Na Genofeva Matemu _MAELEZO

Shirikisho la Wakurugenzi wa Taasisi zinazoendesha Mashtaka wa Nchi za Afrika Mashariki wamekutana nchini Tanzania kwa ajili kupitia upya Katiba yao ili kuimarisha umoja wao. 
 Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Shirikisho hilo Dk. Eliezer Mbuki Feleshi wakati wa mkutano na waandishi wa habari. 
Dkt Feleshi, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano,  alisema kuwa wakati wa mkutano wao watazungumzia mikakati ya kimaendeleo ya shirikisho lao pamoja na kupitia katiba ya shirikisho ili kuweza kuifanya iwe na uzito katika utekelezaji wa majukumu yao na ya Shirikisho hilo. 
 Mambo mengine yaliyokusudiwa kuzungumziwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala ya uanachama, nafasi ya shirikisho kwenye mashirikisho mengine na namna ya kuongeza rasilimali watu kwenye shirikisho hilo. 
 Dkt. Feleshi alisema kuwa shirikisho hilo liliundwa mwaka 2009 ambapo mwaka 2010 lilianza kutekeleza majukumu yake ili kuleta amani, umoja na utulivu Afrika Mashariki. “Malengo yetu ya kuungani ni pamoja na kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha kuna umoja amani na utulivu ndani na nje ya nchi zetu,” amesema DK. Feleshi. 
 Aliongeza kuwa hadi hivi sasa Shirikisho limeweza kufanya kazi kwenye vuguvugu la watu waliorusha bomu Uganda, masuala ya uharamia Kenya, pamoja na kuwasaidia madereva kutoka Tanzania waliopata waliokuwa wamekamatwa nchini Burundi ambapo baada ya mawasiliano madereva hao waliweza kuachiwa. 
 Kuhusu changamoto Dk. Feleshi alisema kuwa changamoto zipo nyingi ikiwemo kuchelewa kupata taarifa, kuchukua muda mrefu kushughulikia kesi, na kupata kesi nyingi kwa wakati mmoja inayopelekea kushindwa kuzimaliza wakati muafaka. Shirikisho hilo limehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Eliezer Mbuki Feleshi ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Kenya Mhe. Keriako Tobiko na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Uganda Mhe. Richard Buteera. 
 Wengine ni Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Rwanda Mhe. Martin Ngoga, pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Valentine Bagorikunda
Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakurugenzi wa Mashataka wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashitaka wa Tanzania Dkt. Eliezer  Feleshi (kushoto) akiongea na wanahabari akiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka wa  Kenya , Mhe Keriako Tobiko leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Mkutano wa Wakurugenzi wa Mashtaka wa  Afrika Mashariki  Dkt, Eliezer  Feleshi (kulia) akiwa pamoja na wajumbe wenzake wa mkutano huo leo katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Chini wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2013

    hili sasa ni kero za muungano, inakuwaje suala la ukurugenzi wa mashtaka sio katika masuala ya muungano lakini hatuoni uwakilishi wa mkurugenzi wa mashtaka kutoka Zanzibar?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2013

    I just liked the background of the photo.......beautiful

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...