mamiss walioshinda Ms Tz ni yupi yupo US tutajie basi. Wacha wivu na uongo, wewe unatakiwa kusupport WaTZ wenzako na sio majungu yasio na mana, badala ya kuandika vitu vya maendeleo unaandika mambo ya chuki na kizushi au hauna kazi. Ungetakiwa kushukuru kwamba angalau WaTZ tumepata muwakilishi mana mara nyingi tunaachwa nyuma kuwakilishwa. Hao waliondaa shoo wangetakiwa kufuatilia wenyewe kwamba hao watu wanaoshiriki kweli walikuwa mamiss, na ninajua sio wajinga kiasi hiko cha kufikiri US kutakuwa na MTZ ambae ashakuwa miss, loh WATZ kweli hatupendani.

    ReplyDelete
  23. Hivi Lundenga ana hati hadi ya jina Miss Tz? hana mamlaka hiyo na kuvaa huo mkanda hakuna wa kumshutumu au kumdhihaki! sasa sijui jamaa analalamika nini!

    ReplyDelete
  24. Inaelekea alieandika habari hizi ana wingi wa hasira, chuki, na jazba. Huyu mwanadada anavyoonekana pichani ni mrembo wa sifa zote tena katika ngazi za kimataifa. Kama Tanzania haikupeleka mtu bila ya shaka kulikuwa na sababu, labda ni kwa ajili ya kiuchumi au labda imeona kuwa kwa sasa hakuna mrembo anaeonekana kuwa competative enough. Sasa ninachouliza ni kwamba kuna ubaya gani kama yupo mtanzania mwingine ambae pia ni mrembo kuliko nyinyi, kutuwakilisha? Acheni roho zenu mbaya.

    ReplyDelete
  25. Sio kila Miss Tanzania lazima apitie kwa Lundenga, kwanza Wabongo wengi wanalalamika kwa kusema Mamiss wanachaguliwa kwa upendeleo na hiyo kamati ya Miss Tanzania au kampuni. Na kama mashindano yalifanyika DC. basi lazima walikuwa navigezo vyao, siyo lazima awe Miss yule mliyemchagua na Lundenga. na vigezo vya umiss Tanzania ni nini? Si Miss aliyetoka Tanzania?!! Na mie naona huyo Dada Maggie ni mrembo kweli, na ninaona sifa kumwita Miss Tanzania kuliko hata warembo tuliona Bongo ambao wanalazimishwa kukaa uchi kushinda huo Umiss. Halafu kusema ukweli kama unavyoona maoni yangu mie napinga mambo ya Umiss, dada zetu wangekuwa wanapimwa kupitia mashindano ya mashule (masomo).Ingesaidia Taifa na wanawake katika kujiinua kimaendeleo. Kwa sasa wote hawa Mamiss, wanaonekana kama wanauza urembo tu. (kama jamaa wa bongo wanavyosema, 'eti ni chakula ya wazee').

    ReplyDelete
  26. Jamaa aliyeandika hii habari inaonekana labda alikataliwa katika haya mashindano, alichemsha kwenye mashindano,au hana kazi ya kufanya. Je kwa hiyo kila miji ya Marekani wanapofanya mashindao yao ya kiafrica inabidi waombe ruhusa kwenye mataifa yote ya Kiafrica? Na unasema unaiibiwa na Watanzania walioko nj'e kivipi? kwani wewe ni MTanzania zaidi kuliko walioko nje'? Kama unasema unaona kwenye mtandao jinsi unavyoibiwa, mbona mafisadi wapo hapa hapa Bongo na wanakomba mali yote ya TZ hupigii kelele kama hizi? Na siyo kwa vile unaona kwenye mtandao ni kweli. Akili ni nywele kweli.........

    ReplyDelete
  27. Hata hapa Belgium ipo kumtafuta Miss East Africa Belgium sijui kama kweli wale wote walishawahi kuchukua mataji ya Ki miss huko Tanzania walivaa kama hivyo alivyo vaa huyo dada sijui hawa waandaaji inakuwa vipi sio swala la hashim hili watu wanajifanyia kupata pesa kwa maslahi yao binafsi sio kwa heshima ya Tanzania Upo Boss wangu

    ReplyDelete
  28. WADAU WA UREMBO WASHINGTON DC USA...

    Salamu kutoka jijini Dar Es Salaam,

    Tumesoma maoni yenu kupitia mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.

    Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.

    Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA kwa mwaka huo.

    Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.

    Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.

    Kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano mengine yoyote ya urembo mahali popote pale.

    Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.

    Hatujui ni vigezo gani walivyotumia hao waandaaji wa shindano hilo la Miss Africa USA, hadi kumpa Jina / sash ya Miss Tanzania, lakini tunaimani tu kwamba ni mrembo anayewakilisha Tanzania japokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa.

