Muuguzi na Mnasihi wa CCBRT Theodola Millinga akielimisha wakazi wa Geita kuhusu fistula na namna ya kupata matibabu yake bila malipo kwenye hospitali ya CCBRT kupitia ufadhili wa Vodacom na Vodafone ya Uingereza. Zoezi hilo ni sehemu ya kampeni ya kusambaza ujumbe wa "Fistula inatibika, jitokeze upate matibabu bila ya malipo inayondelea mikoani kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone ikishirikiana na CCBRT.
Mkuu wa Mkoa wa Geira Said Magalula(katikati), Balozi wa Chapa Vodacom Mwana FA na Meneja Uhusiano wa Mambo ya nje wa Vodacom Salum Mwalim wakifurahia moja ya tukio wakati wa kampeni ya kuelimisha wakazi wa Geita kuhusu fistula na kufikisha ujumbe wa "Fistula inatibika, jitokeze upate matibabu bilaya malipo" liliondeshwa mjini Geita ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea siku ya fistula duniani Mei 23. Vodacom na Vodafone hufadhili matibabu kwa wanawake wenye fistula kwenye hospitali ya CCBRT.
Shuhuda wa fistula akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoteseka na fistula kwa mika mine kabla ya Vodacom kufadhili matibabu yake kwenye hospitali ya CCBRT. Ushuhuda huo ulitolewa wakti wa kampeni ya kuelimisha wakazi wa Geita kuhus fistula na kufikisha ujumbe wa "Fistula inatibika jitokeza upate matibabu bila ya malipo.
Balozi wa Chapa Vodacom Mwana FA akiwahamasisha wakazi wa Geita kuunga mkono kampeni ya kumaliza tatizo la fistula ifikapo mwaka 2016 inayofadhiliwa na Vodacom an Vodafone ya Uingereza kupitia hospitali ya CCBRT.
Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA akichana mistari mbele ya wakazi wa Mji wa Geita waliofika katika kampeni ya uelimishaji umma kuhusu fistula na kusambaza ujumbe wa "fistula inatibika, jitokeze upate matibabu bila ua malipo". Mwana FA yupo kwenye msafara wa kueneza ujumbe huo kw amikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa ufadhili wa Vodacom.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Said Mgalula akimakbidhi kipaza sauti Balozi wa Vodacom Msanii Mwana FA ili awashushie mistari wakazi wa mji huo waliojitokeze kwenye kampeni ya uelimishaji jamii kuhusu fistula na kwamba matibabu yake yanapatikana bila malipo kwenye hospitali ya CCBRT kwa gharama za Vodacom na Vodafone ya Uingereza.
Meneja wa Vodacom Mwanza Victoria na mwenzake wa Misungwi Gift wakihifadhi nambari maalum ya kupiga bure 0800752227 kwa masuala yoyote yanayohusu fistula baada ya kutangazwa kwenye kampeni ya kuwaelimsisha wakazi wa mji wa Geita kuelekea kilele cha siku ya fistula duniani Mei 23. Nambari hiyo ni kwa wateja wa Vodacom pekee.Vodacom na Vodafone ya Uingereza hugharamia matibabu bila malipo kwa wagonjwa wote wa fistula wanaoitibiwa katika hospitali ya CCBRT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2013

    jamani vodacom hamasisha wanaume wasiwatelekeze wake zao wanapopata matatizo ya fistula. Washirikiane nao kupata ufumbuzi.

    Wanaume wote, mkewe akipata tatizo hili hutengwa, hufukuzwa na familia ya mwanamme. Huu sio ubinadamu. Hasa mawifi na wakwe ndio humshawishi ndugu yao kuachana na mke.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2013

    Ina maana JD ndio ameshanyang'anywa na huu ubalozi wa Fistula? Duh jamaa wabaya...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...