Katika pitapita zake kamera ya Globu ya Jamii ilifika mahali hapa katikati ya jiji la Dar es salaam na kukuta mambo mswano. Yaani barabara imetengenezwa na kugeuza kabisa sura ya sehemu hii kwa kusakafiwa concrete slabs (sijui kimatumbi inaitwaje - msaada tutani plizzz) badala ya lami kama ilivyozoeleka. Je, mdau ni mtaa gani huu??


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Hapo ni nyumbani kwetu...nyuma na benki ya nanihii....karibu kabisa na ninapo pata lunch kila siku....ukija utapaona vizuri....naenda pata msosi sasa hivi...ulevi mbaya...ukilewa unsmwaga utumbo mtupu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inamaa huyo mdau wa kwanza ni homeless coz hapo ni barabara inakuwaje kwenu?????

      Delete
  2. Hapa ni Morogoro Road kama unaelekea kipande cha kutokea Stand ya Mabasi ya zamani Kisutu kuelekea Samora Avenue.

    ReplyDelete
  3. Morogoro road

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo kinachokushangaza ni nini? Barabara kujengwa kwa concrete badala ya lami mbona ni kitu cha kawaida sana. Technology hiyo ipo sehemu nyingi tu duniani. Google imeshamaliza ubishi, we ingia tu kwa raha zako utajionea mwenyewe.

    ReplyDelete
  5. Huu ni barabara ya morogoro rd, karibu na mtaa wa samora st

    ReplyDelete
  6. Daaa jina limenitoka ila upo karibu zaidi na mnara wa saa,kule posta ni karibu zaidi na wanapouza vitenge na kanga kwa wingi.Ukipandisha juu unakutana na bibititi road.Nakumbuka kipindi cha nyuma ulishatuwekea hapa picha ya mtaa huu ukiwa na barabara yenye mashimo.

    ReplyDelete
  7. Hiyo ni barabara ya Morogoro ikitokea.

    ReplyDelete
  8. mitaa ya k-koo hii.nahisi mtaa utakua ushauzwa kwa wageni huu.fatilia mzee wa libe utapata ukweli

    ReplyDelete
  9. Mdau wa pili amepatia pasipo na shaka bali wa kwanza mh!

    ReplyDelete
  10. kitumbini

    ReplyDelete
  11. Fuatilieni huyu mdau anayehisi mtaa umeuzwa anaweza kuwa sawa, maana inaelekea mwezekaji ana nguvu sana maana sioni gari, omba omba wala machinga sehemu hiyo

    ReplyDelete
  12. Hapo ni nje ya Dar Es Salaam, Mkoa wa Morogoro Wami Ukutu na Ubena Zomozi ndio zege inatandikwa na Lami inang'olewa.

    Sasa ukiingia Dar Es Salaam ndio balaa mafao kutoka Miradi ya GESI NA MAFUTA YAMEANZA KUFANYA KAZI barabara zinawekewa Almasi na Tanzanite na kuzibiwa kingo za vioo na voyoyozi kuwekwa...yaani Mitaa ina baridi kama MAJUUU bila koti la maana au sweta huwezi tembea Darisalama ya sasa!

    Wa Majuu na Madiaspora fanyeni haraka mrudishe Pasipoti zenu za huko mrudi nyumbani haraka!!!

    Mkifika hatuwezi kuwachomea kwa Uhamiaji, nini mngali ni wandugu zetu!

    ReplyDelete
  13. Mologolo Lodi.

    ReplyDelete
  14. Ankal hii teknolojia ya kutumia saruji na zege hapo kwenye barabara ya Morogoro nimeipenda na itakuwa vema iwapo TAMISEMI wataichukua kwa ajili ya kuboresha barabara zetu zilizopo chini ya mamlaka za serikali za mitaa.TAMISEMI wawatume wahandisi wa miji,manispaa na majiji wakajifunze teknolijia hiyo ili kero ya barabara iwe ni historia nchini TANZANIA.

    ReplyDelete
  15. Huo mtaa mmoja upo manzese uzuri kama sikosei au huo mtaa upo tandika muembe yanga

    ReplyDelete
  16. Mdau wa 16 anony wa Sat Jan 12, 02:11:00 pm 2013

    ...Hilo ni jamvi la maandalizi ili Mabasi yaendayo kasi (DART) yapite, kama unakaa Ubongo ukiwa unakuja Kati kati ya Jiji utaanza kuona matunda ya mwanzo ya Mradi huu ni vile badala ya kugombania mabasi yenye mabati ya kutu sasa utapanda mchuma wa DART (Mabasi yaendayo Kasi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...