    HIDAN .O. RICCO.
    PUBLIC RELATION OFFICER
    MISS TANZANIA COMMITTEE

    ReplyDelete
  29. Jamani wanaposema Miss Tanzania haina maana lazima awe muwakilishi kutoka kwa Lundenga ni Miss kutoka Tanzania ikiwa na maana ni Mtanzania anayeiwakilisha Tanzania. Sidhani kama hao washiriki wote wanatokea moja kwa moja nchini mwao kwa hiyo mlalamikaji hebu angalia kwa kina unacholalamika na kama ulikuwa kwenye kamati ya maandalizi sidhani kama ingekuwa vibaya kumshirikisha Lundenga alete muwakilishi kutoka Miss Tanzania yake. Hebu angalia hili jambo katika upeo mpana zaidi kishuleshule

    ReplyDelete
  30. Kwani amewaomba pesa? Inategemea kuwa ilikuwa event gani. Usidhani Miss. Tanzania lazima ateuliwe toka Tanzania. Kama watu wa Diaspora wana event na nchi nyingine na wameweka mojawapo ya events kuwa kutafuta mrembo toka kila nchi bado wanaweza kutafuta miss. Tanzania wao. Wewe uliyetoa hii article ni mtu mwenye wivu mbaya sana. Kwanza huyo dada ni mzuri sana. Ana sifa zote za kuwa Miss. Tanzania wewe unalalamika nini?
    Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  31. Jamani matangazo yalitolewa kwa waafrica wanaoishi hapa U.S.A. kujitokeza kugombania hii nafasi. Walituma profile zao na wanayotayarisha haya maonyesho nadhani ni dada kutoka Cameroon ( mawinny saidia kumwomba aandike article kwa kiingereza on how they select contestants). Haya ni majungu ya DMV as usual! Watanzania hawataki kujitokeza kwenye jambo lolote na ukijitokeza kashfa zinaanza! Nchi nyingine nyingi walikuwa na washindani 3 au wawili na walichujwa usiku huo na kubaki mmoja. Tanzania tulikuwa na huyu tuu so alipita bila kupingwa. Mwenye interest mwakani wasiliana na wanaotayarisha na wewe ugombee mwacheni mzalendo aliyetuwakilisha ipasavyo othersiwe ingekuwa aibu kuwa Tanzania hatukuwa na muwakilishi. My dear tupo wengi tumefurahishwa na uzalendo wako endelea tuu na tutakusupport. HAPA SI BONGO AMEFATA TARATIBU ZA WANAOTAYARISHA MASHINDANO HAYO HAPA USA, KAMA ANGETAKIWA KUPITIA KWA LUNDENGA ANGEAMBIWA. TUACHE KASHFA NOBODY IS TAPELI.Hii ndiyo website yao. I hope this will put this issue to an end. DMV ACHENI GOSSIP LET US SUPPORT THIS GIRL.

    http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/
    ELIGIBILITY

    1.Applicant must have at least one parent from an African country.
    2.An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.
    3.Applicants must be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.
    4.Applicants above 29 years of age will not be accepted
    5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.
    6.Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.
    7.No Pageant Experience is required.
    8.Applicants must be female at birth and never married.

    ReplyDelete
  32. Your uncle Ludenga has no jurisdiction in the U.S. and Maggie has neither violates any law or commits any crime. Organizers would not let her participates if she did not qualify.

    ReplyDelete
  33. NAONA HAPA KAMA MUANDISHI UNA BIFU LAKO BINAFSI NA HUYU DADA...MIE NINAVYOJUA MASHINDANO KAMA HAYA YAPO NCHI NYINGI ZA ULAYA NA DUNIANI KOTE AMBAKO KUNA MCHANGANYIKO WA WATU TOFAUTI,MFANO MISS UNIVERSITY xxxxxx, NA HATA INAWEZEKANA MISS NCHI FLANI, LAKINI KILA MTU ANAWAKILISHA TAIFA LAKE, SO HUU SI WIZI ILA NI KUTANGAZA TAIFA LAKE.

    ReplyDelete
  34. Nilipoingia kwenye haya maoni kulikua na maoni matatu, lakini ilikuwa saa 12 za asubui kwa mida ya sehemu fulani Ughaibuni, jamaa ndio walikuwa wanaamka aamka. Kufika saa sita mchana maoni 33., Wee!!! chezea wabongo ughaibuni. Na asilimia 98 wanatoa dozi kwa mleta habari. Ingawa kuna maswali kibao, sijaona yeye kurudi kujibu ata moja. Inaonyesha amesoma maoni, ameona bora akae kimya. Liwe fundisho kwa watu wengine ambao wanataka kuleta mfarakano kati ya WaTanzania wa Ughaibuni na waliopo bongo, sie wote ni ndugu. Kwa vile Mtanzania mmoja yuko huku au kule duniani siyo kusema hana uchungu na Taifa letu. Na kila mtu yuko sehemu kwa sababu mbali mbali, siyo kama hana uzalendo.

    ReplyDelete
  35. Binaadamu, kwani mtoa mada wewe uliji register kwenye hilo shindano ukakataliwa? hebu tuache viroho vya kwa nini. Amekwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania yetu. jamani hebu mwacheni mwana wa mwenzanu. Ka!!!

    ReplyDelete
  36. na kwa nini wadau Washington? kwa nini usijiweke wewe binafsi, kwani Wa-DC walikutuma? acha ufitini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...