Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. raisi mstaafu alivosimama katikati ya wenzake inanikumbusha kuleee kama anaimbwa"KASIMAMA PEEEEKE YAKE , ANAONYESHA UTUNDU WAKE"

    ReplyDelete
  2. Warioba ana mwili mzuri sana,kila ninapojaribu kuwaangalia viongozi wetu wawe wastaafu au wale waliobaki serikalini wakitumikia jinsi wanavyoitukuza miili mikubwa sijui hawana washauri wa afya maana ni hatari mno jamani.

    ReplyDelete
  3. hivi mwisho wa kutoa maoni ni lini? kila siku maoni maoni, wapi vitendo?

    ReplyDelete
  4. tuwe wakweli jamani,hawa viongozi wote wastaafu watapenda kuona Katiba Mpya "itakayo walinda wao" katika maisha yao yaliobakia hapa duniani!kuwauliza kuhusu michango na mawazo yao,ni kuwapa "mzigo usiobebeka!".what should we expect from these retirees,to be honest?

    ReplyDelete
  5. ningekuwa na mwili kama wa waryoba sawa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...