Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika
la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, kama ishara ya
uzinduzi mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka Ubungo Dar es Salaam
mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la
Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni
Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuzindua mradi wa Njia ya Pili
ya Umeme,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na
Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana
katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Hiki ni Kituo kikuu cha Umeme cha Mtoni Unguja.ambacho
tayari Mradi wake uliofadhiliwa na MCC Marekani umezinduliwa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,kwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium
Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, pia Balozi wa Marekani Nchini
Tanzania ALfonso Lenhardt, alihudhuria katika uzinduzi
huo,utakaochukua Ukubwa wa Kilowati 100.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la
‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,(katikati) na Balozi wa
Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt,wakipata maelezo ya
kiutendaji kazi katika kituo kikuu cha umeme kutoka Ubungo Dar es
Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la
Marekani,kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali,(kushoto)
baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...