Na Father Kidevu Blog,
KAMATI ya Miss Tanzania imesema
kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano
hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badala yake kufanya hivyo anatumia uzalendo
wake kuitangaza nchi Kimataifa.
Ufafanuzi huo umekuja kufuatia
malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania waishio
katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhalali wa Mrembo Maggie Munthali
kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika USA 2012.
Akizungumza na Blogu hii Msemaji
wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss Tanzania
haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo, kwani
shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.
Awali akitoa historia ya
Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali
kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya
kanda.
Tumesoma maoni yenu kupitia
mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki
shindano la urembo la Miss Africa USA.
“Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania
Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.
Pia aliendelea kwa kusema kuwa
Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo
hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA
ILALA kwa mwaka huo.
Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka
huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.
Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na
LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa
taji la MISS WORLD AFRICA 2005.
Ricco amesema Kamati ya Miss Tanzania
haijui ni vigezo vipi vinatumika katika shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina
Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni mrembo anayewakilisha Tanzania
japokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa.
Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza
jina la Tanzania katika fani ya urembo.
Father
Kidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano
hilo na kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi
ya nchi walikuwa zaidi ya mmoja kama vile Kenya.
Pia baadhi
yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani washiriki
wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na
vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika
nchi husika kwaajili ya kushiriki Miss World.
Haya ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo
katika mtandao huu http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/
ELIGIBILITY
1.Applicant must
have at least one parent from an African country.
2. An applicant
with parents from two countries will choose to represent only one country of
her choice.
3. Applicants must
be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to
compete in.
4.Applicants above
29 years of age will not be accepted
5.We accept
Applications from students, professionals and girls wishing to develop
themselves and improve their status.
6. Applicants are
strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to
uplift the community in need.
7. No Pageant
Experience is required.
8. Applicants must
be female at birth and never married.
go Maggie..
ReplyDelete
ReplyDeleteSASA YULE "MDAU WA WASHINGTON" ALIKUWA ANAKURUPUKA KUTOKA USINGIZINI AU NDIO WALE WA RUSHWA ZA NGONO?
MAANA KAPOST BILA KUFANYA KAUCHUNGUDHI ONA SASA KARUKA STIM
safi sana,yule bin adamu alikua anasambaza fitina akafie mbele
ReplyDeleteAPPLICANT MUST NEVER MARRIED??
ReplyDeleteMdau mtoa mada naomba urekebishe kuwa ni mtu mmoja tu aliyeuliza uhala wa huyo dada kishiriki. Tatizo limeonekana kuwa ni ukosefu wa elimu. Wasomi wengi wanaelewa kuwa kabla hujaandika, lazima ufanye research na kuelewa nini unakiandika.Nafikiri tumsamehe mtanzania mwenzetu na tumshauri aende shule. Natumaini ataupokea ushauri huu with positive attitude.
ReplyDeleteAlafu kapost hajui sheria na tarartibu za shindano. Maggie kakiuka nini pale? Au wivu?
ReplyDelete
ReplyDeletehivi hata sisi watanzania tuliopo ughaibuni tunakua na wivu wa ajabu hvyo?? this is insane yaani wewe bala ya kumpigia kura ashinde unaleta umasikini wako humu ndani?? au ulitaka kwenda wewe??
kweli wanao check eligibility ya nchi kua 3rd world walikosea Tanzania ilitakiwa kua 4th world country kabisaa coz naona hakili haziko sawa kabisaa am totally dissaopited with the person siamini kama anaishi huku huyo?
Bado unamawazo ya 5th world wewe hata sio 4th world pumbavu kabisaa this is bad totally bad
Go Magie tena nakuombea ushinde kabisaa
Duh!Nimesoma maelezo ya pande mbili kwa umakini sana,nimeelewa sasa.Yule wa post ya kwanza siyo kwamba anampinga huyu dada kuwakilisha Tanzania.Yeye,anapinga kujiita `Miss` Tanzania(Matumizi ya neno Miss-kama nilimwelewa vizuri).Kwenye huo mkanda angeweza kuandika tu TANZANIA (kwa maana kwamba ni mshiriki kutoka Tanzania).BTW,alishinda hilo shindano?
ReplyDeleteDavid V
Ivi jamani Hebu muacheni hiyo binti apumue mbona mnamuandama hivyo.....ivi hao mnaowaita mamiss Tanzania mbona wana mambo makubwa wanafanya Julio hiyo binti.. Washirikina wengine wanatembea na dawa za kuweka midomoni ili wakiongea wakubalike au Sababu hatuwasemi...na kutwa mnawasifia..hivi lini mating a nacho nyingine za Africa Kuwa supportive yaani wengi ni wivu na inajionyesha wazi...she is beautiful,hard work na anajaribu kuwakilisha nchi please muacheni Je akishinda mtafanyaje?!tuweni na upends na tusche majungu ili tulete maendeleo nchini..mnataka nyinyi tu kwanini. Muacheni ni mtu kwenye upends,mtulivu....waandikeni hao watoto wenu kila kukicha kurudi nchini kurenew macaws...mkitiuzi tutawataja mamiss wenu washirikina
ReplyDeleteDavid V i'm with you! hoja ya majibu imeshindwa kueleza kama ni sawa kwa miss anayeshindana kuvaa mkanda wa/ulioandikwa MISS TANZANIA hata kabla ya kuwahi/kushinda taji hilo.
ReplyDelete
ReplyDeleteKAKA DAVID V, HIVI UNAELEWA MAANA YA MISS? BILA SHAKA UNAELEWA.
HIYO NDIYO TITLE YAKE KAKA. ADULT WOMAN, NOT MARRIED.
TITLE HAITUMIKI KWENYE MASHINDANO YA UMISI TUU, THE TITLE IS USED EVERYWHERE.
KAZINI, HOSPITAL, CHUONI, KUJAZA FORM...THE LIST GOES ON!!! IT IS JUST A TITLE, SIO TITLE YA KWENYE BEAUTY PAGEANTS TU! YAANA HUJUI?
KAZI IPO.
ReplyDeleteAnon wa TUE DEC 4th 01:54:00AM
Marekani mwanaume ndio anaolewa, mwanamke ndio anayeoa. Bila shaka hiyo eligibility imetokea Marekani.
In US the woman marries a man. Kama umeshawahi kusikia mwanaume asking a woman, "will you marry me"?
"APPLICANT MUST NEVER MARRIED" yaani,
LAZIMA AWE HAJAWAHI KUOA.
Huyo aliyelalamika ktk post ya mwanzo atakuwa ANABEBA MABOSKI tu. Anajua kula mikate na ugali tu ili apate nguvu ya kubeba MABOKSI. LAkini kichwani ni MTUPI.
ReplyDeleteSwali la kizushi: Je, na hao wengine waliondika MISS (ikifuatiwa na jina la nchi), walishinda taji la UMISS katika nchi zao? Mdau unataka aweke kitambaa kilichoandikwa Tanzania; duu! kwani huyo dada ndiyo nchi ya Tanzania. Well done Miss Tanzania for representing us. Nyie wengine mwendelee KUBEBA MABOKSI mpaka MABEGA yaende upande
ReplyDeleteOhhh Maggie Munthali hastahili!
ReplyDeleteWatanzania Majuu wenyewe kwa wenyewe mnabaniana sasa je kweli mtaweza kuijenga Tanzania?
DAVID V, DAVID V, DAVID V, Wacha hizo. Labda ujasoma vizuri, soma tena(rudi nyuma usome maoni ya posti ya awali, maana hii ya pili). Nilishasema nyie ndiyo mnachochea ugomvi kati ya WaTanzania wa Ughaibuni na nyumbani. Nilishasema unachuki binafsi. Angalia unavyodanganya, umesoma maoni pande mbili zipi? Hapa maoni ni pande moja tu, asilimia 98 yanasema jamaa amekosea(hata hizo Miss kamati zote 2 zimejibu) na bila hata hivyo unaona kabisa jamaa ameongea madudu. Labda ni wewe ulieandika, ulikuwa unapima? Umeona sasa, usirudie kuandika madudu. Siye wote ni ndugu. Na jamaa walioko Ughaibuni wana uchungu sana na Taifa lao. Wapo wengi wanafanya mambo mengi kusaidia ndugu na Taifa, lakini hatujitangazi tu kwani siyo tabia yetu sisi wabongo.
ReplyDeleteJAMANI KUWA MISS TANZANIA C O MPAKA USHIRIKI UKIWA TZ KAVAA TAJI HILO KUWAKILISHA VYEMA UTAMBOLISHO WAKE HAWAKUTAKA JINA KWANI NI MISS AFRIKA USA SO KINACHOTAKIWA NI JINA LA NCHI KWA HIYO WEWE MVUTA MADUDE TULIZA WENGE KWA MAMBO YA MAENDELEO YA WENZIO WANAOJUA KWANINI WAKO HAPO DC mdau stockholm sweden
ReplyDeleteAnon wa Tue Dec 04, 01:54:00 AM 2012
ReplyDeletena
Anon wa TUE DEC 4th 01:54:00AM
Kweli lugha gongana. Na kama ni ujanja (kejeli)wa kujifanya mnajua zaidi, naona mmepotea na hapa mnaonyesha aibu jinsi msivyoelewa lugha, lakni mnajiona Poa. Mungu awasadie mpate hekima ya kuelewa. Na kama kweli hamuelewi lugha, samahani, basi ulizia kwa watu wanaojua.